Rafiki yangu mpendwa,
Unayataka mafanikio makubwa ndiyo maana unasoma hapa. Hongera sana kwa hilo.

Lakini kuna habari ambazo siyo nzuri sana kwenye hiyo safari uliyochagua. Takwimu za mafanikio zinatisha na kusikitisha.
Wanaoyataka mafanikio ni wengi, lakini wanaoyapata mafanikio hayo ni wachache mno.

Ni asilimia 1 tu ya watu kwenye eneo lolote lile wanakuwa wamefikia mafanikio makubwa. Huku asilimia nyingine 9 ya watu wakiwa na mafanikio ya wastani.
Kinachoumiza ni hiki, asilimia 90 ya watu kwenye eneo lolote lile hawapati mafanikio.

Siyo kwamba watu hao hawayataki mafanikio, wanayataka mno.
Siyo kwamba watu hao ni wazembe, wanajituma sana.
Lakini kwa namna fulani ambayo wengi hawaielewi, wachache ndiyo wanaofanikiwa huku wengi wakibaki bila mafanikio.

Kwa miaka mingi tafiti zimekuwa zinafanywa kuhusu kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa.
Kila ambacho watu walikuwa wanadhani ni sababu imegundulika siyo.

Watu walidhani elimu ni sababu, lakini siyo. Kuna watu wenye elimu kubwa waliofanikia na ambao hawajafanikiwa. Na kuna watu wenye elimu ndogo waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa.

Wakadhani labda ni mazingira na eneo ambalo mtu yupo, nayo ikawa siyo kweli. Kwenye kila eneo, kuna watu wamefanikiwa sana na kuna ambao hawajafanikiwa. Yaani utakuta watu wanakaa eneo moja, wanafanya kazi au biashara ya aina moja, ila mmoja amefanikiwa na mwingine hajafanikiwa.

Pia watu walidhani ni kurithi, lakini hilo pia siyo kweli. Kuna watu wanarithi mali nyingi na kupoteza zote na kuna watu wanaanzia sifuri kabisa ila wanafanikiwa sana.

Kukosekana kwa majibu ya wazi ya kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa kumefanya watu watengeneze sababu zao wenyewe.
Kwa kuwa binadamu hatupendi kukosa sababu au maelezo ya watu, pale mtu anapokuwa amepata mafanikio makubwa na hatuwezi kuelezea ameyapataje, basi tunajipa jibu.
Tunasema huyo ni FREEMASON, au ana majini, mshirikina na kauli nyingine za aina hiyo.
Kwa kuwa hatujui nini kinawatofautisha watu hao, tunaamini kutakuwa na nguvu fulani za kishirikina ambazo ndiyo zinawatofautisha.

Lakini hilo nalo siyo kweli, ni sababu tu ya kujiridhisha, ambayo inawaacha wengi wakiwa hawajafanikiwa na wachache sana kupata mafanikio makubwa.

Kwa utafiti mkubwa ambao nimeufanya kwenye eneo la mafanikio, nimegundua kuna kitu kimoja ambacho kinawatofautisha wale wanaofanikiwa sana na ambao hawafanikiwi.
Kitu hicho kipo kwa kila aliyefanikiwa na kinakosekana kwa wote ambao hawajafanikiwa.
Tatizo la kitu hicho ni kiko wazi kabisa, lakini wengi hawakioni wala hawakielewi.
Hata wale wanaofanikiwa sana, hawajijui kama wana kitu hicho. Na ndiyo maana hata wanapoitwa freemason au wana majini, wanakosa cha kujitetea kwa sababu hata wao wenyewe hawaelewi kwa nini mafanikio makubwa sana yanakuja kwao.

Kitu hicho kimoja ambacho kinawatofautisha wanaofanikiwa sana na wanaoshindwa nimekipa jina la UBATIZO WA MAFANIKIO.
Hii ni dhana ambayo imekuwa haifundishwi kwenye maarifa mengi ya mafanikio, kwa sababu siyo rahisi kueleweka na wala haiwafurahishi watu.

Kwenye mafunzo mengi ya mafanikio, watu wanapenda kusikia vitu vizuri na vya kuhamasisha. Lakini kwenye uhalisia wa mafanikio mambo ni tofauti kabisa. Hakuna aliyefanikia kwa kufanya vitu rahisi na kwa namna anavyojisikia yeye.

Ubatizo wa mafanikio ni dhana iliyobeba ugumu hasa wa mafanikio ni kiasi ambacho mtu anapaswa kujitoa ili kuyapata mafanikio makubwa.

Umewahi kusikia ubatizo kwenye dini mbalimbali, kwa sehemu kubwa ubatizo huo ukiwa wa maji.
Sasa ubatizo wa mafanikio ni tofauti kidogo, siyo ubatizo wa maji, bali ubatizo wa moto.
Ni ubatizo unaokuacha ukiwa imara na kuweza kupambana na chochote kinachokuja mbele yako, bila kukata tamaa wala kurudi nyuma.

Ukishapata ubatizo huo wa mafanikio kuna vitu viwili tu mbele yako, kupata unachotaka au kufa ukiwa unakipambania. Hakuna chaguo jingine.

Ubatizo wa mafanikio una vitu viwili vikubwa; KAFARA NA MASHARTI.
Huwezi kupata mafanikio makubwa kama hujatoa kafara.
Na hapa kafara haimaanishi kuua watu, bali kuondokana na baadhi ya vikwazo vinavyokuzunguka sasa.
Pia huwezi kufanikiwa kama hujajiwekea masharti makali kwenye maisha yako.

Je upo tayari kupata ubatizo wa mafanikio ili ujihakikishie kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako?
Kama jibu ni ndiyo basi jipatie leo nakala yako ya kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO.
Ndani ya kitabu hicho kipya utajifunza kwa kina kuhusu dhana hii ya ubatizo wa mafanikio na jinsi unavyoweza kujibatiza wewe mwenyewe ili ufanikiwe.

Kwa kusoma kitabu hiki na kuchukua hatua, mafanikio kwako litakuwa swala la muda tu, hutakuwa na wasiwasi wowote kwamba huwezi kufanikiwa.

Jipatie leo nakala ya kitabu kipya cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO ujue kafara unazopaswa kutoa na masharti unayopaswa kujiwekea ili upate mafanikio makubwa.
Kupata kitabu wasiliana na 0752 977 170 na utaletewa au kutumiwa kitabu popote ulipo.

Usikubali kubaki kwenye giza unapokuja kwenye swala la mafanikio.
Usikubali kuwa sehemu ya asilimia 90 ya watu ambao wanahangaika sana ila hawafanikiwi.
Jua kuhusu ubatizo wa mafanikio na ujibatize wewe mwenyewe ili uwe na uhakika wa mafanikio.
Chukua hatua sasa ya kupata kitabu ili ujipe uhakika wa kufanikiwa.

Rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.