Ni tarehe 31 mwezi Disemba, saa nne usiku, unaisubiri kwa hamu saa sita usiku ifike, uusherekee mwaka mpya.

Saa sita usiku inafika, siku na mwaka unabadilika, ni tarehe 01 Januari na una furaha kubwa ya kuuona mwaka mwingine, wengi hawajauona kama wewe.

Unapokea wimbo ambao kila mtu anauimba, ‘mwaka mpya mambo mapya’, kila mtu anakuuliza malengo yako mwaka huu ni yapi?

Kila anayekuzunguka anasema malengo yake, mwaka huu nataka nijenge, mwaka huu nataka kuanza biashara, mwaka huu naoa, nanunua gari na mengine mengi.

Akili yako inakuambia kama wengine wote wanaweka malengo ya mwaka mpya, na wewe pia unapaswa kuwa na malengo. Haraka haraka na wewe unakuna na malengo, mwaka huu nataka hiki au kile. Unakuwa ndiyo wimbo wa siku za mwanzo za mwezi Januari.

Mwezi Januari ni mwezi wa heka heka kweli, vitabu vingi vinanunuliwa, maeneo ya kufanyia mazoezi yanajaa, na vitu vingi huwa vinaanzishwa.

Lakini mpaka kufika mwezi Februari na Machi, heka heka hizo zinakuwa zimetulia kabisa, malengo na mipango ambayo watu walikuwa wamejiwekea wanakuwa wameachana nayo na kurudi kwenye mazoea.

Sasa rafiki nikuulize swali, ni mara ngapi umefanya hivyo kwenye maisha yako? Mara ngapi umeuanza mwaka mpya ukiwa na hamasa kubwa, ukijiwekea malengo makubwa na kusema HUU NI MWAKA WANGU, lakini mwezi mmoja baadaye umerudi kwenye mazoea?

Mwanafizikia Albert Einstein amewahi kunukuliwa akisema; ujinga ni kufanya jambo lile lile, kwa namna ile ile halafu kutegemea matokeo tofauti.

Hiki ndicho watu wamekuwa wanafanya kila mwaka mpya, wanajiambia ni mwaka wao wa kufanya makubwa, wanajiwekea malengo mbalimbali, lakini mwezi mmoja baadaye wameshasahau kabisa. Mwaka unaofuata wanarudia tena zoezi hilo.

HATUTAKI UJINGA.

Kwenye KISIMA CHA MAARIFA, tuliamua imetosha sasa, hatutaki tena kuwa wajinga, hatutaendelea kutegemea kufanya makubwa kwenye mwaka kwa kuimba yale yale mwanzo wa mwaka.

Hivyo tukaamua kuuanza mwaka wetu mapema, kwenye kipindi ambacho watu wengi wanaelekea kupumzika. Sisi tunauanza mwaka mapema na pale mwaka mpya unapofika na watu wanaweka mipango yao kwa hisia, sisi tunakuwa tumeshachanja mbuga na kufika mbali.

Hapa ndipo tulipoanzisha utaratibu wa kuuanza mwaka mpya wa mafanikio mwezi wa kumi na moja.

Kwa utaratibu huu, tayari tumeshauanza mwaka wetu mpya wa mafanikio 2020/2021, ambao umeanza mwezi Novemba 2020 na utamalizika mwezi Oktoba 2021.

Huwa tunaanza mwaka wa mafanikio kwa semina ya kukutana pamoja na katika kuuanza mwaka huu wa mafanikio 2020/2021 tutakuwa na SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020 itakayofanyika Jumapili ya tarehe 15/11/2020 jijini Dar es salaam.

Hivyo nakutumia ujumbe huu, kukukaribisha kwenye semina hii ya kipekee sana, ambayo inakwenda kukupa nguvu ya kufanya makubwa kwa miezi 12 ijayo. Utakwenda kuweka malengo halisi kwako na ambayo utayafanyia kazi.

Na tofauti na malengo unayojiwekeaga mwenyewe kila mwaka, ambayo unaweza kujidanganya, malengo utakayojiwekea kwenye KISIMA CHA MAARIFA utapata ufuatiliaji wa karibu kutoka kwa Kocha na hivyo hutaweza kujidanganya au kuishia njiani.

Kwa mwaka mzima, unapata usaidizi wa karibu kabisa kuhakikisha unayafikia malengo yako, na hili lina nguvu kubwa mno. Hutakuwa tena mjinga wa kufanya mambo yale yale na kutegemea matokeo tofauti. Utafanya mambo tofauti na kwa uhakika yatakuletea matokeo ya tofauti.

KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020.

Kama unataka kupiga hatua kubwa na za kweli kwenye maisha yako, basi kuna sehemu moja unapaswa kuwepo, kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA. Na kama unataka kufanya makubwa mwaka 2021, basi kuna kitu kimoja unapaswa kukifanya, kuhudhuria SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020.

Karibu sana kwenye semina hii ambapo utajifunza mambo mengi, utapata hamasa kutoka kwa wengine, utakuza mtandao wako na utajiwekea malengo na mipango ambayo utakwenda kuifanyia kazi mwaka mzima huku ukiwa karibu na Kocha.

Semina itafanyika jijini Dar es salaam, siku ya Jumapili ya tarehe 15/11/2020 kuanzia saa moja kamili asubuhi mpaka saa moja kamili usiku. Ni siku nzima ya kujifunza, kuhamasika na kuweka mikakati ya kupiga hatua kubwa.

Ada ya kushiriki semina hii ni tsh laki mbili (200,000/=).

Ili kupata nafasi ya kushiriki semina, tuma ada yako kwenda namba 0755 953 887 (majina Amani Makirita) kisha tuma ujumbe wenye majina yako kamili, namba ya simu na maelezo kwamba umelipia kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020.

Mwisho wa kufanya malipo ili kupata nafasi ya kushiriki semina ni kesho tarehe 10/11/2020 hivyo chukua hatua sasa unapopata ujumbe huu.

Nafasi za kushiriki kwenye semina hii ni chache, na muda umeshatuacha, hivyo kama unataka kufanya makubwa mwaka 2021, fursa ndiyo hii, ichangamkie sasa.

Nina shauku kubwa ya kufanya kazi na watu wachache kwa ukaribu ili waweze kupiga hatua kubwa kwenye maisha yao, naamini wewe ni mmoja wa hao wachache, hivyo hutaipoteza fursa hii.

Fanya malipo sasa ya tsh 200,000/= kwenda namba 0755 953 887 kisha tuma ujumbe wenye majina, namba ya simu na maelezo kwamba umelipia semina ili tarehe 15 tuwe pamoja na mwaka mzima 2020/2021 tuwe karibu tukifanya makubwa zaidi.

Wako rafiki kwenye safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani.