Rafiki yangu mpendwa,

Bado tupo kwenye sababu 30 za kwa nini hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

Hili ni tukio la kipekee kabisa linalotokea mara moja tu kila mwaka na kuwaleta wale wote wenye kiu ya mafanikio kutoka maeneo mbalimbali.

Mwaka huu 2021, semina hii itafanyika jijini Dodoma kwa siku mbili, tarehe 16 na 17 ya mwezi oktoba 2021.

Hizo zinakwenda kuwa siku mbili zinazokwenda kuamua jinsi mwaka wako mmoja baadaye utakavyokwenda.

Kwani utajifunza mengi na kujiwekea mipango ambayo utaifanyia kazi kwa mwaka mzima.

Kuweka malengo makubwa siyo tatizo kwa walio wengi. Kila mtu anaweza kujiwekea malengo na mipango mikubwa sana.

Ni utekelezaji wa malengo na mipango hiyo, hasa baada ya kukutana na magumu ndiyo unaoleta tofauti kwa wanaofanikiwa na wanaoshindwa.

Wanaoshindwa huwa hawana namna ya kuwajibika kwenye malengo wanayojiwekea, hivyo mambo yanapokuwa magumu hawakomai na malengo yao, bali wanayakimbia na kwenda kufanya vitu vingine.

Wanaofanikiwa wanajijengea uwajibikaji kwenye malengo wanayojiwekea, hata mambo yawe magumu kiasi gani, hawayakimbii malengo yao, bali wanakomaa nayo mpaka kuyafikia.

Huhitaji kuelezwa sana nani kati ya hao wawili anapata mafanikio makubwa.

Karibu ushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ili ujijengee uwajibikaji wa kufanyia kazi malengo yako kwa mwaka mzima bila ya kuishia njiani.

Upate msukumo wa kuendelea kufanya hata pale unapokutana na magumu na changamoto mbalimbali.

Mafanikio siyo kutokukutana na magumu, bali kuweza kuyavuka magumu hayo na kufanya makubwa.

Na hilo ndiyo unakwenda kulipata kwa kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
Kama bado hujajiwekea nafasi kushiriki semina hii, wasiliana sasa na 0717 396 253.

Maelezo zaidi kuhusu semina yako hapo chini.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz