Rafiki yangu mpendwa,
Kwa muda sasa nimekuwa nakueleza kuhusu KISIMA CHA MAARIFA ambacho ni jamii ya kipekee kabisa katika kuyaendea mafanikio makubwa kwenye maisha.

Tunakwenda kuuanza mwaka wetu wa mafanikio 2021/2022 na katika huo mwaka nakwenda kufanya kazi na mtu mmoja mmoja kwa karibu kabisa ili aweze kupata matokeo ya tofauti.

Ndiyo maana nakusihi sana uchukue hatua leo ya kujiunga, kwani baada ya leo hutaipata tena nafasi hii mpaka mwaka ujao kwenye kipindi kama hiki.
Hakutakuwa na nafasi ya kujiunga na KISIMA mwaka wa mafanikio ukiwa umeshaanza.

Hivyo kama kwenye mipango yako umekuwa unajiambia siku moja utakuja kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, wakati sahihi ndiyo sasa, usiendelee kusubiri tena.
Baada ya siku ya leo kumalizika, hutaipata tena nafasi hii nzuri na ya kipekee sana kwako.
Hivyo chukua hatua sahihi kwako sasa hivi, wasiliana na namba 0717 396 253 sasa ili uweze kupata nafasi hii.

Usijali kwamba haupo tayari au huwezi kumudu, kama kweli unataka kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA na kama kweli umejitoa ili kufanikiwa, tuwasiliane sasa upate nafasi hii.
Unachohitaji ni kuwa na ndoto kubwa na kuwa na utayari wa kuzipigania kwa kila namna ili kuzifikia.
Mengine niachie mimi, najua jinsi ya kukusaidia vyema kwenye hilo.

Sehemu ya jamii ya KISIMA CHA MAARIFA, watu waliojitoa kweli ili kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao.

Rafiki nisikucheleweshe kuchukua hatua sasa, maana mengi nimeshakuambia. Mafanikio yako yapo kwenye maamuzi utakayofanya sasa, iwapo utajiunga na KISIMA CHA MAARIFA na uweze kufanikiwa au hutajiunga na uendelee kubaki pale ulipo sasa.
Hakuna mwingine mwenye uwezo wa kufanya maamuzi hayo isipokuwa wewe mwenyewe.

Kwa kumalizia tu nikukumbushe mambo 10 ambayo utakuwa umechagua kuyakosa kama hutajiunga na KISIMA CHA MAARIFA leo.

1. Utakuwa umechagua kukosa kuwa sehemu ya jamii bora na ya kipekee katika kufanikiwa, watu chanya na wanaojituma ili kufanikiwa zaidi.

2. Utakuwa umekosa nafasi ya kujenga nidhamu muhimu kwa mafanikio yako.

3. Utashindwa kujenga uadilifu wa hali ya juu unaolinda mafanikio yako.

4. Utakosa msukumo wa kujituma zaidi kwenye kile unachofanya, ambacho kinahitajika sana kwenye mafanikio.

5. Utashindwa kujenga mtaji muhimu wa afya ambao ni muhimu kwa mafanikio. Afya inayohusisha mwili, akilo, roho na hisia.

6. Utashindwa kujenga utajiri mkubwa ambao unakupa uhuru kamili. Maana bila ya uhuru wa kifedha hakuna uhuru wa kimaisha.

7. Utakosa hekima muhimu unayohitaji kujijengea ili kufanya maamuzi bora na yenye tija.

8. Utashindwa kujenga urafiki na rafiki wa kweli kwenye maisha yako ambaye ni kazi.

9. Utakosa upendo ambao ndiyo imani kuu kwenye mafanikio, kujipenda mwenyewe, kuwapenda wengine na kupenda kile unachofanya.

10. Utashindwa kutumia nguvu ya huduma kuleta mapinduzi kwenye maisha yako na ya wengine. Kwa kuyafanya maisha yako kuwa huduma, unaleta matokeo makubwa.

Rafiki, najua wewe ni mtu makini na haupo tayari kukosa haya muhimu mno kwa mafanikio yako.
Hivyo basi, tuma ujumbe wako sasa hivi kwenda namba 0717 396 253 ili uipate nafasi hii.
Karibu sana.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.