Rafiki yangu mpendwa,
Nimekuwa nakupa taarifa kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 kwa muda sasa.
Nimekupa kila sababu kwa nini hii siyo semina ya wewe kukosa, maana itakwenda kuwa chachu ya mabadiliko makubwa kwako.

Pamoja na maelezo mengi ambayo nimeyatoa, bado kumekuwa na maswali ambayo watu wamekuwa nayo kuhusu semina hii.

Hapo chini ni maswali yaliyoulizwa na wengi na majibu yake. Karibu upate ufafanuzi wa haya muhimu na uchukue hatua sasa ili usikose semina hii.

Swali; kwa nini ada ya kushiriki ni kubwa sana?

Jibu; ni kweli ada ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni kubwa na ambayo wengi hawajazoea. Tsh laki 2 siyo kiasi kidogo, ukiweka na gharama za usafiri na malazi, itakugharimu kushiriki semina hii.
Kuna kanuni moja ya asili ambayo huwa inafanya kazi kwenye mambo yote bila kushindwa, unapata kile unacholipia.
Kadiri unavyolipa gharama kubwa, ndivyo unavyopata thamani kubwa zaidi.

Kwa kulipa gharama kubwa ya kushiriki semina, unapata faida hizi;
1. Unakutana na watu ambao ni makini na watakaokuwa na mchango mkubwa kwenye mafanikio yako. Maana anayelipa gharama hiyo lazima awe makini.
2. Unapata mafunzo ya kipekee ambayo huwezi kuyapata mahali pengine popote.
3. Unapata usimamizi wa karibu wa Kocha kwa kipindi cha mwaka mzima.

Hivyo kuwa tayari kulipa gharama kubwa ili uweze kupata thamani kubwa.

Swali; je naweza kuja na mtu mwingine?

Jibu; ndiyo unaweza kuja na mtu mwingine, iwe ni mwenza wako, ndugu, rafiki au mfanyakazi wako.
Itapendeza sana na itakufaa kama utaweza kuja na mwenza wako (mke/mum), kwa sababu mtajifunza kwa pamoja na kuweza kuwa kwenye njia moja ya mafanikio.
Kama unataka kuja na mtu, naye pia utamlipia gharama za kushiriki semina ili aweze kupata nafasi.
Kama kuna mtu yeyote kwenye maisha yako unayemjali sana, mpe zawadi hii ya kuja naye kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

Swali; utaweza kweli kumfuatilia kila mtu?

Moja ya ahadi ninazokupa kwenye kushiriki semina hii ni kukufuatilia kwa karibu kwa mwaka mzima.
Wapo ambao wana wasiwasi kama hilo kweli linawezekana.
Ndiyo ni zoezi gumu kufuatilia watu wengi, lakini linawezekana kabisa.
Nimeweka kipaumbele kikubwa zaidi kwenye KISIMA CHA MAARIFA ili kiwe na matokeo makubwa kwa wote waliopo.
Hivyo kinachohitajika ni utayari wako wa kujisukuma zaidi, mengine niachie mimi.

Swali; bado sijawa na biashara na sijajua biashara gani nianze.

Utanufaika zaidi na SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 kama tayari utakuwa na biashara au unapanga kwenda kuanza biashara.
Hata kama hujawa na biashara bado utanufaika na moja ya manufaa makubwa ni hamasa itakayokubadili mno pale unaposikia kutoka kwa wengine.
Huwezi kushiriki semina hii halafu ukabaki ulivyo, utatoka ukiwa na msukumo mkubwa wa kwenda kufanya kitu cha tofauti kwenye maisha yako.

Karibu sana ushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, hata kama unajiona hujawa tayari, semina hii itakuonyesha uko tayari kupitiliza, unachohitaji ni kuanza kuchukua hatua.

Swali; kama nisiposhiriki naweza kupata ufuatiliaji wa karibu kama wengine?

Wenye uhitaji wa kufuatiliwa kwa karibu ni wengi.
Na zoezi la kuwafuatilia watu kwa karibu linahitaji kujitoa kweli, linanilazimu kuachana na vitu vingi ambavyo tayari nilikuwa ninafanya.
Hivyo nahitaji kuwa na mchujo sahihi wa kujua nani kweli anastahili ufuatiliaji huo.
Ushiriki wa semina ni moja ya vigezo vya mchujo.
Kama mtu ameshiriki semina, maana yake amejitoa kweli kupiga hatua na hayupo tayari kuzuiwa na chochote.
Huyo naweza kuweka juhudi zangu kumfuatilia kwa karibu maana juhudi hizo zina nafasi kubwa ya kuzaa matunda.

Hivyo kupata usimamizi wa karibu kabisa kutoka kwa Kocha, hakikisha unashiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

Swali; niko mbali sana, je naweza kushiriki kwa njia ya mtandao?

Jibu; nimekuwa natoa mafunzo kwa njia ya mtandao kila siku kwa zaidi ya miaka 8 sasa.
Semina ya kukutana ana kwa ana ndiyo njia pekee ya kujifunza ana kwa ana inayopatikana mara moja tu kwa mwaka.
Hivyo thamani kubwa ya semina ipo kwenye kukutana ana kwa ana.
Kuondokana na usumbufu mwingine wote na kuwa sehemu moja, kujifunza na kuzungukwa na wengine wenye mtazamo kama wako.

Hivyo njia pekee ya kushiriki semina hii ni kuwepo moja kwa moja. Hakutakuwa na nafasi ya kushiriki kwa njia ya mtandao.

Swali; je semina hiyo itarekodiwa ili niweze kujifunza hata kama sijashiriki?

Kama kwenye jibu la swali lililopita, hakutakuwa na rekodi ya mafunzo ya semina hiyo, zaidi ya yale unayoondoka nayo kwa kushiriki moja kwa moja.
Hivyo karibu sana ushiriki ili uweze kufaidi haya mazuri.

Swali; siwezi kumudu gharama za semina, je nawezaje kusaidiwa maana nahitaji sana haya mafunzo?

Kama huwezi kumudu gharama za kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, hiyo inapaswa kuwa sababu muhimu kwako kuhakikisha unashiriki.
Kwa sababu kuna kikwazo kipo kwenye maisha yako ambacho kinakuzuia usiweze kumudu vitu muhimu kwako.
Kwenye semina tutakwenda kuvunja kikwazo hicho ili wakati mwingine kisipate nafasi ya kukuzuia kupata yale yenye manufaa kwako.

Kama huwezi kumudu gharama za kushiriki semina, tumia hiyo kama sababu na fanya kila linalowezekana kuhakikisha umeshiriki semina hii ili hiyo isije kujirudia tena kama sababu kwako.

Rafiki, naamini maswali hayo na majibu yake yamekupa mwanga mkubwa kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA, acha kuendelea kusubiri na chukua hatua sasa.
Nafasi zilizobaki ni chache na muda wa kuzipata nao unakaribia kuisha.

Chukua hatua sasa ili maisha yako yaende kunufaika kwa kiasi kikubwa.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz