“To do harm is to do yourself harm. To do an injustice is to do yourself an injustice — it degrades you.” — Marcus Aurelius
Unapowafanyia wengine ubaya, siyo wao pekee wanaoathirika, bali wewe mwenyewe unaathirika zaidi.
Huwezi kuwadanganya wengine kama hujajidanganya wewe mwenyewe.
Unapowaumiza wengine, ni kwa sababu ndani yako umeshajiumiza vya kutosha.
Na kama unawadhulumu wengine, ni kwa sababu umeshajidhulumu wewe mwenyewe vya kutosha.
Huwezi kutoa kitu ambacho hakipo ndani yako, hivyo kule unachofanya kwa wengine, ni ambacho umekuwa unajifanyia mwenyewe.
Chochote unachofanya kwa wengine, jua kitakuwa na madhara kwako pia, kwa sababu unakuwa kile unachofanya.
Tambua hakuna unayemuumiza zaidi yako wewe mwenyewe, hivyo kila wakati fanya kilicho sahihi na simama upande ulio bora.
Kabla hujafanys kitu kwa ajili ya wengine, jiulize kama wangefanya kwa ajili yako ungechukuliaje na jibu utakalopata jua ndiyo kitakachotokea ukishafanya kitu hicho kwa ajili ya wengine.
Maana chochote tunachofanya, kinarudi kwetu.
Asili huwa haikopeshi wala kuwa na upendeleo,
Inamlipa kila mtu sawasawa na anavyofanya.
Hivyo kuwa makini sana na unayofanya, maana yatarudi kwako mwenyewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kurudia rudis kufanya, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/10/2141
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.