“The chief task in life is simply this: to identify and separate matters so that I can say clearly to myself which are externals not under my control, and which have to do with the choices I actually control. Where then do I look for good and evil? Not to uncontrollable externals, but within myself to the choices that are my own . . .” —EPICTETUS, DISCOURSES, 2.5.4–5
Hongera sana mwanamafanikio kwa nafasi hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuuanza mwaka 2019 tukiwa na hamasa na nguvu kubwa ya kuendelea kufanya makubwa kama tulivyopanga kwenye mwaka wetu wa mafanikio 2018/2019.
Tunapaswa kuianza siku hii kwa shukrani kubwa sana, kwa sababu siyo kwa nguvu waka ujanja wetu tumeweza kuiona, bali kwa upendeleo wa hali ya juu sana.
Na njia pekee ya kulipa upendeleo huu ni kuitumia vizuri siku hii na kuweza kupiga hatua kubwa sana leo na kila siku.
Mwongozo wetu wa maisha ya mafanikio 2019 ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA na msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA.
Kwa mwongozo na msingi huu, tunayo nafasi ya kufanya makubwa sana leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari UDHIBITI NA UCHAGUZI…
Mambo yanayotokea kwenye maisha yetu yamegawanyika kwenye mambo tunayoweza kuyadhibiti na mambo tusiyoweza kuyadhibiti.
Na jukumu letu kubwa kwenye maisha ni kuweza kuyatenganisha mambo haya na kuchagua kuchukua hatua sahihi.
Mambo ambayo hatuwezi kuyadhibiti ni yale yaliyo nje ya uwezo wetu, na hivyo kuhangaika nayo ni kupoteza muda na nguvu.
Mfano kama umejikuta kwenye foleni wakati unawahi mahali, hata uchukie na kupiga kelele kiasi gani, haitasaidia foleni kwenda kasi. Huwezi kuwalazimisha watu wakupende au wafikirie kama unavyotaka wewe. Kama umezaliwa mfupi au mrefu sana, hakuna kiwango cha kutamani ungekuwa tofauti kitakachokusaidia kubadilika.
Mambo yote ambayo maamuzi yake yapo nje yako, huwezi kuyadhibiti na usiruhusu yapoteze muda wako, yakopee kama yalivyo na songa mbele.
Mambo ambayo tunaweza kuyadhibiti ni yale mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wetu, fikra zetu, maneno yetu, tabia zetu na matendo yetu. Ukiweka nguvu zako katika kuyaboresha maeneo hayo, utaweza kuwa na maisha bora sana.
Chagua leo kuhangaika na yale mambo ambayo yako ndani ya uwezo wako, na yale yaliyo nje ya uwezo wako, yasichukue hata dakika yako moja, maana hakuna unachoweza kufanya kuyabadili, hivyo dakika unayoweka hapo unaipoteza.
Ukawe na siku bora sana leo rafiki, siku ya kuweza kutofautisha yaliyo ndani ya uwezo wako na kuyafanyia kazi na yale yaliyo nje ya uwezo wako na kuachana nayo.
#MaishaYaUstoa, #MaishaNiKuchagua, #SumbukaNaKilichoNdaniYaUwezoWako
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha