Rafiki yangu mpendwa,

Napenda kuchukua nafasi hii kukutakia heri ya sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya 2021.

Huu ni wakati mzuri wa kuwa pamoja na watu wetu wa karibu ili kuimarisha mahusiano yetu.

Lakini pia ni wakati mzuri zaidi wa kutafakari safari yetu ya maisha, kwa kule tulipotoka, tulipo sasa na tunapokwenda.

Kuna vishawishi mbalimbali kwenye hii misimu ya sikukuu vya kutumia fedha vibaya na hata kufanya mambo yanayoweza kuathiri afya yako kama kutumia vilevi kupitiliza.

Nikusihi rafiki yangu uendelee kusimamia nidhamu ya hali ya juu katika msimu huu wa sikukuu, ukijikumbusha kwamba kuna maisha baada ya sikukuu.

Katika kusherekea sikukuu hizi, rafiki yako nimekuandalia zawadi kabambe kwako.
Ni zawadi itakayokuwezesha kuuanza mwaka 2022 kitofauti kabisa na kwenda kufanya makubwa zaidi.

Zawadi hiyo kupata kitabu kimoja cha bure kwa kila vitabu vitatu utakavyonunua siku ya leo.

Vitabu hivyo ni kama ifuatavyo;

1. ELIMU YA MSINGI YA FEDHA (BASIC FINANCIAL EDUCATION); Maarifa Sahihi Ya Kifedha Yatakayokufikisha Kwenye Utajiri Na Uhuru Wa Kifedha. – Tsh 20,000/=

2. BIASHARA NDANI YA AJIRA; Mwongozo Wa Kuanzisha Na Kukuza Biashara Yako Ukiwa Kwenye Ajira (Toleo la Pili). – Tsh 20,000/=

3. ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA; Jinsi Ya Kuanza Na Kukuza Biashara Yenye Mafanikio Makubwa. – Tsh 20,000/=

4. UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA; Tambua Uwezo Mkubwa Wa Akili Na Mwili Wako Na Jinsi Ya Kuutumia Kutenda Miujiza. – Tsh 20,000/=

5. EPUKA UTUMWA KIDIJITALI; Jinsi teknolojia mpya zinavyokufanya mtumwa na njia za kuondoka kwenye utumwa huo. – Tsh 20,000/=

6. MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO; Kanuni za kuyaishi maisha ya mafanikio makubwa kwako. – Tsh 20,000/=

Kupata vitabu hivi, wasiliana na kitengo cha mauzo kwa namba 0752 977 170 na utapewa maelekezo ya kuvipata kwa popote ulipo.

Hivi ni vitabu muhimu sana kwako kuuanza mwaka 2022 kwa kishindi kikubwa.
Usikubali kukosa zawadi hii nzuri kwa siku ya leo.

Na kama tayari umshapata vitabu hivi, basi tumia fursa hii kuvitoa kama zawadi kwa wengine.
Wachague watu wako wa karibu ambao unaona wanaweza kunufaika na vitabu hivi, kisha pata zawadi hii na uwapatie kama zawadi.

Wasiliana sasa na 0752 977 170 kujipatia zawadi yako siku ya leo na usherekee sikukuu hizi ukiwa na msingi imara wa mafanikio.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Muuza Matumaini, Kocha Dr Makirita Amani.