Mpendwa rafiki yangu,

Upendo ndiyo amri kuu ambayo kila mmoja wetu anaalikwa kuuishi katika maisha yake.
Tunaendelea kuishi vizuri kwa sababu ya kuishi upendo hata sisi kuwepo duniani ni upendo wake Mungiu mwenyewe. Hakuna aliyewahi kuomba kuzaliwa bali tumezaliwa kwa upendo wa asili.

Tunapojifunza mambo ya familia ni kwa sababu sisi wote tumezaliwa katika familia ambazo tunazo leo. Na katika familia huwa kuna watoto na ndiyo maana tunajifunza malezi ya watoto.

Watoto huwa wanajifunza sehemu kubwa ya makuzi yao kutoka kwa wazazi. Wanajifunza namna bora ya kuwa mama kutoka kwa mama na namna bora ya kuwa baba kutoka baba. Hata miito mingine chimbuko lake ni katika familia hivyo tukiweza kuwa na familia bora basi tutaweza kuwa na jamii bora.

Je ni namna gani tunaweza kufundisha upendo katika familia zetu?
Njia pekee na bora ambayo wazazi wanaweza kuwafundisha watoto upendo ni wazazi wenyewe kuishi upendo.
Wazazi wakipendana katika familia wale watoto wanavutwa na ule upendo wa wazazi.

Malezi ni vitendo na siyo nadharia, ukitaka watoto wako wajifunze upendo kirahisi basi nyie kama wazazi au walezi muwe wa kwanza kuishi upendo huo. Watoto wataiga upendo wenu kwa namna ambayo nyie wazazi mnaubiri upendo huo. Upendo unahubiriwa kwa matendo na siyo maneno.

Wazazi wakipendana katika familia watoto wanakuwa matajiri wa upendo lakini wakikosa upendo wanakuwa masikini wa upendo, mtu aliyekosa upendo katika familia yake anakuwa ni mtu aliyekosa vitu vingi sana.

Kila mzazi atambue kuwa akiwa na upendo na mwenzake haina haja hata ya kuhubiri kwa njia ya mdomo kwani watoto wanapenda injili inayohubiriwa na matendo kutoka kwa wale wanaoishi nao.

Pendaneni, upendo unaweza kumfanya kila mmoja wetu kuwa mshindi. Bila upendo hatuwezi kuwa washindi lakini tukiwa na upendo ushindi mkubwa utapatikana katika familia zetu.

Ishi ipasavyo wito ulio chagua kuuishi, kiasi kwamba hata wale wanaokuzunguka wavutiwe na wito wako. Na njia rahisi ya kuwavuta watu ni wewe kuhubiri upendo kwa njia ya matendo.

Hatua ya kuchukua leo; Wafundishe watoto wako upendo kwa nyie wazazi kuanza kuishi upendo wa kupendana nyie wenyewe kwanza kwa kuishi upendo watoto watajifunza kirahisi sana.

Hivyo basi, tumia mbinu hii rahisi kuhubiri upendo katika familia yako kwa nyie wazazi kuanza kupendana. Kama wazazi mnaishi kinyume na upendo usitegemee upendo kuonekana kwa watoto wako na familia yako kwa ujumla.

Makala hii imeandikwa na

Mwl. Deogratius Kessy, ambaye ni mwandishi, mwalimu na mjasiriamali. Unaweza pia kujifunza mengi kutoka kwake kupitia mafundisho anayoendelea kuyatoa kupitia mtandao wake wa  http://kessydeo.home.blog ,vitabu na kwenye klabu yake ya MIMI NI MSHINDI inayopatikana kwenye mtandao wa wasapu.  Karibu sana.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Mwl, Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com//kessydeoblog@gmail.com

Asante sana