Rafiki yangu mpendwa,

Nachukua nafasi hii kukukaribisha kwenye uzinduzi wa vitabu viwili vipya vya Kocha Dr Makirita Amani.

Vitabu hivyo ni ELIMU YA MSINGI YA FEDHA ambacho kinakupa mafunzo yote muhimu kuhusu fedha, ambayo hujawahi kufundishwa popote. Na kitabu cha pili ni TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA ambao ni mkusanyiko wa uchambuzi wa vitabu 50 vya mafanikio, siri 50 za mafanikio, makala bora za mafanikio, mafunzo ya kifedha na tafakari za kubadili mtazamo wako.

Tangazo la uzinduzi vitabu.jpeg

Uzinduzi wa vitabu hivi utafanyika jumamosi ya wiki hii, tarehe 03/08/2019 kuanzia saa nane kamili mchana mpaka saa 12 kamili jioni.

Uzinduzi utafanyika kwenye hoteli ya Golden Park iliyopo Sinza Kumekucha Jijini Dar Es salaam.

Kushiriki uzinduzi huu unalipa ada ya tsh elfu 10 (10,000/=) kwa namba 0717396253 au 0755953887 mapema ili kujiwekea nafasi yako ya ushiriki.

WANENAJI KWENYE UZINDUZI WA VITABU.

Katika uzinduzi huu wa vitabu kutakuwa na wanenaji wawili;

MNENAJI WA KWANZA; KOCHA DR MAKIRITA AMANI.

Dr Makirita Amani, ni daktari wa binadamu, kocha wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali. Ndiye mwanzilishi na mwendeshaji wa mitandao ya AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA. Pia ndiye mwandishi wa vitabu viwili vinavyokwenda kuzinduliwa.

Katika uzinduzi huu Dr Makirita atafundisha masomo yafuatayo;

  1. Jinsi usomaji wa vitabu unavyoweza kubadili maisha yako. Hapa Dr Makirita atashirikisha historia fupi ya maisha yake jinsi ambavyo usomaji wa vitabu umeweza kuyabadili maisha yake.
  2. Jinsi ya kujijengea tabia ya usomaji wa vitabu. Hapa Dr Makirita anafundisha jinsi ambavyo kila mtu anaweza kujijengea tabia ya usomaji wa vitabu. Kwa wale wanaosema hawana muda wa kusoma vitabu au wakisoma wanasahau, hapa watapata suluhisho. Lakini pia kwa wale wanaosema hawawezi kupata vitabu vya kusoma, watajifunza njia rahisi za kupata vitabu wanavyotaka.
  3. Kuweka sahihi vitabu. Dr Makirita pia atapata nafasi ya kuweka sahihi kwenye vitabu vya wale walionunua mapema na watakaonunua siku ya uzinduzi wa vitabu hivyo.

MNENAJI WA PILI; PAUL MASATU.

Paul Masatu ni Mfanyabiashara, mwalimu na kocha  wa stadi za maisha na mzungumzaji mhamasishaji.

Katika uzinduzi wa vitabu, Pau atafundisha;

  1. Maarifa ni ufunguo wa maendeleo yako binafsi. Hapa tutajifunza jinsi ambavyo maarifa yanachangia kwenye maendeleo yako binafsi na kama unataka kufanikiwa zaidi kwenye maisha kwa nini unapaswa kufanya uwekezaji wa maarifa kwanza.

Rafiki, utajifunza mambo mengi sana kuhusu usomaji wa vitabu na uwekezaji kwenye maarifa kwa ujumla katika semina hii ya uzinduzi wa vitabu. Ni semina ambayo hupaswi kuikosa kwa namna yoyote ile.

HATUA ZA KUCHUKUA SASA ILI USIKOSE UZINDUZI WA VITABU HIVI.

Rafiki, kama nilivyokueleza hapo juu, uzinduzi huu wa vitabu utakuwa na maarifa mengi na yatakayokusaidia kupiga hatua sana. Hivyo hupaswi kukosa kabisa.

Lakini pia nafasi za kushiriki uzinduzi huu ni chache, ukilinganisha na uhitaji.

Hivyo kama hutaki kukosa uzinduzi huu, chukua hatua ifuatayo sasa, hivi, siyo baadaye, bali sasa.

Tuma ujumbe wenye majina yako kamili, namba ya simu na maelezo kwamba utashiriki uzinduzi wa vitabu. Ujumbe utume kwenye namba 0717396253. Kwa kutuma ujumbe huu unakuwa umejiwekea nafasi ya kushiriki uzinduzi huu. Ni muhimu sana utume ujumbe huo sasa unaposoma hapa kama hutaki kukosa uzinduzi huu, kwa sababu nafasi ni chache.

MWISHO WA KULIPA ADA YA KUSHIRIKI.

Rafiki, kushiriki semina hii nzuri sana ya uzinduzi wa vitabu viwili, unapaswa kufanya uwekezaji wa tsh elfu 10 (10,000/=). Kwa uwekezaji huu mdogo utapata maarifa bora sana lakini pia utapata vitabu vyote viwili kwa bei ya punguzo.

Mwisho wa kulipa ada ya kushiriki semina ni tarehe 31/07/2019 na ada inalipwa kwa namba zifuatazo; 0755 953 887 au 0717 396 253, majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA.

Fanya malipo ya kushiriki semina hii ya uzinduzi kwa wakati ili upate nafasi hii adimu ya kujifunza kuhusu usomaji wa vitabu kwa maendeleo yako.

Nikutakie kila la kheri rafiki yangu na nikukaribishe sana kwenye uzinduzi wa vitabu vyetu vipya viwili, ili usikose nafasi hii, hakikisha unatuma ujumbe sasa wa kuweka nafasi yako ya kushiriki, wenye majina kamili, namba ya simu na maelezo kwamba utashiriki semina, kwenda namba 0717396253.

Karibu sana.

Kocha Dr. Makirita Amani

www.amkamtanzania.com/kocha