Rafiki yangu mpendwa,
Huwa nina utani ambao huwa natumia kwamba mafanikio ndiyo eneo pekee ambalo siri zake zipo bayana, lakini bado watu wanahangaika sana kuzitafuta.

Kwa zama tunazoishi sasa, ambazo ni zama za maarifa na taarifa, kila kitu kuhusu mafanikio kipo wazi kabisa.

Vitabu vingi mno vimeandikwa kuhusu mafanikio.
Kama unajiambia wewe hupendi kusoma, kuna audio ba video nyingi mtandaoni kuhusu mafanikio.
Na hata kama unajiambia huna muda wa kupitia mengi, kuna jumbe fupi fupi nyingi mno mitandaoni.

Kwa mfano anzia tu kwenye ‘status’ za mtandao wa wasap. Utakutana na nukuu na mafunzo mengi ambayo watu wanashirikishana.
Yaani chini ya dakika 1 tu unaweza kujifunza mengi kuhusu mafanikio kuliko waliyoweza kujifunza watu kwa mwaka mzima kwenye karne ya 15.

Swali ni, kwa wingi huo wa maarifa na urahisi wake wa kupatikana, je watu wengi wamefanikiwa zaidi sasa kuliko zamani?

Na jibu lipo wazi, ni hapana. Bado wanaofanikiwa sana ni wachache kati ya wengi wanaotaka mafanikio makubwa.

Katika 100 wanaotaka kufanikiwa sana, ni mmoja pekee anayeyapata mafanikio makubwa kabisa.

Hilo linaonyesha wazi kwamba kikwazo cha wengi kufanikiwa siyo kukosa maarifa.
Maana hayo hamejaa tele katika zama hizi, yaani tunazama kabisa kwenye maarifa.

Swali muhimu ni nini kinachokosekana kwa watu mpaka wanashindwa kufanikiwa?

Jibu ni kujitoa hasa (DEDICATION) na kuweka nia (COMMITMENT) kwamba lazima utayapata mafanikio unayoyataka bila ya kujali unakutana na nini.

Lazima uamue unayataka mafanikio na lazima uazimie kuyapambania mpaka kuyapata.
Kauli mbiu yako lazima iwe nitapata ninachotaka au nitakufa nikiwa napambana, kamwe sitoishia njiani, hata mambo yawe magumu kiasi gani.

Kusoma na hata kusema hayo ni rahisi, na wengi tayari wameshafanya hivyo, na bado hawafanikiwi.

Hapo ndipo kinahitajika kitu kimoja muhimu mno ili uweze kufanikiwa, kitu ambacho hakitakupa nafasi ya kurudi nyuma hata kama umejishawishi kiasi gani kwamba huwezi kuendelea tena.

Kitu hicho ni uwajibikaji (ACCOUNTABILITY).
Hiki ndiyo kinachokosekana kwa wengi na kukosekana kwake kumekuwa kaburi la mafanikio ya wengi.

Rafiki, tuwe tu wakweli na tusitake tu kufurahishana, kama huna namna ya kuwajibika kwenye malengo na mipango yako, hakuna namna unaweza kufikia.
Haipo kabisa. Mwisho wa hadithi.

Unaweza kujaribu mengi, lakini mwisho wa siku utarudi pale pale ulipoanzia.

Kama unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa uwajibikaji, mfumo utakaokusukuma mpaka ufike kule unakotaka. Mfumo wa muda mrefu na siyo tu wa hamasa za muda mrefu.
Basi hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

Hii ni semina ya kipekee kabisa ambapo siyo tu unakwenda kupata maarifa na hamasa, bali pia unaenda kupata mfumo wa kukuwajibisha ili utekeleze kweli yale unayopanga.

Mfumo huo hautakuwa na huruma kwako, utakachotaka ni mchakato na matokeo, mengine yote ni hadithi zisizokuwa na maana.

Je umedhamiria kweli kufanikiwa na siyo tu kutamani mafanikio?
Je upo tayari kufanya kila kinachopaswa kufanyika ili uweze kupata mafanikio unayotaka?
Kama majibu ni ndiyo, hakikisha hukosi kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 maana ndipo penye mwarobaini wa mafanikio yako.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz