“What reward should a good deed bring you? Only the joy you receive by performing it. And any other reward lessens the feeling of this joy.” – Leo Tolstoy

Zawadi unayoipata kwa kutenda wema ni ile furaha unayoipata wakati unatenda wema huo.
Pale unapojua unafanya kitu kizuri kwa ajili ya mwingine, kitu ambacho hakustahili wala kutegemea, unajisikia vizuri sana.

Zawadi hii hupotea pale unapotaka wema wako ujulikane na kila mtu.
Pale unapofanya wema siyo kwa ajili yako au ya unayemfanyia, bali kwa ajili ya kuonekana na wengine kwamba wanatenda wema.
Wema wowote unaoutenda ili kuonekana na wengine, haukupi ile furaha ya kutenda wema.
Unaishia kuwa kama biashara, ambayo wewe ndiye unayepata hasara.

Tenda wema kwa sababu ndiyo kitu sahihi kwako kufanya,
Na usipoteze muda wako kutaka kila mtu ajue umetenda wema,
Kama wewe ni mtu mwema, watu watajua hata kabla hujawaambia.

Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kutenda wema kama sehemu ya maisha yako na siyo kwa maonesho.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania