3086; Uhakika wa ushindi.
Rafiki yangu mpendwa,
Maisha ni mchezo mkubwa ambapo kila mtu anapambana kupata ushindi ambao ni mafanikio.
Pamoja na kila mtu kuwa kwenye mapambano hayo, ni wachache sana ambao wanapata ushindi mkubwa wanaokuwa wanautaka.
Wengine wengi sana hawaupati ushindi huo, licha ya kukazana sana kuiga yale ambayo wachache wanaoshinda wamekuwa wanayafanya.
Kwenye mchezo wa aina yoyote ile, kushinda au kushindwa huwa hakuanzii uwanjani, bali kunaanzia kwenye mtazamo wa mchezaji mwenyewe.
Mambo ambayo watu wanafanya kwa nje yanatofautiana sana, lakini wote wanaopata ushindi, huwa na mtazamo ambao unaendana.
Kama unataka kuwa na uhakika wa ushindi kwenye safari yako ya maisha, kuna mambo makubwa matatu unayopaswa kuyajenga kwenye mtazamo wako.
Moja ni kuchukua hatua kubwa sana.
Hakuna ushindi unaopatikana bila kuchukua hatua ambazo ni kubwa.
Unatakiwa kuchukua hatua kubwa sana kwenye kila unachotanya kwenye maisha yako ili kuzalisha matokeo makubwa na ya tofauti.
Kila wakati unapaswa kufanya tofauti na ulivyozoea kufanya, ili uweze kupata matokeo ya tofauti pia.
Mara zote kaa kwenye upande wa kuchukua hatua kubwa.
Mbili ni kuendelea kusonga mbele bila ya kujali mambo unayokabiliana nayo.
Kuchukua hatua kubwa haimaanishi kwamba mambo yatakuwa rahisi kwako.
Mambo yatakuwa magumu, utakutana na kila aina ya changamoto na vikwazo mbalimbali.
Ili kupata ushindi wa uhakika, unapaswa kuendelea mbele bila ya kukwamishwa na chochote.
Wewe unapaswa kuwa na mwendo wa aina moja tu, ambao ni kusonga mbele bila ya kujali umekutana na nini.
Ni ung’ang’anizi huu wa kusonga mbele ndiyo unaokupa ushindi wa uhakika.
Tatu ni kutokujali kuhusu maumivu, kushindwa, kukataliwa, kupoteza, kudharauliwa na kukatishwa tamaa. Unajua nini, hayo ni mambo ambayo lazima utakutana nayo kwenye safari yako ya maisha. Lazima uyapokee na kuendelea na mashindano bila kukwama. Ukijali tu kuhusu mambo hayo, ukianza kuona wewe hustahili kukutana nayo, hapo ndipo unapokuwa umekaribisha kushindwa.
Unapaswa kuendelea na safari yako kama vile mambo hayo hayajakutokea, licha ya kwamba kila wakati yatakuwa yanakutokea.
Ukiweza kuyapuuza hayo, ushindi kwako ni swala la muda tu.
Hutapata ushindi mkubwa kwenye maisha yako kwa kuangalia yale ambayo wanaoshinda wanayafanya.
Unayoona kwa nje hayana nguvu kubwa kama yale yaliyo ndani ya fikra za watu.
Jenga mambo haya matatu uliyojifunza kwenye fikra zako na ushindi utakuwa ni wa uhakika kwako.
Mara zote chukua hatua ambazo ni kubwa sana kuliko ulivyozoea.
Endelea kusonga mbele kwa kasi kubwa bila ya kujali mambo unayokabiliana nayo.
Na futa kabisa yasiyoendana na ushindi unaotaka, unachotaka wewe ni ushindi tu, mengine yote unayapuuza.
Ukiweza kukamilisha hayo, ushindi unakuwa wa uhakika kwako bila ya kujali ni vitu gani unavyofanya kwa nje.
Kaa kwenye njia hii ili upate ushindi wa uhakika kwenye maisha yako.
Itangazie dunia nzima ielewe kwamba upo kwenye haya maisha kwa ajili ya kitu kimoja pekee, ambacho ni ushindi.
Akili yako haipaswi kuwa na msamiati mwingine isipokuwa ushindi pekee.
Unashinda kwa uhakika pale unapokataa kupokea chochote kisichokuwa ushindi.
Anzia hapo na kwa hakika utashinda.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Unashinda kwa uhakika pale unapokataa kupokea kitu chochote kisichokuwa ushindi.
LikeLike
Kataa kata kata.
LikeLike
Hatua kubwa
Songa mbele
Futa kabisa yasiyohusu ushindi
LikeLike
Tukae humo
LikeLike
Nitachukua hatua kubwa sana kuelekea ushindi kila siku
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kitu kikubwa ni ushindi,kuacha vyote na kupambana na kitu kitakachoniletea ushindi.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nipo hapa kwa kitu kimoja tu, Ushindi!
LikeLike
Ieleweke wazi kabisa.
LikeLike
Asante sana kocha,sifikirii chochote zaidi ya ushindi,siangalii napitia nini sasa,mimi ni mshindi tu.
LikeLike
Ushindi ni lazima.
LikeLike
Itangazie dunia ielewe kwamba upo hapa kwaajili ya kitu kimoja tu
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kwenye mchezo wa aina yoyote ile, kushinda au kushindwa huwa hakuanzii uwanjani, bali kunaanzia kwenye mtazamo wa mchezaji mwenyewe.
Asante sana
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Maisha ni mchezo mkubwa ambao kila mtu anapambana kupata ushindi ambao ni Mafanikio
Kwenye mapambano haya akili yangu haipaswi kuwa na msamiati mwingine isipokuwa ushindi pekee.
LikeLike
Futa kabisa misamiati ambayo siyo ushindi.
LikeLike
Nipo duniani kwa,ajili ya jambo moja tu ambalo ni ushindi
LikeLike
Shida.
LikeLike
Asante Kocha,
Ili kufanikiwa nitachukua hatua kubwa kabisa, nitasonga mbele na nitafuta yote yasiyohusu ushindi.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Nachukua hatua kubwa na kuendelea kusonga mbele na kuupambania ushindi mara zote bila kujali magumu yaliyopo kwenye safari ya mafanikio
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Naitangazia dunia kuwa kwenye haya maisha nipo kwa kupambania ushindi tu na si vinginevyo.
LikeLike
Ieleweke wazi kabisa.
LikeLike
Itangazie dunia nzima ielewe kwamba upo kwenye haya maisha kwa ajili ya kitu kimoja pekee, ambacho ni ushindi.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Tangazo liwe la kishujaa.
LikeLike
Nipo Duniani kwa ajili ya kushinda.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Mara zote chukua hatua ambazo ni kubwa sana kuliko ulivyozoea.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Mtazamo chanya na kuchukua hatua ni kila kitu katika kupata ushindi. Asante sana kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Nimeipenda hii ya kuwa hakuna rivas ni mbele tu hadi kupata ushindi
LikeLike
Kabisa.
LikeLike