Rafiki yangu mpendwa,
Mazingira yanayokuzunguka yanaathiri sana mafanikio yako.
Unaweza kuwa unayataka kweli mafanikio, unaweza kuwa na maarifa ya kutosha kuhusu mafanikio, lakini bado ikawa vigumu kwako kufanikiwa.

Kama mazingira yako hayakuungi mkono na kukuchochea wewe kufanikiwa, hutaweza kufanikiwa, hata kama unakazana kiasi gani.

Mazingira yana vitu vingi, watu, eneo, vyakula, habari na kadhalika.
Lakini katika vitu hivyo, watu ndiyo wenye nguvu kubwa zaidi, hasa wale watu wa karibu.

Moja ya kanuni muhimu za mafanikio ni ile inayosema mafanikio yako ni wastani wa mafanikio ya watu watano wa karibu kwako.
Yaani huwezi kufanikiwa kuwazidi watu watano wa karibu sana kwako, wale unaotumia nao muda wako mwingi.

Hivyo imekuwa inashauriwa mtu uchague kwa usahihi watu wako wa karibu, wale utakaowapa muda wako mwingi na watakaojua mambo yako mengi.

Kwa bahati nzuri kabisa ni kwamba katika watu wako wa tano wa karibu, mmoja tayari yupo na huwezi kumwondoa ili kuleta mwingine. Hivyo nafasi za kuchagua zimebaki nne.

Ila hiyo moja ambayo tayari imeshachukuliwa, ina nguvu kubwa sana ya kuamua mafanikio yako.

Aliyechukua nafasi hiyo ni mwenza wako, yaani mke, mume au mchumba wako ambaye mmeshaafikia kwamba mtakuwa pamoja kwa maisha yenu yote.

Kwa kuwa nafasi hii tayari imeshajazwa na kwa kuwa ina athari kubwa kwenye mafanikio yako, unapaswa kuhakikisha mwenza wako anakuwa mchango kwa mafanikio yako.

Ipo kauli ya kivita inayosema kama haupo upande wetu basi wewe ni adui yetu. Na kwa kuwa mafanikio yanafanana sana na vita, kama mtu hayupo upande wako, basi huyo ni kikwazo kwa mafanikio yako.

Mwenza wako anapaswa kuwa upande wako wa mafanikio. Anapaswa kuwa mtu wa kwanza kukuamini na kukupa moyo kwenye ndoto kubwa ulizonazo.
Anapaswa kuwa mtu wa kukuwajibisha ili utimize yale uliyopanga.

Lakini peke yake hawezi yote hayo, anahitaji naye kupata maarifa sahihi ya mafanikio ili aweze kuwa mshirika wako mzuri na mpambane kwa pamoja kufanikiwa.

Ni kwa sababu hiyo nimechagua kutoa zawadi ya mtu kuja na mwenza wake kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
Kwa kuwa mwenza wako ni sehemu muhimu ya mafanikio yako, natoa zawadi kwa yeyote atakayekuja na mwenza wake kwenye semina.

Itumie nafasi hii kujenga timu yako ya mafanikio ambayo haiwezi kuangushwa na chochote.
Njoo na mwenza wako kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ili aelewe ndoto kubwa unazofanyia kazi na nafasi yake katika kuzikamilisha ndoto zako.

Kupata zawadi hiyo ya kuja na mwenza wako kwenye semina, tuwasiliane kwa namba 0717 396 253.  Fanya hivyo leo hii ili tuweze kutunza nafasi kwa ajili ya mwenza wako.

Usikubali kupoteza fursa hii ya kipekee sana kwako, safari iliyo mbele yako ni kubwa, unahitaji kutumia kila rasilimali iliyo mbele yako, na mojawapo ni mwenza wako.
Njoo na mwenza wako kwenye semina ili ajue namna bora ya kukuunga mkono katika kuyapambania mafanikio makubwa.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz