#SheriaYaLeo (62/366); Ingia Ndani.

Safari ya ubobezi inaweza kuelezewa kwa namna moja, kuzidi kuzama ndani kwenye kile unachotaka kubobea.

Wakati unapoianza safari hii unakuwa unakiona kitu kwa nje na mambo mengi huyaelewi.

Lakini kadiri unavyojifunza na kufanya, unazidi kuzama ndani zaidi.
Unapata uelewa wa kina kuhusu kitu hicho na kuweza kukifanya kwa viwango vya juu zaidi.

Watu walio nje wanaweza kushangaa umewezaje kufanya ulichofanya, lakini kwa ndani wewe unajua ni muda na juhudi ulizoweka katika kubobea kitu hicho ndiyo zimekuwezesha kufikia ngazi hiyo.

Zidi kuzama ndani kadiri unavyokwenda, hiyo ndiyo njia ya kufika na kudumu kwenye ubobezi wa hali ya juu.

Sheria ya leo; Kama utaweka juhudi kubwa, utazidi kuingia ndani kwenye kina cha maarifa na ujuzi. Hiyo ndiyo njia ya kufika na kudumu kwenye ubobezi kwa kukielewa kitu kwa undani zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu