Rafiki yangu mpendwa,

Nianze kwa kukushukuru kwa namna ambavyo umeendelea kuwa pamoja na mimi katika safari hii ya mafanikio makubwa.

Kama umekuwa unafuatilia na kusoma maarifa ninayokushirikisha kila siku, naamini kuna kitu kikubwa ndani yako kinakusukuma ili ufanikiwe zaidi.

Na kama unachukua hatua baada ya kujifunza, nina imani kubwa kwamba utaweza kufika kokote unakotaka kufika.

Msingi wa yote ninayofanya upo kwenye imani kwamba maarifa sahihi ndiyo ufunguo pekee wa maisha bora na mafanikio. Kwamba chochote tunachotaka tunaweza kukipata kama tukiwa na maarifa sahihi na kuchukua hatua kupitia maarifa hayo.

Ninaamini sana hili kwa sababu nimeona matokeo yake kwenye maisha yangu, mara zote ambazo nimekuwa nakwama ambacho kimekuwa kinanikwamua ni maarifa sahihi na kuchukua hatua kwenye maarifa hayo.

Na ndiyo maana kanuni kuu ya KISIMA CHA MAARIFA ni hii; MAARIFA SAHIHI + KUCHUKUA HATUA KUBWA = MAFANIKIO MAKUBWA.

SAMSUNG CAMERA PICTURES
SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2017

Rafiki, kwenye makala hii ya leo nakwenda kukushirikisha mabadiliko makubwa kwenye bidhaa za maarifa na ukocha ninazotoa, ili tuweze kwenda pamoja vizuri na kila mmoja aweze kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yake.

Kwanza kabisa utaona nimetumia neno BIDHAA na siyo HUDUMA kama ambavyo nimekuwa natumia siku za nyuma na wengi walivyozoea. Nageuza yale yote ninayofanya kutoka kwenye huduma na kwenda kwenye bidhaa, ili kuweza kuendesha vizuri na watu kunufaika pia.

Yafuatayo ni mabadiliko kwenye bidhaa ninazotoa.

Ili kuweza kupeleka muda na nguvu zangu sehemu sahihi ambayo itakuwa na manufaa makubwa, nimepunguza sana mambo ambayo nimekuwa nafanya. Kwa sasa bidhaa kuu ninazotoa zinakuwa nne (04) pekee na itakuwa kama ifuatavyo.

  1. AMKA MTANZANIA NA EMAIL.

Kila siku kutakuwa na makala nzuri za mafunzo na hamasa ambazo zitawekea kwenye mtandao wa AMKA MTANZANIA pamoja na kutumwa kwenye email. Maarifa haya ni bure na yataendelea kuwa bure kabisa. Hutahitaji kulipia chochote.

Pamoja na maarifa haya kuwa bure, yataendelea kuwa ya thamani kubwa sana kiasi kwamba ukiyaweka kwenye matendo utaweza kupiga hatua kubwa sana.

Kila siku tembelea www.amkamtanzania.com kujifunza. Pia hakikisha umejiandikisha kwenye mfumo wetu wa email ili uweze kupokea email za mafunzo kila siku. Kujiandikisha fungua kiungo hiki; http://eepurl.com/dDZHvL

  1. VITABU VILIVYOCHAPWA.

Kila mwaka nitachapa angalau vitabu viwili. Kitabu kimoja kitatokana na makala za TANO ZA JUMA za mwaka mzima, ambapo kitabu hiki kitakusanya maarifa haya mengi na kila mmoja wetu aweze kuyasoma na kufanyia kazi. Kitabu cha pili kitatokana na moja ya semina ambazo tutakuwa tumejifunza kwa njia ya mtandao.

Bei ya vitabu itategemea wakati kitabu kinatoka, lakini kwa sehemu kubwa kitakuwa tsh elfu 10 na kitabu kikubwa tsh elfu 30. Bei hizi zinaweza kubadilika kulingana na wakati kitabu kimechapwa.

  1. CHANNEL YA TANO ZA JUMA.

Kama unapenda kusoma vitabu na kupata uchambuzi wa kina wa vitabu basi nina bidhaa hii ya channel ya TANO ZA JUMA. Kupitia channel hii unapata uchambuzi wa vitabu pamoja na vitabu vyenyewe. Kwa kujiunga na channel hii, utaweza kujisukuma kusoma vitabu zaidi kwenye maisha yako.

Gharama za kujiunga na channel hii ni tsh elfu moja kwa wiki ambayo utalipa kila wiki, au elfu 3 kwa mwezi ambayo utalipa kila mwezi, au elfu 30 kila mwaka ambapo utalipa kila mwaka. Wiki ya kwanza ya kujiunga na channel hii ni bure, hivyo una wiki nzima ya kupima kama channel hii ni bora kwako, na baada ya hapo unachagua kuendelea kujifunza au kuondoka.

Karibu sana kwenye channel ya TANO ZA JUMA hapa utajifunza na kupata hamasa ya kusoma vitabu zaidi.

  1. KISIMA CHA MAARIFA.

Bidhaa ya nne ya maarifa na ukocha ninayotoa ni KISIMA CHA MAARIFA. Hii ndiyo huduma kuu ambayo mtu yeyote makini na aliyejitoa kweli kufanikiwa anapaswa kujiunga nayo ili aweze kufikia mafanikio makubwa.

Hii ndiyo huduma ya kwanza ambayo kila anayetaka kujifunza zaidi kupitia kazi zangu anapaswa kujiunga nayo.

Kila anayetaka ushauri na hata ukocha kutoka kwangu, anapaswa kwanza kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ndiyo ngazi ya kwanza ambayo mtu anapaswa kuipanda ili twende pamoja kwenye safari hii ya mafanikio. Naweza kusema pia kwamba hii ndiyo tiketi ambayo mtu anapaswa kuwa nayo ili tuwe karibu kwenye safari hii ya mafanikio.

KISIMA CHA MAAARIFA ni bidhaa ya kujiunga na kulipa ada ya mwaka mzima ambao unakuwa unatumia bidhaa hii. Gharama za kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA kwa sasa ni tsh laki moja (100,000/=) ambayo inalipwa kwa mara moja na kulipwa tena mwaka unapoisha tangu mtu alipolipa. Ada hii inabadilika kadiri muda unavyokwenda.

Ada hiyo ni kubwa kwa wengi, lakini ni ndogo mno ukilinganisha na manufaa utakayopata kwa kutumia bidhaa hiyo ya KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama bado hujaanza kutumia bidhaa hii ambayo ni bora sana kwa mafanikio yako, unajichelewesha, jiunge na uanze kunufaika sasa.

SAMSUNG CAMERA PICTURES
SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018

FAIDA KUBWA TANO ZA KUJIUNGA NA KISIMA CHA MAARIFA.

Kama ambavyo nimekushirikisha hapo juu, KISIMA CHA MAARIFA ndiyo bidhaa kuu ya mafanikio ninayotoa. Ndiyo bidhaa ambayo nimeweka nguvu zangu nyingi kuhakikisha kila anayeitumia ananufaika kweli.

Zifuatazo ni faida tano kubwa za kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

  1. MAFUNZO YA KILA SIKU, KILA JUMA SEMINA KWA NJIA YA MTANDAO.

Unapojiunga na KISIMA CHA MAARIFA, kila siku unapata mafunzo bora sana yatakayokusukuma kuchukua hatua zaidi ili kufanikiwa.

Kwanza kabisa unaianza siku kwa tafakari, ambayo inakufanya ufikiri tofauti na kukuondoa kwenye msongo pamoja na kukupa hamasa ya kupiga hatua zaidi.

Pili unapata makala ya KURASA ZA MAFANIKIO, hizi ni makala fupi zenye ujumbe muhimu sana kuhusu safari ya mafanikio.

Tatu unapata mjadala wa pamoja na wale ambao wapo kwenye safari ya mafanikio kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA.

Nne unapata darasa la juma, ambapo kwa baadhi ya majuma tunakuwa na darasa la mambo yanayohusu mafanikio au ushuhuda kutoka kwa mwanamafanikio mwenzetu.

Tano unapata nafasi ya kushiriki semina mbili zinazoendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap mara mbili kwa mwaka. Hizi ni semina zinazokupa maarifa na hamasa ya kuchukua hatua na kufanikiwa zaidi.

Pia kila mwezi unapata maswali ya kujifanyia tathmini ili kujua pale ulipo, na kule unakokwenda. Maswali haya yanakusaidia kujitambua na kuona wapi unalegalega ili kuweza kupiga hatua na kufanikiwa zaidi.

  1. KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA pia unapata nafasi ya kuwa mwanachama wa KLABU YA KISIMA CHA MAARIFA. Hizi ni klabu za mafanikio ambapo mnakutana ana kwa ana wale wote mliopo eneo la karibu, ndani ya mkoa mmoja au wilaya moja.

Kwa kuwa ndani ya klabu hizi, unapata nafasi ya kujifunza na kuhamasika kutoka kwa wengine pia.

Kila mwezi mnakutana kama klabu mara moja, ambapo mnashirikishana maarifa ya kitabu ambacho kila mmoja amesoma, mnashirikishana mipango ambayo kila mmoja amefanyia kazi, changamoto alizokutana nazo na mipango ya mwezi unaofuata.

Pia kwa kuwa kwenye klabu hizi mnapata nafasi ya kutembeleana na kujifunza pamoja na kushauriana zaidi.

Klabu pia zitakuwa zinafanya shughuli mbalimbali za kijamii kama kutoa misaada kwa wenye uhitaji, kuboresha mazingira na huduma nyingine za kijamii kama elimu na afya.

Muhimu zaidi, klabu hizi zitakuwa zinatembelewa na Kocha Dr Makirita Amani mara kwa mara ili kutoa mafunzo zaidi na kufuatilia maendeleo ya kila mmoja wetu.

Kwa kifupi, kuwa kwenye KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ni moja ya kitu bora kabisa unachoweza kufanya kwenye maisha yako na kikakulipa sana.

  1. SEMINA YA KUKUTANA ANA KWA ANA.

Kila mwaka tunakuwa na semina kubwa ya kukutana ana kwa ana. Semina hii huwa inafanyika mara moja tu kwa mwaka na wanamafanikio kutoka sehemu mbalimbali za nchi pamoja na nje ya nchi tunakutana kujifunza na kuhamasika ili kuendelea na safari hii ya mafanikio.

Kwenye semina hizi, kunakuwa na mafunzo bora kabisa ya mafanikio. Lakini pia kitu kikubwa unachopata kwenye semina hii ni kusikia hadithi za wanamafanikio wengine ambao wameweza kutoka chini na kupiga hatua zaidi kwenye maisha yao.

Faida kubwa pia ya kushiriki semina hizi ni kukuza mtandao wako wa mafanikio. Maana kwenye semina hizi unakutana na watu mbalimbali, hivyo wapo ambao utaweza kujifunza zaidi kwao na wengine ukashirikiana nao kwenye kazi au biashara unazofanya.

Gharama za kushiriki semina hii ya ana kwa ana inategemea eneo inapofanyika na wakati pia. Lakini mara nyingi imekuwa tsh laki moja (100,000/=), ada hiyo inabadilika kulingana na wakati na mazingira.

  1. BIDHAA YA UKOCHA YA GAME CHANGERS.

GAME CHANGERS ni bidhaa ya ukocha ambayo unajiunga na kufanyia kazi eneo moja la maisha yako kwa siku 30. Hizi zinakuwa siku 30 za mabadiliko makubwa kwenye maisha yako. Siku hizo 30 unaishi kwa namna ambayo hujawahi kuishi kwenye maisha yako na hivyo kuweza kutengeneza matokeo ambayo hujawahi kupata.

Hizi zinakuwa siku 30 za kutengeneza msingi wa tofauti kwenye safari yako ya mafanikio.

Bidhaa hii inapatikana mara 4 pekee kwa mwaka, na kwa wakati mmoja inachukua washiriki watano tu. Bidhaa hii inaleta pamoja nguvu ya ukocha pamoja na nguvu ya wale wanaokuzunguka. Kwa sababu kila juma tunakuwa na simu ya pamoja kwa washiriki wote pamoja na kocha, hivyo unajifunza kutoka kwa kocha na kutoka kwa wengine pia.

Hii ni huduma muhimu sana kwa wale ambao wanataka kuleta mabadiliko makubwa kwenye maisha yao, kwa siku 30 za kushiriki bidhaa hii, zitakujengea msingi mkubwa sana ambao utakuwezesha kuwa na maisha bora na ya mafanikio.

Gharama za kupata bidhaa hii ni tsh laki tatu (300,000/=) ambayo inalipwa mara moja kabla ya kuanza kwa msimu wa GAME CHANGERS. Ada hii itabadilika kulingana na muda unavyokwenda.

  1. BIDHAA YA UKOCHA YA LEVEL UP.

Bidhaa nyingine ya ukocha ni ya LEVEL UP. Hii ni bidhaa maalumu ya ukocha kwa wale ambao tayari wana biashara wanazoziendesha.

Biashara zimekuwa changamoto kwa watu wengi, kwa sababu wamekuwa wanaziendesha kwa mazoea. Hivyo biashara zimekuwa hazikui na nyingi kufa. Lakini tafiti zinaonesha kuendesha biashara kwa mfumo sahihi, pamoja na kuendelea kujifunza kila siku kunaiwezesha biashara kukua sana.

Hivyo bidhaa hii ya LEVEL UP inasaidia wafanyabiashara kukuza biashara zao, kwenda kwenye ngazi ya juu zaidi.

Kwa kuwa kwenye LEVEL UP, unapata mafunzo ya biashara, usimamizi wa karibu kwa kutuma namba zako za kibiashara kila wiki. Lakini pia unapata nafasi ya kuwa na maongezi na Kocha kila mwezi, kupitia yale unayofanyia kazi, changamoto unazokutana nazo pamoja na mipango ya baadaye.

Bidhaa hii unajiunga kwa mwaka mzima na ada unalipa kila mwezi. Bidhaa hii ina uwezo wa kuchukua watu 12 pekee kwa mwaka. Hivyo nafasi zake ni adimu sana ukilinganisha na uhitaji wake.

Gharama za kupata bidhaa hii ni ada ya tsh laki moja (100,000/=) kila mwezi. Ada hii itabadilika kulingana na muda unavyokwenda.

Karibu sana ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwani ukishajiunga, una uwanja mpana sana wa kujifunza na kuwa karibu na Kocha na utaweza kupiga hatua zaidi kuelekea kwenye mafanikio makubwa.

Ili kupata bidhaa yoyote iliyoelezwa hapa, wasiliana na kocha kwa namba 0717 396 253 au 0755 953 887 kwa simu au ujumbe wa kawaida au kwa ujumbe wa wasap namba 0717 396 253 na utaelezwa upatikanaji wa nafasi kwenye bidhaa unayohitaji pamoja na utaratibu wa malipo.

Karibu sana rafiki tuwe pamoja kwenye safari hii ya mafanikio. Nimekuwa najifunza sana kupitia wale ninaofanya nao kazi, na nimegundua kufanya kazi kwa karibu na watu wachache kunaleta matokeo makubwa sana. Ndiyo maana unaona bidhaa ya KISIMA CHA MAARIFA inalenga kufanya kazi na watu wachache. Nafasi kwenye bidhaa hii ya KISIMA CHA MAARIFA ni chache kuliko uhitaji wa watu, hivyo kama umesoma hapa na kuona ni kitu unachohitaji kweli basi nakushauri usisite, chukua hatua sasa na utajishukuru sana baadaye.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Rafiki, mwezi julai mwaka huu 2019 tutakuwa na semina kwa njia ya mtandao wa wasapa inayohusu kutengeneza mfumo wa kuendesha biashara yenye mafanikio. Biashara ambayo itakupa wewe mmiliki uhuru kamili na kukuwezesha kuwa na kipato kisichokuwa na ukomo.

Ili uweze kushiriki semina hii unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAAARIFA kabla ya tarehe 01/07/2019. Kama umekuwa kwenye biashara na inakunyima uhuru, au kama unapanga kuingia kwenye biashara basi hii siyo semina ya wewe kuikosa.

Chukua hatua sasa ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA unufaike na semina hii na hata semina za nyuma pia.

Kujiunga tuma ada ya mwaka ambayo ni shilingi laki moja (100,000/=) kwenda namba 0717396253 au 0755953887 kisha tuma ujumbe kwenye wasap namba 0717396253 wenye majina yako na kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa.

Kumbuka ukijiunga kwenye KISIMA CHA MAARIFA kwa ajili ya semina hii, unapata faida zote tano za KISIMA CHA MAARIFA nilizokushirikisha hapo juu.

Karibu sana rafiki yangu, usikose semina hii muhimu kwa ukuaji wa biashara yako, lakini pia usikose manufaa makubwa ya kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Kama hujapata maelezo zaidi kuhusu semina hii unaweza kuyapata hapa;

Kuhusu semina; SEMINA; Mfumo Wa Kuendesha Biashara Yenye Mafanikio.

Masomo yatakayofundishwa; Haya Ndiyo Masomo Kumi (10) Utakayojifunza Kwenye Semina Ya Kutengeneza Mfumo Wa Biashara.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge