Rafiki yangu mpendwa,
Nichukue nafasi hii kukukumbusha kwamba leo ndiyo siku ya mwisho kabisa kwako kupata nafasi ya kufanya makubwa mwaka 2021.
Wote tunajua jinsi mwaka 2020 ulivyoenda, kama hukuwa na msingi mzuri unaouishi na usimamizi wa karibu basi ni kama umeupoteza mwaka huu 2020.
Sasa ipo nafasi ya kuuanza mwaka 2021 mapema kabisa na kuanza kufanya makubwa wakati wengine wanasubiri mwaka huo uanze.
Jumapili ya wiki hii, tarehe 15/11/2020 tutakuwa na SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA, hii ni semina ya kipekee kabisa kwako kujifunza na kuweka mikakati ya kuchukua hatua kubwa kwa mwaka mzima.

Kwenye semina hii ya mwaka 2020, tunakwenda kujifunza mambo mengi ya mafanikio pamoja na kupata shuhuda kutoka kwa wengine wanaopiga hatua ili kufanikiwa zaidi.
Pia kwa kushiriki semina, unapata nafasi ya kusimamiwa kwa karibu na kocha kwa kipindi cha mwaka mzima na hivyo hutakata tamaa na kurudi nyuma kama inavyotokea unapokuwa mwenyewe, kocha anakupa moyo na mwongozo wa hatua sahihi kwako kuchukua ili uweze kusonga mbele.
Unapokwenda kushiriki semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2020, unakwenda kuuanza mwaka 2021 mapema kabisa kabla haujafika, hivyo unapokuja kufika na wengine kuwa wanaweka malengo kwa hisia, wewe unakuwa umeshapiga hatua kubwa.
SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA ni sehemu ambayo wale wote wenye kiu ya mafanikio na waliojitoa kufanikiwa kweli wanapokutana. Usikose nafasi hii, kwa sababu ina manufaa makubwa kwako.
Leo tarehe 10/11/2020 ndiyo siku ya mwisho kufanya malipo ili uweze kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020, hivyo chukua hatua ili usikose semina hii.
Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) na unailipa kwa namba 0755 953 887 (majina Amani Makirita). Ukishatuma fedha tuma ujumbe wenye majina yako, namba ya simu na maelezo kwamba umelipia SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020.
Rafiki, tukio hili huwa linatokea mara moja tu kwa mwaka, usijipe sababu yoyote ya kulikosa kwani nguvu yake itakupa msukumo wa kufanya zaidi kwa mwaka mzima unaofuata.
Karibu sana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020, ambapo unakwenda kupata maarifa ya kipekee na hamasa kubwa ya kuchukua hatua ili ufanikiwe zaidi.
Fanya malipo yako sasa hivi kama bado hujakamilisha ili usiikose nafasi hii nzuri kwa ajili ya mafanikio yako. Tuma ada kwenda namba 0755 953 887.
Ninakusubiri kwa shauku kubwa kwenye semina, ili tuweze kushirikishana maarifa na mbinu sahihi za kwenda kuikabili dunia ambayo imebadilika mno ndani ya mwaka huu 2020. Bila ya mbinu za tofauti, mwaka 2021 utakuwa mgumu kwa wengi. Usikubali uwe mgumu kwako, njoo tuweke mikakati pamoja kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020.
Rafiki yako kwenye safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani.