Rafiki Yangu,

Amini Wewe ni Mshindi, na Ushindi Upo Ndani Yako…

Nakumbuka kama jana tu, Jumatano saa 4 na nusu asubuhi nikiwa ofisini maeneo ya Tabata Dar es salaam nilipokea simu kutoka kwa Godfrey ambaye ni client wetu wa KISIMA CHA MAARIFA na Chaneli ya SOMA VITABU TANZANIA.

Godfrey kwa sasa ni MENEJA katika kampuni ya WAMICCO.LTD.

Awali ya yote nilimkaribisha kwa bashasha kweli kweli…

Godfrey mara zote ni mchangamfu na msema kweli…

…..na mazungumzo yalianza yeye ni msemaji na mimi ni msikilizaji…

Alianza kwa kutupongeza kwa kazi kubwa na nzuri tunayoifanya ya kuelimisha na kugusa maisha ya watanzania walio wengi.

Haikuwa ishu sana,

Godfrey aliendelea kutoa ya moyoni, niseme tu ukweli kabla sijasoma kitabu cha Biashara Ndani Ya Ajira.

Kwanza nilikuwa sifikirii kufanya biashara kabla sijakamilisha malengo yangu mengine ambayo makubwa zaidi ilikuwa ni kujenga Nyumba yangu nzuri na ningeweza kufungua biashara zangu na kuacha kazi na kuendesha maisha yangu binafsi.

Lakini nilikuta napitia wakati mgumu sana katika kufanikisha hilo kiasi kwamba majukumu yalikuwa makubwa kuliko hata kipato changu matokeo yake nilitumbukia kwenye madeni.

Baada ya kushiriki katika semina ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA iliyoendeshwa kwa njia ya mtandao niliweza kujipatia ZAWADI ya vitabu 15 ambapo mpaka sasa nmeshasoma vitabu 7 ikiwemo kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA.

Niseme tu semina ile na vitabu hivi vimejaa matunda tele katika mafanikio yangu.

Kwanza nmefanikiwa pakubwa kudhibiti kipato changu ikiwemo kujilipa kwanza 1/10 ya kipato changu.

Pili kuhakikisha mishahara yangu inakutana, mpaka sasa zile ndoto zangu za kujenga nyumba kama zimetimia kwani nimeshainua nyumba yangu iko katika hatua ya mwisho za uezekaji,

Nilifanikiwa kuanzisha biashara na sasa hivi tunavyozungumza ina thamani ya 12.9Milioni

Nashukuru nilifanikiwa kulipa madeni yote ya nyuma ambayo nilikuwa nadaiwa na benki,

…..na hii ni nguvu ya ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

Changamoto katika kufikia ushindi na kufanikisha hayo yote niliyoyataja hapo haikuwa kazi rahisi sana kama ambavyo mtu mwingine anaweza kufikiria,

….kwani ilinibidi nibadili mtindo mzima wa maisha yangu kuanzia kula , kulala, kutembea hiyo yote ni kutaka kufanyia kazi yale ambayo nilikuwa nmejifunza.  

Changamoto kwenye kula kuna wakati niligombana na familia yangu kwa kuonekana kutokuwajali sana katika swala la kula vizuri lakini ilibidi niwaelimishe hasa hasa mke wangu ni nini nmekusudia kufanya juu ya maisha yetu,

….sote sisi kama familia namshukuru mungu alinielewa na kuona ile hali ni ya kawaida na itakubidi kupitia hali hiyo ili kufikia mafanikio makubwa tunayoyahitaji.

Nikija kwenye changamoto niliyokutana nayo wakati wa  kuanzisha biashara kwanza ilikuwa ni MTAJI.

Mtaji ulikuwa mdogo na hivyo ilinisababisha niishi kwa nidhamu ya hali ya juu,

…..kila pesa iliyokuwa inapita mkononi kwangu nilitenga 1/10 kwaajili ya kuweka akiba.

Nashukuru sana na ninakiri kwamba nidhamu hii ndiyo iliyonifikisha hapo nilipo kwa sasa nina vyanzo vitatu vya kuniingizia kipato.

Akamalizia kwa namna hiyo…

Nikamshukuru kwa mda wake , kabla hajakata simu nikamuuliza UNAWASHAURI NINI WALE AMBAO WAMEAJIRIWA LAKINA HAWANA NJIA NYINGINE YA KIPATO?…

Akajibu…

Ushauri wangu kwa wale ambao wameajiriwa lakini hawana njia nyingine ya kuingiza kipato ni hivi” Hakuna maisha maisha magumu sana ambayo mtu anaweza kuchagua kuishi kwa hiari yake hapa duniani , basi ni kuishi kwa kutegemea chanzo kimoja pekee ,

…haya ni maisha magumu sana na huwa hayana uhuru.

Kuwa na chanzo kimoja cha kipato ni UTUMWA MKUBWA sana kwenye maisha yako.

Rafiki yangu, wewe ni mshindi….

Kama Godfrey kaweza wewe ushindwe una nini?…

Angalia!..

Godfrey kashauri wale wote ambao wanataka kuungana naye kwenye safari yake ya ubilionea.

……basi huna budi kusoma vitabu viwili:

KITABU; ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na

KITABU; BIASHARA NDANI YA AJIRA.

Kupata vitabu vyote viwili piga simu namba; 0752977170.

Kupata OFA Yako Ya Mwezi Wa Pili.

Rafiki Yako Anayekujali Sana,

Bwana Rama|COPYWRITER OF SOMA VITABU TANZANIA|