3029; Msimu wa HAPANA.
Rafiki yangu mpendwa,
Hakuna neno moja lenye nguvu kubwa sana kwenye safari yako ya mafanikio kama neno HAPANA.
Hapana siyo tu neno, bali ni sentensi inayojitosheleza.
Ili uweze kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako na kufika kule unakotaka kufika, lazima useme HAPANA kwa mambo mengi sana.
Kusema HAPANA ni rahisi kueleza, lakini ngumu sana kutekeleza, hasa pale tunapohitajika kusema HAPANA kwenye vitu ambavyo tumeshazoea.
Pia kusema HAPANA ni rahisi pale inapokuwa mara moja moja, lakini ngumu sana pale inapokuwa kwenye mengi na kwa muda mrefu.
Kwenye safari kubwa ya ubilionea ambayo tupo, siyo tu tunahitaji kusema HAPANA kwenye baadhi ya vitu, bali tunahitaji kusema HAPANA kwenye kila kitu isipokuwa yale tu yanayotufikisha kwenye lengo.
Na hapo ndipo tunahitaji kuingia kwenye msimu muhimu sana wa maisha yetu, MSIMU WA HAPANA.
Msimu wa HAPANA ni kipindi cha maisha ambapo tunasema hapana kwa mambo yote ambayo hayana mchango kwenye lengo kuu tulilonalo, yaani yote kabisa.
Umakini wetu wote unakwenda kwenye yale tu yanayotufikisha kwenye lengo kuu tulilonalo.
Msimu wa HAPANA ni kipindi ambacho kinahitaji ujasiri wa hali ya juu, kwani mengi unayohitaji kuyakataa tayari ni mazoea kwenye maisha yako.
Kwenye huu msimu wa HAPANA, siyo tu unasema HAPANA kwa yale ambayo ni usumbufu, bali pia unasema HAPANA kwa yale ambayo ni mazuri kwenye maisha yako, lakini hayana mchango kwenye malengo makubwa uliyonayo.
Hapa kuna maeneo matano ya maisha yako ambayo unapaswa kuyasemea HAPANA kwenye huu msimu wa HAPANA;
Moja; Hapana kwa familia.
Hapana kubwa na ngumu unayopaswa kusema kwenye maisha yako ni kwa familia yako.
Familia yako ina tabia ya kutaka kukupangia ni namna gani uende na maisha yako.
Inaweza kufanya hivyo kwa nia njema kabisa, kwa sababu haitaki uumie, lakini nia hiyo njema haiwezi kukufikisha kwenye mafanikio makubwa unayoyataka.
Hivyo ni lazima useme HAPANA kwa mambo mengi ambayo familia yako inataka kwako, ambayo hayaendani na lengo lako kubwa.
Ni vigumu kusema HAPANA kwa familia kwa sababu ina tabia ya kutumia hatia kukufanya ukubaliane nayo.
Pale unapochagua kufanya mambo yako unaonekana kama mtu usiyejali familia.
Lakini ukweli ni kwamba utakuwa na manufaa makubwa sana kwa familia yako pale utakapopata mafanikio makubwa.
Hivyo kubali lawama na hatia za muda mfupi ili uweze kupata mafanikio makubwa ya muda mrefu.
Mbili; Hapana kwa marafiki.
Marafiki ni kundi jingine ambalo unahitaji kusema HAPANA sana kwenye huu msimu ambao tupo.
Marafiki zako, ambao ni watu wa karibu sana kwako wana ushawishi mkubwa sana kwako.
Watu hao ni rahisi kukuondoa kwenye mambo yaliyo muhimu kwako na kukupeleka kwenye mambo ambayo siyo muhimu.
Pale unapochagua kuweka muda wako wote kwenye malengo yako makubwa, marafiki zako watakuwa wa kwanza kukulaumu kwamba huwajali tena.
Watakuonyesha kwamba umebadilika.
Hupaswi kujali hilo wala kuhofia kuwapoteza marafiki kwa sababu kubwa tatu;
1. Marafiki wa kweli watakuelewa na kuheshimu maamuzi yako, hivyo watakuunga mkono na kuendelea kuwa wa msaada kwako kufikia ndoto zako.
2. Hata kama marafiki zako hawatakuelewa, utakapofanikiwa, bado watakuwa wanakuhitaji sana, hivyo hakuna utakachopoteza.
3. Na hata kama utawapoteza marafiki wako kwenye msimu wa HAPANA, kwenye safari yako ya mafanikio utatengeneza marafiki wengine wanaoendana na aina mpya ya maisha yako.
Usiogope kusema HAPANA kwa marafiki zako wa karibu katika hiki kipindi.
Tatu; Hapana kwa fedha.
Kusema HAPANA kwenye fedha ndiyo eneo jingine gumu sana na ambalo wengi huwa wanashindwa.
Na hili linachanganya kidogo, japokuwa mafanikio makubwa unayoyapigania yanahusisha fedha, inabidi useme HAPANA kwenye fedha.
Hapa inamaanisha kusema HAPANA kwenye vifursa vidogo vidogo vinavyojitokeza vya kuingiza fedha, lakini haviendani na lengo kuu ulilonalo.
Kuna fursa zinaweza kujitokeza mbele yako za kuingiza fedha, lakini ukizifanyia kazi unakuwa umetoa muda na umakini wako kwenye lengo lako kuu.
Ndiyo utapata fedha kidogo kwenye fursa hizo, lakini unakuwa umejizuia kupata fedha nyingi zaidi kwenye fursa kubwa zaidi za baadaye.
Hivyo unapaswa kuwa na ujasiri wa kusema HAPANA kwenye fursa mbalimbali za kuingiza fedha zinazojitokeza mbele yako kila mara.
Weka akili, muda, nguvu na umakini wako wote kwenye lengo kuu unalofanyia kazi na matokeo utakayoyapata yatakuwa makubwa sana.
Huwa nasema, hela ndogo ni adui wa hela kubwa. Unapohangaika na fursa ndogo ndogo zinazokuingizia fedha kidogo, unakuwa umejizuia kwenye fursa kubwa zinazoweza kukuingizia fedha nyingi.
Usikimbizane na kila fursa inayoweza kukuingizia kipato, kataa fursa ndogo ndogo na nyingi zinazokujia ili ukae kwenye fursa yako kuu.
Nne; Hapana kwa matukio ya kijamii.
Kuna matukio mengi ya kijamii ambayo huwa yanachukua muda, nguvu na umakini wako mwingi.
Kuanzia burudani na starehe mbalimbali ambazo umeshazizoea, mpaka kwenye mambo unayohusiana na wengine kwenye jamii.
Hapa ni mambo kama sherehe, michezo, vikundi mbalimbali na matukio mengine yanayotaka muda wako.
Unahitaji kusema HAPANA kwa mambo yoyote yale ambayo yanachukua muda wako ambao ungeweza kuutukia kwenye lengo lako kuu.
Sema HAPANA kwa michezo mbalimbali unayopenda kuifuatilia.
Sema HAPANA kwa sherehe mbalimbali unazoalikwa kushiriki.
Huhitaji kuwa kwenye kila kamati, kila kikundi na mikusanyiko mingine ya kijamii.
Jamii inaweza kukufanya ujione una hatia kwa kukataa kuendana nayo kwenye kila kitu, lakini utakapopata mafanikio makubwa, utakuwa wa msaada mkubwa kwa jamii hiyo hiyo.
Hivyo usihangaike kuiridhisha jamii kwa kuenda vile inataka uende, pambania mafanikio yako makubwa na hayo yatakupa heshima kubwa kwenye jamii yako.
Tano; Hapana kwa tamaa za mwili.
Halafu sasa kuna kusema HAPANA kwenye tamaa za mwili.
Mwanafalsafa Seneca amewahi kusema; mwili inabidi uteswe ili uweze kuwa na utii kwenye akili.
Kama hutaweza kuutesa mwili wako, jua pia hutaweza kufikia mafanikio makubwa unayoyataka.
Na huutesi mwili wako kwa kuumiza kwa makusudi, bali unautesa kwa kuuambia HAPANA kwa tamaa mbalimbali ambazo mwili wako unakuwa nazo.
Sema HAPANA kwa tamaa ya kupata vilevi na mambo mengine ya kuburudisha mwili.
Sema HAPANA kwa tamaa ya kupumzika pale ambapo hujaweka kazi ya kutosha.
Sema HAPANA kwa tamaa ya kufanya mapenzi mara kwa mara hasa na watu wasio wenza wako halali.
Sema HAPANA kwenye tamaa ya kula vitu vitamu na mara kwa mara.
Mwili ni wako, unatakiwa uutumie kufika kule unakotaka kufika na siyo ukutumie wewe kuhangaika na tamaa mbalimbali.
Kama hutaweza kudhibiti mwili wako kwa kujiambia HAPANA, hutaweza kufanya makubwa.
Rafiki yangu mpendwa na Bilionea uliye Mafunzoni, tumeuanza rasmi MSIMU WA HAPANA.
Msimu huu utakwenda mpaka pale wote tutakapokuwa tumefanikiwa kujenga biashara zinazoweza kujiendesha zenyewe bila ya uwepo wetu wa moja kwa moja.
Kabla ya kufikia hatua hiyo, mambo yote ni HAPANA, isipokuwa tu kwenye biashara moja tunayojenga na kwenye uwekezaji tunaoendelea kufanya kidogo kidogo kila mara.
Kwa kipindi chote, akili yako, muda wako, nguvu zako na umakini wako wote unaweka kwenye kujenga biashara yako kuu na kufanya uwekesaji.
Mengine yote yasiyokuwa na mchango kwenye hayo mawili, jibu lake ni HAPANA.
Hiyo ni HAPANA ambayo haina mjadala.
Unahitaji kuwa imara sana kwenye huu msimu wa HAPANA, kwa sababu hakuna atakayekuelewa.
Utakutana na changamoto nyingi na hata kushindwa, lakini usirudi nyuma.
Huu ndiyo msimu wa kukaa kwenye mchakato kwa asilimia 100 bila kuyumba na kuambatana na watu sahihi kama kuwa hapa kwenye programu ya BILIONEA MAFUNZONI.
Uzuri ni kwamba, ukishapata mafanikio makubwa, kila mtu atakuja kwako, atakusifia na kuona umefanya vyema.
Ila kabla hujayapata mafanikio hayo, kila unachofanya unakosea.
Kubali hilo ili uweze kufika unakotaka kufika.
Rafiki, hebu fikiria ni hatua kubwa kiasi gani utakazopiga kwenye maisha yako kama kila siku kuanzia saa 10 alfajiri mpaka saa 2 usiku unaweka muda, nguvu, akili na umakini wako wote kwenye kujenga biashara yako kuu na kujenga uwekezaji?
Kwa hakika ni hatua kubwa mno mno.
Hivyo basi, kubali kukaa kwenye msimu huu wa HAPANA.
Karibu ushirikishe kwenye maoni hapo chini orodha ya mambo ambayo kuanzia sasa ni HAPANA kwenye huu msimu wa HAPANA.
Orodhesha yote mazuri uliyokuwa unayafanya ila hayana mchango kwenye lengo na kuanzia sasa acha kuyafanya.
Karibu kila mmoja kushirikisha hayo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Hapana ni sentensi iliyojitosheleza.
LikeLike
Haihitaji maelezo ya ziada.
LikeLike
Asante sana hapa siitajaji mjadala wa kusema hapana, ni kukaa kwenye mchakato wa mauzo.
LikeLike
Hakika, HAPANA inahitajika sana.
LikeLike
Hapana inakusaidia kuondoa usumbufu kwenye maisha yako.
Nitasema hapana mara zote.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hakika, bila HAPANA usumbufu utatupoteza.
LikeLike
Ahsante sana kocha.
Nitasema hapa kupoteza muda na marafiki
Nitasema hapana kutoa fedha kwa dharura za ndugu
Nitasema hapana kuhudhuria kila tukio la kijamii
Nitasema hapana matumizi mabaya yabfedha yasiyokuwa kwenye bajeti
Nitasema ndiyo kwenye kila jambo lenye mchango wa kukuza biashara yangu
LikeLike
Hongera sana.
Kaa kwenye msimamo huu.
LikeLike
Nasema hapana kwa
1.familia-kwa kutaka nishiriki kwenye kila tukio linalojitokeza kwenye familia
2.Marafiki-kuwa tayari kutengwa nao kwa kuniona siendani na vile wanavyotaka na nitatengeneza marafiki wengine wanaondana na mimi kwa msimu huu wa hapana
3.Mambo ya kijamii-kupunguza kushiriki kabisa baadh ya mambo ya kijamii
4.Fedha-kutaka kufanya kila fursa kwa kufikiri nitapata kipato zaidi kumbe ninapoteza fedha nyingi
5.Mwili-kupunguza masaa ya kulala ili kutumia muda huo kujenga na kukuza biashara yangu
LikeLike
Vizuri sana,
Simamia hizi hapana ili uweze kufanya makubwa.
LikeLike
Orodha ya masuala ambayo nilikuwa nafanya lakini sasa HAPANA
Hapana kutumia muda kuburuika
Hapana kutumia muda na marafiki kwenye group za watsap
Hapana kuchukua nafasi yoyote ya uongozi kwenye jamii
Hapana kwenye kufuatilia fedha za fursa ndogo
Hapana kwenye kushiriki sherehe au mikutano isiyonisaidia kufikia lengo
Hapana kwa mapumziko bila kazi ya kutosha
Ni Hapana kwa yote isipokuwa Biashara na Uwekezaji
LikeLike
Safi sana.
Simama kwenye HAPANA hizi ili ubaki na ndiyo kwenye yale makubwa.
LikeLike
Asante kocha,
1.Hapana kwenye kutembelea marafiki na kupoteza mda.
2.Hapana kushiriki shughuri za kijamii sherehe na vikao mbali mbali vya vikundi visivyo na tija kwangu.
3.Hapana kunywa pombe na vitu vitamu.
4.Hapana kutumia fedha bila mpangilio wa bajeti.
5.Hapana kutekeleza mipango ya familia kwa kushawishiwa bila lengo.
6.Hapana kuingia mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii na kushiriki kwenye kumbi za kuangalia mpira.
LikeLike
Safi sana kwa HAPANA hizi.
Baki na NDIYO ya mchakato pekee.
LikeLike
MSIMU WA KUSEMA HAPANA
1. Hapana kwenye mambo ya familia yasiyo na mchango kwenye lengo kuu
2. Hapana kwenye vifursa vidogo vidogo
3. Hapana kwa marafiki wasio na mchango kwenye MCHAKATO wangu
4. Hapana kushiriki Kila mambo ya kijamii, hasa sherehe
5. Hapana kwenye tamaa za mwili , kulala, kula vitamu , kutokukamilisha kazi
HAPANA! HAPANA ! HAPANA. HAPANA. HAPANA
LikeLike
Safi sana kwa HAPANA hizi.
Zisimamie kwa uhakika.
LikeLike
Hapana kwenye mambo mengi ya kijamii.Hapana kwenye matumizi zaidi ya mtandao.
LikeLike
Safi sana.
Baki na NDIYO ya kwenye mchakato.
LikeLike
Nitasema hapana kwa:
1. Familia pale wanapotaka kunipangia cha kufanya.
2. Kwa marafiki pale wanapojifanya wao ndio washauri wakuu.
3. Fedha zangu kuzifanyia matumizi ambayo hayako kwenye malengo yangu.
4. Matukio ya kijamii yanayonipotezea muda wangu.
5. Tamaa za mwili wangu kutaka kufanya kila kizuri kinachotaka akili yangu yangu kifanye. Kama anasa na TAREHE za mwili.
LikeLike
Safi sana, kuwa na msimamo kwenye haya.
LikeLike
Hapana Kwa Familia
Hapana Kwa marafiki
Hapana Kwa fursa ndogondogo nje ya lengo kuu
Hapana Kwa matukio ya kijamii yasiyonisaidia kufikia lengo
Hapana Kwa taratibu nyiiingi za kanisa Ili kukubalika
Hapana hapana hapana
Ndiyo ni Moja tuu_Kujenga biashara
LikeLike
Vizuri sana kwa hapana hizi.
Zisimamie kwa uhakika ili ndiyo ya kujenga biashara ipate nguvu.
LikeLike
kutokushiriki bm – HAPANA
kutokuwasiliana na wateja – HAPANA
kutokutembelea wateja – HAPANA
kwenda kuokota no – HAPANA
mwaka huu kutokununua hisa za CRDB NA NMB – HAPANA
kutokutekeleza ahadi – HAPANA
kutokutuma tathimini kwa wakati – HAPANA
kutoa fedha za biashara kiholela – HAPANA
kufatilia habari isiyonihusu – HAPANA.
NI HAPANA, HAPANA, HAPANA, HAPANA ISIPOKUWA KWENYE BIASHARA NA UWEKEZAJI.
LikeLike
Msimu wa HAPANA na upambe 🔥🔥
Ndiyo ni moja tu ya kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
Hapana kwa familia kunipangia cha kufanya
Hapana kwe vikao visivyo na tija kwangu
LikeLike
Vizuri sana, kuwa na msimamo kwenye HAPANA zako ili NDIYO ipate nguvu.
LikeLike
Asante sana Kocha. Hapana ambayo Bado inanipa changamoto ni ya familia. Nyingine zote naziweka kwenye vitendo mara moja
LikeLike
Unaposhindwa kusema HAPANA kwa yale yasiyo muhimu, unaishia kusema HAPANA kwa yaliyo muhimu.
LikeLike
1.Hapana Kwa marafiki wasio na tija
2.Hapana kwenye mitandao ya kijamii
3.Hapana kwenda kutembelea watu bila mpango
4.Hapana kuangalia mippira,siasa na mikutano isiyo na tija
Hapana Kwa michepuko
Asante
LikeLike
Safi sana, simamia HAPANA hizi ili NDIYO ya kukaa kwenye mchakato ipate nguvu.
LikeLike
Hapana Kwa Familia.
Hapana Kwa marafiki.
Hapana kwa fedha.
Hapana kwa matukio ya kijamii.
Hapana kwa tamaa za mwili.
Ahsante sana Kocha.
Nimekuelewa vizuri mno.
Sasa ni MSIMU WA HAPANA.
LikeLike
Kila la kheri katika kukaa kwenye msimu huu wa HAPANA.
LikeLike
HAPANA kwa yote ambayo hayachangii kwenye kupambania mafanikio yangu,kwa uchache maeneo ya Fedha,muda,na nguvu zangu.
Narudia kusema tena BIG NO!!!!!
LikeLike
Ni HAPANA kubwa, bila kujali.
LikeLike
Hapana kutumia muda kujiburudisha
Hapana kwa familia kupanga cha kufanya na kunioea huruma
Hapana mambo ya kijamii harusi,msiba na burudani mbalimbali
hapana kwenye fedha za biashara kubemendwa
HAPANA kubwa kwa marafiki,FURSA ndogo ndogo hapa nahitaji kukubali lawama nyingi msimu huu.
shukrani kocha kwa msimu tunaonza sasa utaleta mapinduzi makubwa kwetu.
LikeLike
Tukae kwenye huu msimu wa HAPANA, tuweze kufanya makubwa zaidi.
LikeLike
Nitasema HAPANA kwa makusanyiko ambayo hayana tija
Nitasema HAPANA kwa vitu ambavyo vinapoteza muda na siyo vyenye manufaa kwenye maisha
Nitasema HAPANA kwa vitu ambavyo havina tija kwenye maisha
Nitasema HAPANA Kwa wanafamilia ambao watanikatisha tamaa kwenye safari ya mafanikio ambao hawajafanikiwa kwa kile ninachofanya
Nitasema HAPANA kutoa hela vidogo vidogo kwenye vitu ambavyo havina msingi
LikeLike
Vizuri sana, simamia HAPANA hizo bila kuyumbishwa.
LikeLike
Hapana kwa Mambo yote yasiyo na tija
LikeLike
Vizuri, simamia hapana yako.
LikeLike
Ninasema HAPANA kwa Matumizi ya pesa yasiyo kwenye bajeti na mikopo isiyo na tija na misaada isiyo na tija.
Ninasema HAPANA kwa tamaa ya mwili ya Kupumzika bila Kukamilisha malengo niliyojiwekea.
Ninasema HAPANA kwa matukio ya kijamii yasiyoendana na malengo yangu makuu
Ninasema HAPANA kwa vitu vinavyopoteza muda badala ya kuukomboa.
Asante
LikeLike
Vizuri sana, simamia hapana hizi kwa msimamo.
LikeLike
Asante Kocha kwa makala hii.
Nitasema hapana kwenye mambo ya kijamii ambayo yatataka kula muda wangu.
Nitasema hapa kwenye kuubembeleza mwili
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Hapana kwa matumizi ya hovyo ya pesa zangu
Hapana kwa tamaa za mwili sex,pombe
Hapana kwa sherehe na mikutano
Hapana kwa marafiki
Hapana kwa Uvivu
Hapana kwa familia
LikeLike
Vizuri, kaa humo.
LikeLike
Nitasema hapana kwa Kufuatilia vita urusi
Nitasema hapana kuahilisha majukumu
Nitasema hapana kwa kukaa bila jukumu
Nitasema hapana kuchelewa kuandika tathimini ya siku
Nitasema hapana kwa famili
LikeLike
Vizuri sana, simamia hapana hizi ili ndiyo ya mchakato iwe na nguvu.
LikeLike
Hapana kwa tamaa za kimwili.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Hapa Kwa fedha ndogo ndogo.
LikeLike
Hapana Kwa fedha ndogo ndogo.
LikeLike
Vizuri sana, maana hizo zina tamaa ya kukunyima fedha nyingi.
LikeLike
Uzuri ni kwamba, ukishapata mafanikio makubwa, kila mtu atakuja kwako, atakusifia na kuona umefanya vyema.
Ila kabla hujayapata mafanikio hayo, kila unachofanya unakosea.
Kubali hilo ili uweze kufika unakotaka kufika.
LikeLike
Huwa kuna usemi kabla hujafanikiwa kila mtu anakuona umechanganyikiwa.
Ila ukishafanikiwa kila mtu anakuona una akili sana.
Tuwe tayari kuvuka hicho kipindi cha kuonekana tumechanganyikiwa ili tufike kipindi cha kuonekana tuna akili nyingi.
LikeLike
Huu msimu ni msimu wangu wa mabadiliko na ni mabadiliko yenye kunipeleka kwenye lengo
1.hapana kwenye shughuli za kijamii hapo nyuma nilikua kiongozi lakini kwa sasa hapana
2.hapana kwa familia mambo ya kulala kukumbatiana alfajiri hapana
3.vikao vya maandalizi ya sherehe na kwenda kwenye sherehe mbalimbali hapana
4.kuangaika na fursa ndogondogo hapana
5.kustarehesha mwili hapana
6.kuchat na marafiki na kupambana na mitandao ya kijamii
Mwisho kabiasa ndiyo kwa kukaa kwenye mchakato hadi kupata uhuu wa kifedha na mafanikio makubwa
LikeLike
Safi sana,
Tukae kwenye mchakato kwa msimamo bila kuyumba.
LikeLike
HAPANA kwenye tamaa za mwili
HAPANA Kwenye kuombwa pesa ndogo ndogo ambazo ningeweza kuweleza kwa kununua hisa
LikeLike
Safi sana, simamia hayo.
LikeLike
Asante sana Kocha kwa kuleta Msimu huu wa WA HAPANA.
Nitasema;
1. Hapana kwa marafiki wasiothamini muda wangu.
2. Hapana kuwapa fedha zangu kwa urahisi wakopaji, wanaojifanya wahitaji.
3. Hapana kwa matukio ya kijamii yanayonipotezea muda wangu.
4. Hapana kuuhurumia mwili wangu pale ninapokuwa sijakamilisha yale ninayopaswa kufanya.
Ndiyo ni moja tu kwenye yale yote yanayochangia kwenye kujenga biashara yangu.
LikeLike
Kaa humu.
LikeLike
Neno hapana litakuweka huru
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Niasema HAPANA kwa
Shughuli za kijamii
Vikao visivyo na tija
Marafiki
Vitu vitamu
LikeLike
Kila la kheri m
LikeLike
MSIMU WA HAPANA ni muhimu sana ktk safari yetu ya Ubilionea. Mara nyingi watu tunaona tabu kutumia sentensi hii kamili “HAPAPA” kwa kuona watu tunao wajibu watajisikia vibaya. Lakini si hahihi kutotumia hii setensi muhimu mno.
Nimejifunza kusema HAPANA kwa
i. Familia
ii. Marafiki
iii. Fedha
iv. Mambo ya kijamii
v. Tamaa za mwili.
LikeLike
Lazima tujue hatuwezi kumfurahisha kila mtu.
Hivyo HAPANA ni muhimu sana itumike.
LikeLike
Asante kocha kwa makala hii bora kabisa. Nitasema hapana kwa yeyote anayenikwamisha nisiyafikie malengo yangu. Baadhi ya watu au tabia ambazo nitasema hapana kwao ni;
Mwili wangu
Mke wangu
Watoto wangu
Ndugu wengine pamoja na marafiki zangu
Uvivu
Ulevi
Uzembe n.k.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike