3014; Kama hushindwi, unashindwa.
Rafiki yangu mpendwa,
Sisi binadamu huwa tunaepuka sana kushindwa.
Hiyo ni kwa sababu tumekuzwa tukiaminishwa kwamba kushindwa ni kubaya.
Tumeaminishwa anayeshindwa anakuwa na matatizo fulani.
Tangu utotoni, kushindwa kumekuwa kukiadhibiwa kwa namna mbalimbali.
Hilo limetujengea hofu kubwa kwenye kushindwa.
Na hofu hiyo imepelekea tusiwe tayari kujaribu vitu vipya, kwa kuwa hatutaki kushindwa.
Ili pia tusishindwe, tumekuwa tunajiwekea ndoto na malengo madogo sana.
Japo ndani yetu tunaweza kuwa tunataka zaidi, hatuthubutu kwenda na kile tunachotaka, kwa sababu tunahofia kushindwa.
Tunaweza kuona kutokushindwa ni ushindi mkubwa, kwa sababu jamii haipati nafasi ya kutukosoa na kutubeza kwenye kushindwa kwetu.
Lakini kwa uhasilia, kutokushindwa ni kushindwa.
Kama hushindwi kwenye maisha yako, maana yake hafanyi vitu vipya na vikubwa.
Unafanya vitu vidogo na vya kawaida sana, kitu kinachokukwamisha kupata matokeo makubwa na ya tofauti.
Hakuna kitu kinacholevya kama ushindi.
Ushindi unaleta kiburi na majigambo.
Ushindi unafanya mtu ajione tayari anajua na kuweza kila kitu, hivyo kutokuwa tayari kujifunza.
Hayo ndiyo yanayopelekea wengi kushindwa vibaya baada ya kuwa wamepata ushindi kidogo.
Kushindwa ni mwalimu mzuri sana.
Kushindwa kunaleta unyenyekevu.
Kushindwa kunafanya mtu ajione kuna mengi hajui hivyo anapaswa kujifunza.
Hayo ndiyo yanayopelekea watu kupata ushindi baada ya kuwa wameshindwa.
Ni muhimu uwe na ndoto na malengo makubwa,
Ambavyo vitakusukuma ufanye zaidi ya ulivyozoea.
Hilo litakuweka kwenye mazingira ya kushindwa.
Kitu ambacho kitakusukuma uwe bora zaidi na kuweza kufikia ndoto na malengo makubwa uliyonayo.
Na pale unapofikia ndoto na malengo hayo, usibweteke, badala yake weka ndoto na malengo mengine makubwa zaidi na pambana kufanyia kazi.
Kila wakati hakikisha unakuwa kwenye hali ya kujisukuma zaidi ili kuweza kupata matokeo makubwa zaidi.
Ukibweteka na matokeo yoyote unayoyapata, kwa kujiona tayari umeshashinda, unakuwa umejiweka kwenye nafasi ya kushindwa zaidi.
Kushindwa ni ushindi mkubwa kama utatumia vizuri.
Ondoa kila hofu ya kushindwa na mara zote kuwa katika hali ya kufanya mapya na makubwa ambayo hujawahi kuyafanya.
Unaposhindwa unajifunza na kuwa bora zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante kocha,Sintabweteka na ushindi badala yake ni kujisukuma na kuweka malengo makubwa na kuyafanyia kazi.
LikeLike
Kuogopa kushindwa kumenifanya mara nyingi kubaki kulinda goli na kuacha kushambulia lakini kuwa katika jamii ya KCM imenifanya niaznze kushambulia na kunihoji kila siku, wiki, mwezi na mwaka.
Kwa sasa asiliyangu ni kushambulia.
LikeLike
Kweli inahitajika kujifunza zaidi na kutoogopa kujaribu vitu vipya kwenye kuelekea ushindi kwenye maisha.
LikeLike
Nitajitahiji zaidi kuweka malengo bila kuogopa kushindwa. Kushindwa na kunyanyuka ni njia sahihi yakunifikisha kwenye mafanikio makubwa.
LikeLike
Naacha kuogopa kufanya makubwa na kuweka mbali hofu ya kushindwa Ili nifanye makubwa.
LikeLike
Kushindwa ni sehemu ya maisha ukishindwa maana yake kuna sehemu haupo vizuri inabidi ujifunze zaidi
Asante
LikeLike
Hakuna kitu kinacholevya kama ushindi.
Ushindi unaleta kiburi na majigambo.
Ushindi unafanya mtu ajione tayari anajua na kuweza kila kitu, hivyo kutokuwa tayari kujifunza.
Hayo ndiyo yanayopelekea wengi kushindwa vibaya baada ya kuwa wamepata ushindi kidogo.
LikeLike
Ni sahihi kuna watu wanalewa kwa sababu ya ushindi wanaoupata
LikeLike
Kama hushindwi kwenye maisha yako, maana yake hufanyi vitu vipya na vikubwa.
Unafanya vitu vidogo na vya kawaida sana, kitu kinachokukwamisha kupata matokeo makubwa na ya tofauti.
Ahsante Kocha.
Nimekuelewa sana.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante sana kocha,
Nimejifunza kuwa kutokushindwa katika maisha ni kushindwa na kama sishindwi kwenye maisha yangu maana yake sifanyi vitu vipya na vikubwa.
Nitajiwekea malengo makubwa na kufanya makubwa na kama nikishindwa sitakata tamaa kwani nitakuwa nimejifunza.
LikeLike
Tupambanie makubwa na tujifunze kupitia kushindwa.
LikeLike
Asiye kubali kushindwa huyo sio mshindani. Ni msemo wa toka enzi kutuony3sha kuwa hatuna Budi kukubali kushindwa ili tuwe kwenye mashindano ya haki. Na wanasema kosa sio kosa Ila kutudia kosa ndiyo kosa lenyewe. Kushindwa kunanipa fursa ya kujifunza na kusahihisha makosa ya kwanza.
Nitayakubali makosa na kushindwa kwangu ili nijirekebishe na kupiga hatua.
LikeLike
Tushindwe ili tuweze kushinda.
LikeLike
Nikushkuru sana kocha kwa upekee kunitoa kwenye hofu na uoga,nimechelewa sana kuanza biashara kwa sababu ya hayo,kwa sasa siongopi tena kushindwa maana najua Nyuma ya ushindi kuna kushindwa nyingi.
LikeLike
Safi sana, endelea kuwa jasiri na imara.
LikeLike
Ahsante sanaa kocha
LikeLike
Karibu.
LikeLike