3051; Kupanda na kushuka.
Rafiki yangu mpendwa,
Safari ya mafanikio huwa ina kupanda na kushuka.
Hizo ni pande mbili za safari hiyo, ambazo huwa hazifanani.
Upande mmoja unahitaji kazi kubwa wakati upande mwingine hauhitaji kazi yoyote.
Kupanda kunahitaji kazi, kunahitaji juhudi kubwa kuwekwa ili kuvuka nguvu kubwa ya mvutano inayofanya vitu vibaki chini.
Kama ilivyo kupaa kwa ndege au chombo chochote cha angani, nguvu kubwa inahitajika kupanda juu.
Kushuka hakuhitaji kazi yoyote, kushuka kunaendana na nguvu kubwa ya mvutano inayofanya vitu vibaki chini.
Chombo ambacho kimetumia nguvu kubwa kupanda angani, kikishindwa na kuanguka, hakihitaji nguvu yoyote ya ndani ili kuanguka.
Bali kuanguka kunafuata nguvu ya mvutano inayotaka vitu vibaki chini.
Haijalishi kitu kipo juu kiasi gani, kama inabidi kiendelee kuwa juu, lazima nguvu iendelee kuwekwa ili kuivuka nguvu ya mvutano inayovuta kitu hicho chini.
Pale tu nguvu ya kupanda inapopungua, ndipo nguvu ya anguko inapofanya kazi ya uharibifu.
Ndiyo maana unaweza kuona mtu ambaye alianza kwa kuweka juhudi kubwa sana na kufanikiwa, anakuja kupata anguko kubwa na baya.
Kupanda kunatumia muda mrefu na kazi kubwa, wakati kuanguka kunatumia muda mfupi na kazi ndogo.
Umeona hapo, kumbe kazi na muda vinahitajika kwenye kupanda.
Lakini havihitajiki kabisa wakati wa kushuka.
Sasa umekuwa unajionea wewe mwenyewe jinsi ambavyo watu wanatafuta njia ya mkato ya mafanikio, yaani njia isiyohitaji kazi na ya haraka.
Tunaona hapo kwa asili kwamba kitu pekee kisichohitaji muda na kazi ni anguko.
Hivyo kama kuna watu wanakuja kwako kukupa njia ya mafanikio ambayo haihitaji kazi wala muda, jua wanakupa njia ya kushindwa.
Ni anguko ndilo lisilohitaji kazi wala muda.
Hiki ni kitu cha kuelewa kwa kina na kujisisitizia sana ili usikaribishe anguko kwenye safari yako ya mafanikio.
Hata baada ya kupanda, nguvu kubwa inahitajika ili kubaki juu ambapo mtu amefika.
Nguvu hiyo inapokosekana, anguko linakuwa kubwa na la haraka.
Mtu anaweza kutumia muda mwingi kujenga jina na sifa yake kwenye maisha, lakini akapoteza jina na sifa hiyo kwa tendo moja la muda mfupi sana.
Utatumia nguvu kubwa kujenga wateja wa biashara yako, mmoja baada ya mwingine, lakini ukifanya kosa moja unawapoteza wengi kwa wakati mmoja.
Kwa kifupi ni kwamba ukijiona umefika hatua ambayo huweki tena nguvu ulizokuwa unaweka awali, jua upo kwenye anguko.
Ni kama samaki aliye kwenye maji, kama hatumii nguvu kwenda kinyume na mkondo wa maji, anakuwa anapelekwa na mkondo huo wa maji.
Kupelekwa na mkondo wa maji hakuhitaji nguvu yoyote ya ndani, kwani hata samaki aliyekufa hupelekwa na mkondo wa maji.
Unapojikuta umeanza kukubaliana na mambo ambayo awali ulikuwa unayakataa, maana yake umeacha kuweka nguvu iliyokuwa inakutofautisha na badala yake unaenda tu na mazoea.
Kuna nguvu kubwa sana inayokuvuta ubaki kwenye mazoea ambayo watu wengi wapo.
Ili uvuke nguvu hiyo na kufanikiwa, ni lazima uweke nguvu nyingine kubwa zaidi.
Kama hakuna nguvu yoyote kubwa unayoweka kuvuka nguvu inayokufanya ubaki chini, huwezi kupanda kwenda juu.
Na kama utaweka nguvu ya kwenda juu lakini ukaiacha baada ya kufika juu, jua kinachofuata ni anguko.
Huwa kuna utani unasema ukiona choo kwenye ndoto usikitumie, huo ni mtego.
Kadhalika ukiona njia rahisi na ya haraka ya kupata mafanikio makubwa kwenye maisha usiitumie, hiyo ni ya kukupeleka kwenye anguko.
Hayo yote unaweza kuwa unayajua, lakini atakuja mtu na kukuambia njia anayokupa ni mpya na ya kweli na hupaswi kuikosa.
Kama vile kupandika kitu chochote kile angani hakutahitaji tena nguvu.
Hakuna ukweli mpya, kanuni za asili zinafanya kazi wakati wote na kwa hali zote.
Ni uchague kuzifuata kanuni za asili kwa kuweka nguvu na muda ili ufanikiwe.
Au uchague kuzivunja kanuni hizo kwa kutafuta njia za mkato zitakazokupeleka kwenye kushindwa.
Chagua kazi na muda wakati wote, malipo yake ni mafanikio makubwa.
Lakini njia za mkato, malipo yake ni kushindwa vibaya.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Chagua kazi na muda wakati wote, malipo yake ni mafanikio.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Hakuna njia ya mkato ni kuweka kazi mara zote
LikeLike
Kweli.
LikeLike
Epuka sana kutafuta mafanikio kwa njia za mkato au rahisi weka kazi na kaa kwenye mchakato kwa msimamo bila kuacha, kufanikiwa kunachukua nguvu kubwa na muda mrefu, lakini kuanguaka ni mara moja.
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Chagua kazi na muda wakati wote = mafanikio
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitaendelea kufanya kazi kwa bidii na maarifa maana najua mafanikio yake ni makubwa,katu na kamwe sitajihusisha na njia za mkato.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kupanda kunahotaji nguvu kubwa lakini anguko halohitaji nguvu yoyoyete ya ndani.
Nakazana kuweka nguvu kubwa kwenye biashara yangu ili niendelee kupanda na nguvu hii ni ya kuweka mara zote kwani nikizembea kidogo anguko linaanza kutokea.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nguvu kubwa inahitajika kwenda juu na kupanda, lakini huhitaji nguvu kushuka.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Katika mafanikio siwezi kukwepa kazi na muda. Nitaweka kazi kubwa na kuwa mvumilivu Kwa muda mrefu Ili kupata mafanikio makubwa.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kazi na muda ni nguvu inayotakiwa kuiweka wakati wote kwenye kazi, kinyume chake ni anguko kubwa litakuja
LikeLike
Kweli.
LikeLike
Kaz Kaz kaz
LikeLike
Kazi zaidi.
LikeLike
Chagua kazi na muda wakati wote, malipo yake ni mafanikio makubwa.
Lakini njia za mkato, malipo yake ni kushindwa vibaya.
Asante
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha,nitajituma na kufanya kazi kwa bidii ili nipate mafanikio hakuna urahisi bila juhudi na kujituma na bila kazi ni anguko kubwa.
LikeLike
Kwenye maisha kuna pande mbili, kupanda na kushuka.
Asante sana.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Hakika
LikeLike
kitu pekee kisichohitaji muda na kazi ni anguko.
Hivyo kama kuna watu wanakuja kwako kukupa njia ya mafanikio ambayo haihitaji kazi wala muda, jua wanakupa njia ya kushindwa.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kumbe kazi na muda vinahitajika kwenye kupanda.
Na hata baada ya kupanda, nguvu kubwa inahitajika ili kubaki juu ambapo mtu amefika.
Nguvu hiyo inapokosekana, anguko linakuwa kubwa na la haraka. ✍️
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
kazi na muda
LikeLike
Viwekezd hivyo.
LikeLike
Hakuna njia ya mkato na ya haraka kwenye mafanikio.
LikeLike
Haitakuja kuwepo.
LikeLike
Nitachagua kazi na muda wakato wote!
LikeLike
Hakuna ukweli mpya,nguvu za asili zinafanya kazi,zikwepe uliwe kichwa.
LikeLike
Nachagua kazi muda wakati wote maana malipo yake ni mafanikio makubwa.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Na kweli unatumia miaka mingi kujenga jina na nguvu na mwisho wake unavunja kwa kuzembea kuweka juhudi anguko ni la siku moja kwa kutoa huduma mbovu
LikeLike
Tuepuke sana huo uzembe unaoweza kutugharimu.
LikeLike
Njia hizo zimenifikisha pabaya sana
LikeLike
Ziepuke kaka ukoma.
LikeLike
Kazi na Muda vinahitajika kwenye kupnda, Na Anguko halihitaji kazi wala muda.
Na hii ndio kanuni ya Asili.
Asante
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante sana kocha kwa makala hii. Nitajitahidi kuweka kazi na muda wakati wote ili niweze kufikia mafanikio makubwa katika maisha yangu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike