Ni mahusiano.

Bila kuficha fedha ni tatizo katika mahusiano mengi lakini nimegundua mahusiano ndiyo shida zaidi. Mtu anaweza kuwa na fedha lakini mahusiano yake yanapokuwa ya hovyo anapoteza kabisa ramani ya maisha.

Watu huwa wanaweka kazi kwenye eneo la kutafuta fedha lakini wanasahau kuweka kazi katika eneo la mahusiano. Kama nyumbani hapako vizuri hata utulivu wa akili wa kufanya kazi unakosa ndiyo maana huwa napenda kuona mahusiano mazuri yakiwepo basi mafanikio yatakuja yenyewe.

Mahusiano yanawachosha watu bila hata kufanya kazi. Na cha ajabu ni kwamba watu wengi hawana muda wa kujifunza zaidi elimu ya msingi ya mahusiano ndiyo maana kila siku mahusiano yanakuwa yanawaliza.

Wako watu ambao wangekuwa mbali sana ila kwa sababu mahusiano yaliingilia kati na kuvuruga mahusiano yao. Wako ambao wamefika hapo walipo kwa sababu ya kuwa na mahusiano mazuri na familia yake au wale anaohusiana nao kikazi au kibiashara.

Mahusiano mazuri ni sababu chanya ya mafanikio kwa kila mtu ambaye anapenda mafanikio. Lakini, mahusiano yako yakiwa hasi, huwezi kuona hata maana ya mafanikio yenyewe.

Iko njaa kubwa kwenye mahusiano yetu ambayo yametuzunguka. Kila binadamu ni kiumbe wa mahusiano kadiri ya vinasaba. Huwezi kukosa mahusiano kama wewe ni binadamu, kwani umezaliwa katika familia na una ndugu nk.

Ni mpango wa Mungu wa kila mmoja wetu kuzaliwa katika mahusiano ya kifamilia.

Ndoa siyo mpango wa mwanadamu, ni mpango wa Mungu hivyo ukiwa na ndoa nzuri hata mambo yako mengine yataenda vizuri sana.

Maisha yako ya kindoa yakiyumba, hata sehemu nyingine pia zinayumba.

Shabaha yangu kubwa ni kukutaka wewe rafiki yangu ujifunze zaidi eneo la mahusiano na kulifanyia kazi. Mahusiano ni kazi kama zilivyo kazi nyingine.

Hatua ya kuchukua leo;
Usikubali kupoteza siku yako bila kuimarisha eneo la mahusiano yako. Weka kazi kutafuta fedha lakini usisahau kutunza na kulinda familia na mahusiano yako kiujumla.

Nunua vitabu vya mahusiano na jifunze. Mara kwa mara ongeza maarifa na jua saikolojia ya watu ili uweze kujenga ushawishi na kuimarisha mahusiano yako na wengine.

Ukiwa na mahusiano mazuri yatakupa nguvu ya ushawishi ya kupambana kuhakikisha unapata kile unachotaka. Mahusiano yetu yakiwa mabovu yanakuwa yanamaliza nguvu zetu na muda.

Yaani watu wengi wanatembea lakini wana maumivu ya mahusiano ndani yao. Ninakusihi sana uanze kusoma kitabu chako cha Ijue Njaa Ya Wanandoa ili uweze kupata maarifa sahihi ya kunogesha mahusiano yako.

Makala hii imeandikwa na
Deogratius Kessy, ambaye ni mwandishi, mwalimu na mjasiriamali.

Unaweza pia kujifunza mengi kutoka kwake kupitia mafundisho anayoendelea kuyatoa kupitia mtandao wake wa
http://kessydeo.home.blog vitabu na kwenye klabu yake ya MIMI NI MSHINDI. Karibu sana.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,
Mwl, Deogratius kessy
0717101505//0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante sana