Mpendwa rafiki yangu,

Wote tunajua kuwa watoto ni zawadi ya ndoa, hivyo basi, kila mmoja wetu anapokwenda kununua kitu kama vile jokofu au friji atapewa na kijitabu cha mwongozo jinsi ya kutumia. Lakini sisi binadamu pale tunapopata mtoto hatuna kitabu cha mwongozo kama vile unaponunua bidhaa nyingine.

Malezi ya mtoto ni kazi kama unavyoziona kazi nyingine. Kama mzazi unatakiwa kuwajibika katika malezi ya watoto. Unatakiwa kuwapa misingi sahihi ambayo itawaongoza kwenye maisha yao.

Unaposhindwa mzazi kumlea mtoto wako vizuri dunia itakusaidia kumfundisha adabu lakini kwa riba kubwa. Dunia haitombembeleza bali itamlea kikatili sana.

Je ni vitu gani mtoto anapaswa kuvijua kutoka kwa mzazi?

Wewe kama mzazi mtoto anapaswa kujua vitu hivi viwili kutoka kwako

Kujua vile ambavyo unavipenda katika malezi. Mtoto anatakiwa kujua kabisa kuwa mzazi anapenda moja mbili tatu. Mzazi anapenda tabia njema, anapenda kumuona mtoto akiwa namna hii  na mtoto akishajua kuwa mzazi wake ni mtu wa namna gani na yeye atajishepu kadiri ya mzazi anavyotaka awe. Mtoto akishajua baba unapenda nini naye atakuwa anafanya vile unavyopenda wewe na kuepuka vile ambavyo huvipendi.

Kujua vile ambavyo huvipendi. Mtoto anapaswa kujua wewe kama mzazi hupendi kutoka kwa mtoto wako. Ukianza kumjengea mtoto msingi vizuri kuwa huhitaji kufanya moja mbili tatu, ataanza kutii na kufanya vile unavyopenda kufanya.

Sasa inakuja ugumu pale ambapo mtoto hajui hata mzazi yuko upande gani, unakuta anafanya vile anavyojisikia yeye kufanya. Mtoto yoyote makini lazima hata mzazi wake atakuwa makini.

Tuwafundishe watoto namna ya kuvua samaki na siyo kuwapa samaki. Wafundishe watoto namna ya kuishi misingi bora na siyo maonesho tu.

Ukiwa na mwongozo mtoto ataufuata lakini kama mzazi huna mwongozo mtoto atakua hana cha kufuata , atakuwa hana mwelekeo, na mtoto asipokuwa na mwelekeo mwelekeo wowote utamchukua.

Hatua ya kuchukua leo; mzazi hakikisha unakuwa wazi kwa mtoto wako, ni vitu gani unavipenda na vitu gani huvipendi. Ikiwezekana mwandikie kabisa ili ajue na kuufuata kila siku.

Kwahiyo, binadamu tuna asili moja, tunaposetiwa kuwa watu wa namna fulani basi tunajikuta tu tunasetika. Hivyo ukiweza kumseti vizuri mtoto wako utakua umesaidia sana katika dunia hii ya leo ambayo kama siyo imara kuishi ni ngumu.

Makala hii imeandikwa na

Mwl. Deogratius Kessy, ambaye ni mwandishi, mwalimu na mjasiriamali. Unaweza pia kujifunza mengi kutoka kwake kupitia mafundisho anayoendelea kuyatoa kupitia mtandao wake wa  http://kessydeo.home.blog vitabu na kwenye klabu yake ya MIMI NI MSHINDI.  Karibu sana.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Mwl, Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com //kessydeoblog@gmail.com

Asante sana