Habari rafiki yangu mpendwa,

Kwa muda sasa nimekuwa nakupa taarifa kuhusu semina yetu ya KISIMA CHA MAARIFA 2019 ambayo itafanyika siku ya jumapili ya tarehe 03/11/2019. Hii ni semina ya mwaka ambayo inawakusanya pamoja wapenda mafanikio wote kutooa nchi nzima na hata nchi za jirani ili kuweza kujifunza na kuhamasika pamoja na kisha kwenda kuchukua hatua kwa mwaka mzima ili kufanikiwa zaidi.

SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2017
SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2017

Kumekuwa na maswali mbalimbali kuhusu semina hii, na moja ya swali ambalo limejirudia kwa wengi ni je mtu anaweza kushiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019 hata kama siyo mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA?

Jibu ni ndiyo, ipo nafasi kwa ambaye siyo mwanachama kushiriki semina hii. Semina hii inawalenga watu wote wenye kiu ya kupiga hatua na kufanikiwa zaidi kwenye maisha yao. Japokuwa watu wa aina hiyo ndiyo waliopo kwenye KISIMA CHA MAARIFA, wapoa ambao hawajaingia bado. Na kupitia semina, ndiyo wanaweza kujifunza vizuri kupitia wengine na hata kuchagua kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Hivyo kama wewe umekuwa mfuatiliaji wa kazi zangu, na umekuwa unapata vitu ambavyo vinakusaidia kupiga hatua kwenye maisha, nakualika tuwe pamoja siku ya tarehe 03/11/2019 kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019.

Kama ambavyo nimekushirikisha orodha ya wanenaji tisa, tunakwenda kujifunza mambo mengi sana ndani ya siku moja, ambayo tutaweza kuyatumia kwa mwaka mzima.

Pia unayo nafasi ya kuja na mtu wa karibu kwako, iwe ni mke au mume, mtoto wako, rafiki au jamaa. Kama kuna mtu wa karibu ambaye unaona anaweza kunufaika sana na mafunzo haya ya semina, basi ipo nafasi ya kuweza kushiriki naye kwa pamoja. Unachopaswa kufanya ni kumlipia mtu huyo ada ili na yeye apate nafasi ya kushiriki semina hii.

Rafiki, tuna siku moja pekee kwa mwaka mzima kukutana pamoja, kujifunza na kushirikishana hatua mbalimbali ambazo tunapiga ili kufanikiwa zaidi. Lakini pia kwenye semina ya mwaka huu, kutakuwa na kitu cha tofauti na miaka mingine, kwani utakwenda kuweka lengo moja utakalofanyia kazi kwa mwaka mzima na kila mwezi kushirikisha hatua unazopiga. Hili litakupa msukumo wa kuchukua hatua zaidi.

Ili kupata nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019, unapaswa kulipa ada ya kushiriki ambayo ni tsh laki moja (100,000/=). Ada inalipwa kwa njia ya MPESA; 0755 953 887 au TIGO PESA/ AIRTEL MONEY; 0717 396 253. Ukishafanya malipo tuma ujumbe wenye majina yako kamili na namba ya simu na maelezo kwamba umelipia semina. Ujumbe utume kwa njia ya wasap ili uweze kuweka kwenye kundi maalumu kwa ajili ya semina.

Rafiki, chukua hatua sasa ili uweze kupata nafasi hii nzuri ya kuwa pamoja na wanamafanikio kutoka nchi nzima, kujifunza, kuhamasika na kupata msukumo wa kuchukua hatua zaidi. Mwisho wa kulipa ili kupata nafasi ya kushiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019 ni tarehe 31/10/2019.

Kama utamlipia mtu wako wa karibu unayekuja naye, tuma majina yake kamili kama utaratibu unavyoeleza hapo juu.

Karibu sana rafiki yangu tuwe pamoja kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019, itakayofanyika tarehe 03/11/2019 jijini Dar es salaam. Kamilisha malipo yako ya ada ya kushiriki leo ili usikose nafasi hii ya kipekee.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,