3013; Muda na biashara.
Rafiki yangu mpendwa,
Mtu mmoja aliwahi kunukuliwa akisema, kama umewapenda watu wawili na unatakiwa kubaki na mmoja, unatakiwa kumchagua wa pili, kwa sababu kama ungekuwa unampenda kweli wa kwanza, usingeenda kwa wa pili.
Kwa kuhamishia msingi huo kwenye biashara nakwenda kukuambia; kama kuna kitu chochote unachokipa muda wako zaidi ya unavyoweka kwenye biashara yako, unapaswa kuachana na biashara na kuendelea na kitu hicho.
Kama kuna kitu kinapata nafasi kubwa kwako kuliko biashara yako ni kiashiria kwamba biashara siyo kipaumbele cha kwanza kwako.
Na kama biashara siyo kipaumbele cha kwanza kwako, ni vigumu sana kufanikiwa.
Biashara ni kama mpenzi mwenye wivu,
Ikiona unapeleka umakini wako kwenye kitu kingine chochote, inaona unaisaliti na hivyo yenyewe inakusaliti pia.
Pale unapokuwa na vipaumbele vingine zaidi ya biashara yako, biashara inashindwa kusimama imara.
Kwenye hii safari ya ubilionea tuliyopo, biashara inapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza kwako.
Unapaswa kuifikiria biashara yako muda wote.
Unapaswa kuweka umakini wako wote kwenye biashara yako.
Unakoweka umakini wako ndiko kunakokua.
Kama unaona hautakuwa mtu wa kawaida kama utaipa biashara yako kipaumbele cha kwanza, kumbuka watu wa kawaida siyo mabilionea.
Hivyo chagua mapema, unataka kuwa mtu wa kawaida na uendeshe maisha ya kawaida au unataka kuwa bilionea na uendeshe maisha ambayo siyo ya kawaida.
Maisha ni kuchagua na kile unachochagua ndiyo kinachoamua maisha yako yaweje.
Mara nyingi umekuwa unachagua vitu bila kujua umechagua, yaani unajikuta tu unafanya kwa mazoea au kwa kufuata mkumbo.
Amka sasa na uchague kwa akili zako timamu.
Kama kweli unautaka ubilionea, biashara inapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza kwako, bila ya kujali upo ngazi gani ya kibiashara kwa sasa.
Maisha mengine yataendelea, lakini biashara haitaathiriwa na chochote kinachoendelea kwenye maisha yako.
Biashara itaendelea kusimama imara kwa sababu ndiyo kipaumbele cha kwanza kwako.
Na kama umegundua kuna vitu vingine ulikuwa umevipa kipaumbele kuliko biashara yako, lakini hutaki kuiacha biashara yako, basi acha vitu hivyo mara moja.
Yaani viache ghafla na peleka umakini wako wote kwenye biashara.
Usiseme unaviacha kidogo kidogo, maana tayari vilishakutawala, hivyo kubaki navyo vitaendelea kujipenyeza na kupata umakini wako.
Wewe achana navyo mara moja na ombwe linalojengeka lijaze na biashara yako.
Kwenye maisha, tunachokipa umakini ndiyo kinachokua.
Kama biashara yako haikui, ni kwa sababu huipi umakini wa kutosha.
Kuna vitu vingine unavyokuwa umevipa kipaumbele kikubwa kuliko biashara yako.
Zoezi la haraka la kujua vitu gani unavipa umakini kuliko biashara yako, orodhesha vitu vyote unavyovipa muda wako kwa kipindi cha wiki nzima.
Kisha pata jumla ya masaa yanayoenda kwenye mambo yote unayofanya.
Kama biashara yako inapata chini ya masaa 84 kati ya masaa 168 kwa wiki haina nafasi ya kutoboa.
Yaani kama biashara yako haipati zaidi ya nusu ya muda wako wote ni kama unacheza tu.
Biashara na muda ni sawa na ushindi kwenye chaguzi za kidemokrasia, anayepata zaidi ya nusu ya kura ndiye mshindi.
Kwenye wiki kuna masaa 168, ambayo ukigawa kwa mbili ni masaa 84 ambayo ukiyagawa kwa sita ni masaa 14 na ukigawa kwa saba ni masaa 12.
Kama biashara yako inapata chini ya masaa 84 kwa wiki, itapata tabu sana, utahangaika sana lakini haitaweza kutoboa.
Kwa wale ambao bado wapo kwenye ajira na wanaendesha biashara, ambapo hawawezi kuziacha ajira zao mara moja, wanapaswa kuyaacha maisha.
Wanapaswa kuifanya biashara kuwa kipaumbele cha kwanza na ajira kipaumbele cha pili, halafu kutokuwa na kipaumbele kingine chochote.
Yaani hawapaswi kuwa na maisha ya kawaida kabisa.
Maisha yao yote yanapaswa kuwa biashara na kazi, muda wote ambao hayupo kwenye kazi anapaswa kuwepo kwenye biashara.
Tukirudi kwenye hesabu zetu, kwa sheria ya kazi, mtu anatakiwa kufanya kazi masaa 45 kwa wiki.
Na biashara inataka masaa 84 kwa wiki.
Jumla inakuwa masaa 129 kwa wiki, ya kazi na biashara.
Ukichukua jumla ya masaa 168 ya wiki na ukatoa masaa 129 ya kazi na biashara unabaki na masaa 39 kwa wiki.
Ukiyagawa masaa 39 kwa siku 7 unapata masaa 5 na nusu kwa siku.
Sasa unadhani nini unaweza kufanya kwenye huo muda uliobaki nao? Ni kitu kimoja tu, kulala.
Makala ya leo imekuwa na hesabu nyingi lakini ni tumaini langu kwamba umeelewa.
Na kama hujaelewa, rudia tena na tena kusoma mpaka uelewe kila sentensi kwa uhakika na uchukue hatua.
Ipe biashara yako ushindi kwa kuipa zaidi ya nusu ya muda wako wa wiki.
Usiwe na kipaumbele kingine kinachoizidi biashara yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nitaipa biashara yangu muda zaidi Ili iweze kukua na kustawi.
LikeLike
Ahsante sana kocha, nimechagua biashara kama kipsumbele changu cha kwanza na nitaipa muda wangu wote siku zote
LikeLike
Kwa hesabu hii nina uhakika wengi tuko nje ya hayo masaa na hata kama tunatimiza tunatimiza kwa kukaa kwenye biashara na kufanya jambo lingine yaani uko kwenye biashara lakini unaangalia mitandao ya kijamii muda wa kupiga simu kwa wateja
LikeLike
Biashara itakua ndio kipaumbele changu
LikeLike
Asante sana kocha huu ni ukweli halisi tunahitaji kuwekeza muda wetu kwa hakika kwenye biashara angalau saa 84 kwa wiki. Nitalifanyia kazi hili
LikeLike
Kwa sasa biashara ndio kipaombele changu cha kwanza na ajira ndio kitu cha pili,sipasw kupoteza muda wangu kwenye vitu vingine
LikeLike
Kwenye maisha tunachokipa umakini ndicho kinacho kuwa …. Tuzipe umakini mkubwa biashara zetu
Asante
..
LikeLike
naweka muda na vipaumele vyangu kwenye biashara ili ikue na kutokuwa mtu wa kawaida.
shukrani kocha.
LikeLike
Si mchezo hii ni kupotea duniani Kwa muda na kuingia ulimwengu mwingine…
Hapa nimewaza muda Wa ibada,muda Wa familia?
Masaa 5.5 hakuna kingine zaidi ya kulala…
Hapa inahitaji kujitoa kafara kabisa…
Biashara kipaumbele changu Cha kwanza nitaipa masaa yote stahiki bila kuiba muda Wa biashara
Nitafanya kazi Kwa bidii Ili kufikia uhuru Wa kifedha na Uhuru Wa Muda Ili kufikia ubilionea nimechagua kutokuishi maisha ya kawaida.
Uhuru huu utanisaidia kupata muda Wa kutosha na familia yangu na hata maisha ya kijamii…
LikeLike
Hii hesabu leo si mchezo kwenye ukuaji wa biashara na muda naoupa
LikeLike
Zaidi ya nusu ya muda ni reasonable kabisa, kuna watu zamani walifanya mambo mengi sana kwa muda huo huo. Nitahakikisha biashara inapata kuanzia masaa 16 mpaka 18 kwa siku.
LikeLike
Nitaipa biashara yangu zaidi ya 80% ya muda wangu.
LikeLike
Kwenye hii safari ya ubilionea tuliyopo, biashara inapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza kwako.
Unapaswa kuifikiria biashara yako muda wote.
Unapaswa kuweka umakini wako wote kwenye biashara yako.
Unakoweka umakini wako ndiko kunakokua.
Ahsante sana Kocha.
Naweka umakini wangu wote kwenye biashara yangu.
LikeLike
Asante kocha,Biashara ndo kipaombele cha kwanza na kazi ni ya pili.
LikeLike
Haya sasa maneno kuntu”huu ujumbe ukiweka na ujumbe wa mwezi April, Biashara iheshimiwe na kuthaminiwa na watu wote,kwangu kazi ninayo,Ila biashara kweli kwangu ni kipaumbele kikubwa
LikeLike
Safi sana, kaa humo.
LikeLike