2973; Wape sababu ya kukuheshimu.
Rafiki yangu mpendwa,
Tunajifunza mambo mengi kwenye biashara na mauzo.
Na mengi sana tunayojifunza yameegemea kwenye kuwajali sana wateja na kuweka maslahi yao mbele.
Hayo ni mambo yenye nguvu na ushawishi mkubwa kwa wateja.
Lakini pia kuna wateja wanachukulia kujali kwetu kama sehemu ya kutaka kutunyanyasa.
Kwa kuwa tumechagua kuwajali sana na kuweka maslahi yao mbele, wanaona tuna uhitaji mkubwa na bila wao hatuwezi kuendesha biashara zetu.
Na hapo ndipo wanaanza manyanyaso yao.
Wanaanza kutupangia ni kwa namna gani tuendeshe biashara zetu, ili kuendana na matakwa yao.
Wanatutaka tuwauzie kwa bei ndogo hata kama ina hasara kwetu.
Wanataka tuwakopeshe, kwa ahadi kwamba watalipa baadaye, lakini tukishafanya hivyo wanakuwa wasumbufu sana kwetu.
Hayo yanatuchanganya na kutuweka njia panda, tunajikuta hatujui nini tufanye katika hali hizo.
Hapa tunakwenda kujifunza mambo muhimu ya kufanya na kuzingatia ili wateja watupe heshima kubwa kwa namna tunavyowajali.
Kwanza kabisa tunahakikisha kuna vitu tunawapa wateja wetu ambavyo hawawezi kuvipata kwa wafanyabiashara wengine wowote.
Siyo lazima iwe bei nafuu, japo kama unaweza hilo litakuwa zuri.
Inaweza kuwa huduma bora kabisa ya kuwajali na kuweka maslahi yao mbele.
Inaweza kuwa uhakika wa kupata bidhaa au huduma wakati wote anapokuwa na uhitaji.
Inaweza kuwa uharaka wa kupata kile wanachonunua.
Inaweza kuwa huduma za ziada wanazopata baada ya manunuzi.
Au inaweza kuwa jinsi unatatua changamoto wanazokutana nazo kwenye kile unachowauzia.
Kwa vyovyote vile, hakikisha wateja wanaponunua kwako kuna thamani kubwa wanayoipata ambayo hawawezi kuipata kwa wafanyabiashara wengine wowote.
Ni wewe uchague tu thamani gani utakayowapa kisha jenga msimamo hapo.
Halafu basi, mteja atakapoleta kiburi na kutaka kukupangia namna gani uendeshe biashara yako, mjibu tu kwa unyenyekevu kwamba kwa upande wako hilo limeshindikana.
Mweleze wazi ungependa sana kumhudumia na kumpa thamani, ila kama ameshindwa kwenda na utaratibu uliopo, itashindikana kumhudumia vizuri.
Hapo utamwacha aende huko kwingine ambapo anaona ataweza kuwapangia jinsi ya kuendesha biashara.
Na huko ataikosa ile thamani aliyokuwa anaipata kwako.
Hilo litamfanya arudi kwako, na atakaporudi atakuwa tayari kufuata utaratibu uliopo.
Akirudi mpokee vizuri, mshukuru kwa kurudi na mpe thamani kubwa kama ambavyo umekuwa unatoa.
Usimwonyeshe kisirani kwamba wewe umeshinda na yeye amehangaika bure.
Onyesha kumjali zaidi na mhudumie vizuri.
Yote hayo yatamfanya mteja afuate utararibu ulioweka ili asikose thamani unayotoa.
Itawafanya wakuheshimu na kufuata maelekezo unayowapa.
Utaweza kufanya hili kama tu una thamani ya tofauti unayowapa wateja na una wateja wengi ambao umewatengeneza na unaendelea kuwatengeneza.
Kama hakuna cha tofauti ambacho wateja wanapata kwako, ambacho hawawezi kupata kwingine, na kama huna wateja wengi uliowatengeneza, utajikuta ukiwa mateka kwa wateja wachache ulionao.
Watakupelekesha wanavyotaka wao na wataiua biashara yako kwa ubinafsi wao.
Hakikisha wateja hawachanganyi kujali kwako kwa kuona ni udhaifu.
Chora kabisa mstari ambao mteja akiuvuka anakuwa amejikosesha mwenyewe kile unachouza.
Kisha weka juhudi kubwa sana kuhakikisha unatoa thamani kubwa na unatengeneza wateja wengi.
Hakikisha kwa upande wako una machaguo mengi kuliko mteja na hilo ndiyo litakalokupa nguvu.
Kuna wateja watajichanganya, kwa kudhani wataweza kukupangia uendesheje biashara yako. Na hapo ndipo watashangaa namna utakavyokuwa tayari kuwaacha waende na wakifika huko nje, hawatakuwa na budi bali kurudi.
Nisisitize sana haya mawili; TOA THAMANI KUBWA WASIYOWEZA KUIPATA KWINGINE na KUWA NA WATEJA WENGI SANA UNAOWATENGENEZA NA KUWAHUDUMIA.
Hayo mawili ndiyo yatakayokupa nguvu kubwa ya kusimamia yale uliyopanga kwenye biashara yako na hata kuiendesha biashara yako kwa furaha kubwa.
Kuwa tayari kumpoteza mteja yeyote na biashara isitetereke sana.
Hata kwa wateja ambao tayari wanaelewa thamani yako na kuiheshimu, usibweteke, hakikisha unatengeneza wengi zaidi wa aina hiyo.
Kwani watu huwa wana tabia ya kuzoea vitu na kujisahau.
Mteja wako mzuri anaweza kudhani unachompa anaweza kupata popote.
Na hilo litamfanya aanze kuwa na kiburi na kukupangia uendesheje biashara yako, akijua hutakuwa na uthubutu wa kumpoteza.
Ni katika nyakati kama hizo ndiyo utamshangaza kwa jinsi utakavyokuwa tayari kumpoteza, ukijua hakuna atakapoweza kwenda kupata thamani unayompa.
Na pia ukijua akiondoka, kuna wengine tayari wanashika nafasi yake.
Kumbuka hukuingia kwenye biashara unyanyasike maisha yako yote.
Ungetaka hivyo ungeweza kuajiriwa na wengine na maisha yako yakaenda hivyo.
Umeingia kwenye biashara ili ujijengee uhuru mkubwa wa muda, kipato na maisha kwa ujumla, ufanye yale unayotaka na kufurahia kufanya.
Kama hutatoa thamani kubwa na kutengeneza wateja wengi, wateja watakunyanyasa na kukunyima uhuru ulioufuata kwenye biashara.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Machaguo mengi kuliko mteja.
Machaguo mengi kuliko mfanyakazi.
LikeLike
Hiyo inakupa nguvu kubwa.
LikeLike
Asante kocha,nitafanya kwa thamani kubwa ili mteja aone umuhimu wa bidhaa zangu.na sio anipangie anachotaka.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante sana Kocha kweli tujenge biashara kwa kutoa thamani kubwa hakika tutapata wateja tunaowataka
LikeLike
Kabisa, thamani lazima itathaminiwa.
LikeLike
Ahsnate sana kocha, sitawafanya wateja wanipangie bali nitawapa sababu ya kuheshimu
LikeLike
Hilo linawezekana kabisa.
LikeLike
Thamani kubwa na ya kipekee ambayo nahakikisha nitazidi kwa washindani wangu hata akienda huko aone kuna cha ziada bado hapati huko alipokwenda ,kimsukume arudi.Akirudi nisimpokee vibaya kama aliekosea bali awe tayari kufuata utaratibu uliopo na kuuheshimu.
Bila viwango wengi watataka kukupelekesha tuu watakavyo wao na kukuharibu.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kutoa thamani kubwa ambayo mteja hawezi kuipata sehemu nyingine ndiyo itakayomfanya mteja akuheshimu.
LikeLike
Kabisa.
Kama huna maajabu atakupangia ufanyeje biashara yako.
LikeLike
Hakikisha wateja hawachanganyi kujali kwako kwa kuona ni udhaifu.
LikeLike
Watu huwa wanajisahau haraka sana.
Tuwakumbushe mara kwa mara.
LikeLike
Ahsante sana Kocha Dr Makirita Amani kwa nondo ya leo, nimeikubali sana.
“Sikuingia kwenye biashara kunyanyasika….” Kwahiyo nipo radhi mteja aondoke aiache biashara yangu kuliko kunipangia Nini Cha kufanya kwenye biashara yangu.
🔥🔥🔥 Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Tutoe thamani kubwa mno ili itupe nafasi ya kufurahia biashara kwa kufanya kazi na wateja sahihi.
LikeLike
Kujenga hesitate yako kwa kutoa thamani bora kwa wateja
LikeLike
Thamani tunayotoa iwe kubwa sana.
LikeLike
Nitakahakikisha naendelea kutoa huduma Bora zaidi
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Wakati mwingine wateja wanachukulia ukarimu kwamba ni udhaifu na kujaribu kutaka kukunyanyasa kupitia hilo, kushinda hili unapaswa kuwa bora na kuwa na machaguo mengi pamoja na kuwa na vigezo na masharti yako binafsi.
LikeLike
Hakika, tutoe thamani kubwa mno, halafu tuwaonyeshe mahali mstari ulipo ili wasiuvuke.
LikeLike
Ahsante kocha nakwenda kutoa thamani zaidi ambayo haiwezi kupatikana kokote.
LikeLike
Vizuri, toa thamani kubwa sana.
LikeLike
Kweli kabisa
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Nimechagua kutoa thamani kubwa na kutengeneza wateja wengi kiasi kwamba hakutakua na mteja wakunipangia namna ya kuendesha biashara yangu pale atakapotaka nifanye anachotaka yeye.
LikeLike
Vizuri, fanya hivyo.
LikeLike
Asante Kocha,
Nitawapa Wateja Wangu sababu ya kuniheshimu kwa:-
1. Kutoa thamani kubwa wasiyowweza kuipata kwingine.
2. Kuwa na wateja wengi sana ninaowatengeneza na kuwahudumia
Najua kuwa nimeingia biashara ili:-
1, Kujijengea uhuru mkubwa wa muda,
2. Kujijengea uhuru mkubwa wa kipato
3. Kujijengea uhuru mkubwa wa maisha kwa ujumla,
4. Kufanya yale ninayotaka na kufurahia kufanya.
Hivyo basi:-
LikeLike
Well summarized.
Tukae humo ili tujenge na kufurahia uhuru tulioufuata kwenye biashara.
LikeLike
Tutoe thamani kubwa sana na tutengeneze wateja wapya tunaowahudumia hapa ndipo penye heshima yetu Kwa wateja
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Tutoe thamani kubwa sana na tutengeneze wateja wapya tunaowahudumia hapa ndipo penye heshima yetu Kwa wateja
Asante sana.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Wateja wanajua wao ni wafalme kwa hiyo wanaweza kutufanya chochote kile.
LikeLike
Muhimu tuwakumbushe ukomo wao unaishia wapi, maana kwa utashi wao hawajuagi mwisho.
LikeLike
Na huko ataikosa ile thamani aliyokuwa anaipata kwako.
Hilo litamfanya arudi kwako, na atakaporudi atakuwa tayari kufuata utaratibu uliopo.
LikeLike
Kabisa, maana anajua kuna kitu hawezi kukipata pengine.
LikeLike
Nitahakikisha mteja havuki mstari wa taratibu nilizoweka.
LikeLike
Mstari uwe umekolezwa kabisa, asije kusema hakuuona.
LikeLike
Tuwape wateja huduma Bora kabisa pia tuweke maslahi yao mbele. Vile vile tuhakikishe tuna wateja wengi .
Tuhakikishe wateja wanaelewa kwamba kuwajali wao sio udhaifu , hivyo Kama Kuna mteja atataka akupangie jinsi ya kuendesha biashara zete , kwa unyenyekevi mwambie Mimi ninafuata utaratibu wangu ambao ni huu. (ASANTE SANA KOCHA, NI MUONGOZO BORA KABISA)
LikeLike
Kwa namna hiyo tutaendesha biashara zetu kwa uhuru mkubwa.
LikeLike
kutoa thamani bora kabisa ambayo hawezi kupata kwa huraisi ili biashara inipe heshima na sio kuninyanyasa bali kunipa muda zaidi na kuwa uhuru zaidi
sukrani kocha kwa makala nzuri sana.
LikeLike
Tuhakikishe uhuru tulioufuata kwenye biashara tunaupata.
LikeLike
Kwa kweli ukitoa huduma bora kuliko watu wengine, ni sababu tosha ya watu kukuheshimu na kukubali misingi unayoyasimamia. Lakini ukiwa na huduma mbovu hata kama una misiingi bora unayoisimamia bila shaka wateja hawaheshimu hiyo misingi yako na watakukimbia.
LikeLike
Hakika, kushindwa kutoa huduma bora ni kuwapa watu nafasi ya kukuendesha wanavyotaka wao, hata kama inakuumiza wewe.
LikeLike
Thamani kubwa na wateja wengi wapya.Kwa kuzingatia haya basi wateja watatuheshimu.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Napaswa kutoa thamani kubwa kwa wateja, napaswa kutengeneza wateja wengi pia.
Wateja hawatakiwi kuninyanyasa.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Tukatae unyanyasaji kwa kutoa thamani kubwa sana.
LikeLike
Nipo kwenye biashara ili nijengee uhuru mkubwa wa muda, kipato na maisha kwa ujumla. Asante sana Kocha Dr. Amani Makirita
LikeLike
Linda sana uhuru huo unaoujenga, maana ukizembea watu watakuchukua mateka na kukunyanyasa.
LikeLike