#SheriaYaLeo (11/366); Nini Kinakupa Shauku Zaidi?

Kila mmoja wetu kuna kitu ambacho akikifanya anajisikia vizuri zaidi na kupata msukumo wa kuendelea kukifanya kwa muda mrefu bila kuchoka.

Katika kufanya kitu hicho, mtu unakuwa na nguvu kubwa na ubunifu ambao wengine wanaushangaa.
Wakati kwa wengine kufanya kitu hicho ni kazi ngumu, kwako inaonekana kama mchezo tu.
Wakati wengine inabidi walazimishwe kufanya, wewe unafanya bila hata ya kulazimishwa.

Jua ni kitu gani kwako kina sifa hiyo, kitu ambacho kina msukumo mkubwa ndani yako kukifanya na kifanye kwa ubora zaidi.
Hapo ndipo wito na wajibu wako mkubwa kwenye maisha ulipo.

Usijiambie hujajua wito na wajibu wako, angalia vile vinavyokupa shauku kubwa kufanya na uvifanye vizuri.

Sheria ya leo; Fanya kitu ambacho kinakupa shauku kubwa na kukufanya ujisikie vizuri zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma