Rafiki yangu mpendwa,

Dunia ya sasa ni kama kijiji, kitu chochote kinachotokea kwenye kona yoyote ile ya dunia, kinaleta athari kwa dunia nzima.

Na hilo tumeliona vizuri sana mwaka 2020 baada ya mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19 ulioanzia kwenye jimbo moja nchini China, kuweza kusambaa kwenye kila nchi duniani.

Japokuwa madhara ya ugonjwa yametofautiana kati ya nchi na nchi, kuna mapinduzi makubwa ya kiuchumi yamechochewa sana na mlipuko huu, ambayo kila mtu anapaswa kuyajua kwa sababu yanakwenda kuathiri sana maisha ya kila mtu.

Wataalamu wa uchumi na wanateknolojia wanasema Covid 19 imefanya vitu ambavyo vilikuwa vitokee miaka 10 ijayo, kutokea ndani ya mwaka mmoja. Yaani imechochea sana mabadiliko, vitu ambavyo watu, makampuni na hata nchi zilikuwa zinahofia kufanya, zimelazimika kufanya kutokana na mlipuko huo.

Moja ya vitu hivyo na ambacho kinakwenda kubadili kabisa soko la ajira na biashara ni kufanyia kazi nyumbani. Wakati wa mlipuko wa Covid, nchi nyingi ziliweka sheria ya karantini na hivyo watu walipaswa kukaa majumbani. Kutokana na uimara wa mtandao wa intaneti na aina ya kazi za wengi, makampuni makubwa yaliwataka wafanyakazi wake kufanyia kazi zao wakiwa nyumbani.

Hili la watu kufanyia kazi majumbani, limekuwa ombi na kilio cha wengi kwa miaka, ambapo watu walieleza kwamba kwa maendeleo ya teknolojia tuliyonayo sasa, hakuna tena haja ya watu kwenda kujikusanya eneo moja. Kwani mtu anaweza kufanyia kazi popote na akapimwa kwa kile alichozalisha na siyo kwa kuonekana eneo la kazi.

Makampuni mengi hayakuwa tayari kuchukua hatua hiyo, lakini baada ya mlipuko wa Covid 19 na kujaribu hilo, baadhi ya makampuni makubwa yanaeleza wazi kwamba sera ya kufanyia kazi nyumbani wataendelea nayo milele.

Ukisikia ule usemi kwamba ukionja asali utachonga mzinga ndiyo kilichotokea kwenye kufanya kazi nyumbani. Baada ya makampuni makubwa kujaribu hilo, yaliona manufaa ambayo awali hawakuwa wanayapata. Gharama za kuendesha biashara zinashuka huku ufanisi wa watu ukiongezeka maana hawapotezi muda mwingi kwenda na kurudi kazini.

Sasa kwa hili moja tu la watu kufanyia kazi nyumbani, linakuja na madhara mengi na makubwa.

Kwanza kabisa ni kushuka kwa thamani ya majengo ambayo makampuni yalikuwa yanapanga kwa ajili ya wafanyakazi wao kufanyia kazi.

Pili ni kupungua kwa nafasi za kazi maana kazi nyingi zinarahisishwa na teknolojia.

Tatu ni watu kupunguza kusafiri kwenda na kurudi kazini, kitu kitakachopunguza matumizi yao na hivyo baadhi ya biashara zilizokuwa zinawategemea watu hao kukosa wateja.

Hilo ni badiliko moja kubwa na ambalo linakuja na madhara mengi, yapo mengine mengi ambayo kila aliye makini na anayetaka kufanikiwa anapaswa kuyajua.

Hatua kubwa mbili za kuchukua.

Ili kuweza kukabiliana na mapinduzi haya makubwa yanayoendelea kutokea kwenye dunia kuna hatua mbili kubwa unazopaswa kuchukua.

Hatua ya kwanza ni kujitambua wewe mwenyewe, kujijua kiundani, kujua uimara na udhaifu wako ulipo na kisha kutumia uimara wako kufanya makubwa ambayo yatawafanya watu wengine waje kwako. Kwa zama tunazoendea sasa hutalipwa kwa sababu una kazi na hutapewa kazi kwa sababu ya cheti ulichonacho au koneksheni uliyonayo. Bali utalipwa kwa thamani unayozalisha, ambayo hakuna mwingine anayeweza kuzalisha kama wewe. Lazima ujitambue, ujue utofauti wako na uweze kuutumia kuyafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi.

Hatua ya pili ni kuhakikisha unakuwa na biashara. Kwa dunia inakoelekea, tunarudi kwenye zama za kabla ya mapinduzi ya viwanda, ambapo kila mtu alikuwa anafanya shughuli zake mwenyewe. Hakukuwa na ajira rasmi hivyo kila mtu alifanya shughuli zake na kutoa thamani kwa wengine. Sasa teknolojia zinapunguza nafasi za ajira zilizokuwepo, kila siku tunaona maroboti yakizidi kuchukua kazi za watu, hata kazi nyeti kama za tiba, kufundisha, udereva na nyingine, sasa kuna maroboti yanaelekezwa kwa urahisi na yanafanya. Njia pekee ya kukabiliana na hili ni kuhakikisha una kitu chako unachofanya, kinachoongeza thamani kwa wengine na wapo tayari kukulipa. Hapa namaanisha biashara, lakini siyo zile biashara za kuigana, bali biashara ya kipekee kwako, ambayo hakuna mwingine anayeweza kuifanya.

Zawadi mbili kwako.

Ili uweze kupiga hatua hizo mbili nilizokushirikisha hapo juu, nimekuandalia zawadi kubwa mbili ambazo zitakusaidia sana kufanya hayo mawili.

Zawadi ya kwanza ni kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA, kitabu hiki kinakupa nafasi ya kujitambua wewe mwenyewe, kujua nguvu kubwa iliyopo ndani yako, jinsi ya kuifikia na kuitumia kufanya makubwa kwenye maisha yako. Huwezi kushindana na maroboti kwa kuwa kawaida, bali utaweza kuyashinda kwa kuwa wewe, kwa kujitambua na kutumia nguvu kubwa iliyopo ndani yako ambayo hakuna roboti linaweza kuwa nayo. Kitabu hiki kinauzwa kwa tsh elfu 20, lakini leo nakupa zawadi ya kukipata kwa tsh elfu 15.

Zawadi ya pili ni kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA, kitabu hiki kinakupa nafasi ya kuweza kuanzisha na kukuza biashara ya kipekee kabisa kwako, biashara ambayo itatokana na kile kilicho ndani yako na siyo ya kuiga. Kitabu hicho kina mafunzo yote kuhusu biashara, kuanzia kupata wazo, kupata mtaji, kusajili biashara, kuikuza na kufikia mafanikio makubwa. Hiki ni kitabu kitakachokusaidia zama hizi ambazo ajira zinapungua, kinakupa mahali pa kusimama wewe kama wewe. Kitabu hiki pia kinauzwa kwa tsh elfu 20, lakini leo nakupa zawadi ya kukipata kwa tsh elfu 15.

Rafiki yangu mpendwa, nakupa zawadi hizi mbili ili uweze kujitambua na kuchukua hatua sahihi zitakazokuwezesha kukabiliana na mapinduzi makubwa yanayoendelea duniani kwa sasa.

Zawadi hii ni ya muda mfupi sana, hivyo nikusihi uchukue hatua sasa, ili usiikose zawadi hii na uweze kusimama imara kwenye zama hizi zisizokuwa na uhakika.

Changamkia sasa zawadi hizi nzuri za vitabu viwili nilivyokupa, kwani vitakusaidia sana kwenye maisha yako. Kimoja kinakufundisha jinsi ya kufanya makubwa kwa kuanzia hapo ulipo sasa na kingine kinakupa misingi ya kuanzisha na kukuza biashara. Wasiliana sasa na mtu wa mauzo kwa namba 0752 977 170 kupata zawadi hizo za vitabu.

Karibu upate na kusoma vitabu vizuri vya maendeleo binafsi na mafanikio kwa lugha ya Kiswahili. Pakua na weka app ya SOMA VITABU na upate maarifa sahihi. Kwa maelezo zaidi fungua; https://amkamtanzania.com/somavitabuapp

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania