Rafiki yangu mpendwa,

Kumekuwa na utani mwingi sana unaoendelea kwamba kila kitu kwenye maisha kinahitaji ‘connection’. Kwamba hata kama kuna picha za uchi za watu maarufu zimevuja mitandaoni, ili uzipate unahitaji kuwa na ‘connection’.

Japo watu wanachukulia hili kama mzaha, na kwa namna ambayo haina manufaa kwao, lakini ukweli ni kwamba ‘connection’ ina mchango muhimu sana kwa mafanikio yako.

Sehemu kubwa ya mafanikio yako siyo unajua nini, bali unamjua nani. Unaweza kuwa unajua vitu vingi sana, lakini ukashindwa kupiga hatua kama hujakutana na watu sahihi wa kukuongoza au kukusaidia kuvuka vikwazo mbalimbali unavyokutana navyo kwenye safari yako ya mafanikio.

Nimekuwa nakuambia mara kwa mara kwamba kwenye mafanikio hakuna jeshi la mtu mmoja, hakuna anayeweza kusema ameanzia chini kabisa na kupambana yeye mwenyewe mpaka akafanikiwa.

connection.jpg

Lazima kuna nyakati ambazo mtu alipata msaada wa namna moja au nyingine kutoka kwa watu wengine. Inaweza kuwa ushauri, mwongozo na hata michango mbalimbali ambayo imemsaidia mtu kufanikiwa.

Lakini sasa, tumekuwa na changamoto kubwa kwenye jamii zetu. Sehemu kubwa ya wale wanaotuzunguka wanakuwa siyo watu wenye mchango bora kwa mafanikio yetu. Wengi hawaishi maisha ya kusaka mafanikio, wamekata tamaa na kukubali kuishi maisha ya kawaida. Kikubwa wanachoweza kufanya ni kujaribu kukurudisha nyuma ili usifanikiwe.

Sasa swali linakuja, kwa mazingira kama haya unawezaje kutengeneza ‘connection’ nzuri kwa mafanikio yako? Na jibu lipo wazi, ila kabla sijakupa jibu hilo, nikupe ushuhuda wa mwanamafanikio mwenzetu ambaye ameweza kunufaika sana na ‘connection’ alizopata.

Mimi leo napenda nitoe ushuhuda Na connection  niliyopata kwa kuhudhuria Semina za ana Kwa ana inayofanyika mara moja Kwa mwaka,

Licha ya kukutana na watu wengi kwenye semina hizo lakini leo kipekee kabisa naomba niwashukuru watu wawili ambao ni Mr Pascal Kasanda wa mpanda Na Mr Remod Kibona WA mpemba.

Watu hawa tuna fanya biashara zinazofanana Kwa baadhi ya bidhaa Na wamekuwa wananipa mawasiliano ya wafanyabiashara mbalimbali wanaouza bidhaa ninazo zihitaji Tena kwa bei rafiki. Nimekuwa nawasiliana nao muda mwingi Na nimeonana nao mara mbili kwenye semina na mwaka huu mungu akipenda tutaonana nao tena. Ahsanteni sana wanamafanikio wote. – Selemani Mbwambo.

WhatsApp Image 2019-09-18 at 05.49.19.jpeg

Kama anavyotushirikisha mwanamafanikio mwenzetu Selemani Mbwambo hapo juu, njia bora kabisa ya kupata ‘connection’ nzuri kwako ni kuhudhuria matukio ambayo yanawakusanya pamoja wale watu wenye sifa unazozitaka.

Na kwa Tanzania, sehemu nzuri kwako kupata ‘connection’ zitakazokuwezesha kupiga hatua na kufanikiwa zaidi, ni kuwa eneo moja na watu ambao nao wana kiu ya kufanikiwa zaidi. Eneo hilo kwa sasa ni kwenye SEMINA ZA KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni kundi maalumu la watu ambao wana kiu kubwa ya mafanikio. Watu ambao wanajifunza kila siku na kuchukua hatua kubwa ili kufanikiwa zaidi kwenye maisha yao. Watu hawa wapo kwenye nyanja mbalimbali na wametapakaa nchi nzima ya Tanzania.

Mara moja kila mwaka, watu hawa huwa wanakusanyika pamoja kwenye SEMINA YA MWAKA, ambayo imejaa mafunzo na hamasa mbalimbali za mafanikio. Kwenye semina hizi kunakuwa na masomo ya mafanikio, lakini pia kunakuwa na shuhuda mbalimbali za wale ambao wanapiga hatua kubwa zaidi za mafanikio kwenye maisha yao.

Na hapo sasa ndipo unapopaswa kuwepo wewe, kuzungukwa na watu hawa wengi ambao wana kiu kubwa ya mafanikio. Kwa kuwa na watu hawa, kuna faida nyingi unazipata, lakini kubwa kabisa ni hizi mbili;

Moja unaambukizwa hamasa ya mafanikio. Unapowaona na kuwasikia wenzako kwamba wameanzia chini na wanapambana na changamoto mbalimbali lakini hawakati tamaa, na wewe pia unapata moyo kwamba licha ya changamoto unazopitia, mafanikio yako mbele yako.

Mbili unapata taarifa sahihi za kukusaidia kwenye kazi au biashara yako. Hapa sasa  ndipo unapotengeneza ‘connection’, kwa kukutana na wale wanaofanya kazi au biashara inayofanana na yako, unaweza kujifunza mengi kutoka kwa wengine na hata kupata siri za ndani ambazo wengi huwa hawazitoi waziwazi.

Mwaka huu 2019, SEMINA YETU YA KISIMA CHA MAARIFA itakuwa siku ya jumapili ya tarehe 03/11/2019 na itafanyika jijini Dar Es Salaam. Ada ya kushiriki semina hii ni tsh 100,000/= (laki moja), ambayo unapaswa kuwa umeilipa mpaka kufikia tarehe 31/10/2019 ili kuweza kushiriki semina hii bora sana kwako.

Zipo nafasi za kulipa ada hiyo kwa awamu ili mpaka inapofika tarehe hiyo ya mwisho, uwe umeshakamilisha malipo yako na kupata nafasi ya kushiriki semina hii inayofanyika mara moja pekee kwa mwaka.

Wanamafanikio kutoka kila kona ya Tanzania wanakutana siku hiyo na kujifunza pamoja na kuhamasika pamoja. Usiseme tena huna ‘connection’, nimeshakupa siri ya wapi unaweza kupata connection hizi, kazi ni kwako sasa kuchukua hatua.

HATUA ZA KUCHUKUA LEO ILI USIKOSE SEMINA HII.

Rafiki, ili kuhakikisha hukosi semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, basi chukua hatua hii sasa, andika ujumbe wa kawaida au wasap na tuma kwenye namba 0717396253, ujumbe uwe na majina yako kamili, namba yako ya simu, barua pepe yako na maelezo kwamba utashiriki semina. Pia kwenye ujumbe huo eleza kama utalipa ada kwa siku, wiki, mwezi au mara moja, na tarehe utakayofanya hivyo.

Mfano wa ujumbe ni kama hivi; mimi Makirita Amani, simu; 0717396253, email; makirita@kisimachamaarifa.co.tz Nitashiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, ada nitalipa kila tarehe ya mwisho wa mwezi.

Chukua hatua hiyo sasa rafiki yangu ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kushiriki kwenye semina yetu ya KISIMA CHA MAARIFA mwaka 2019, kitu ambacho kitakupa msukumo mkubwa wa kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.

Asante sana rafiki yangu na nina uhakika tarehe 03/11/2019 tutakuwa pamoja kwenye semina, tuma ujumbe wako sasa wa kuthibitisha kushiriki ili usikose nafasi.

MUHIMU; Ili usisumbuke, thibitisha ushiriki wako mapema kwa kutuma ujumbe wenye majina yako, mawasiliano na mpango wako wa malipo.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha