“A man is well equipped for all the real necessities of life if he trusts his senses, and so cultivates them that they remain worthy of being trusted.” – Johann Wolfgang von Goethe
Miili yetu sisi binadamu huwa ina milango mingi ya fahamu.
Acha ile mitano ambayo kila mtu anaijua (macho, pua, masikio, ulimi na ngozi), kuna milango mingine mingi ya fahamu iliyosambaa kila sehemu ya mwili.
Kazi ya milango hiyo ni kukupa taarifa mbalimbali kuhusu hali ya mwili.
Mwili unapotaka maji unasikia kiu, ukitaka chakula unasikia njaa.
Mwili ukiwa kwenye joto dogo unasikia badiri, joto likiwa jingi unatokwa jasho.
Mwili ukiwa umechoka unauma na kusinzia.
Hizo na nyingine nyingi ni ishara ambazo mwili huwa unatupa, kutuonesha kuna mambo hayapo sawa.
Kama tukiusikiliza mwili na kuchukua hatua kwenye taarifa mbalimbali ambazo unatupa, tutakuwa na maisha bora na tulivu.
Tunakaribisha matatizo mengi kwenye maisha yetu pale tunapoupuuza mwili, unatuletea taarifa mbalimbali ila sisi tunaupuuza.
Mwili unakupa taarifa kwamba umechoka, lakini wewe unaendelea kuusukuma, kinachotokea ni unakulazimisha upumzike kwa kutengeneza ugonjwa wowote.
Jifunze kuusikiliza mwili wako, unajua mengi na ya muhimu kuhusu wewe na maisha yako, ambayo ukiyazingatia, utakuwa na maisha bora.
Kadiri unavyousikiliza mwili wako na kuuamini, ndivyo unavyozidi kukupa taarifa sahihi kupitia milango yako ya fahamu.
Hivyo hata unapojikuta njia panda na hujui nini ufanye, usikilize mwili wako, unajua kilicho sahihi kwako kufanya.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu jinsi ya kufanya kila kitu kama tahajudi, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/12/2143
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.
Asante sana kocha kwa kunijuza hili kuwa mwili wangu huwa unaniambia mambo mengi nitausikiliza
LikeLike
Vizuri James
LikeLike