3128; Kazi na muda.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna vitu ambavyo huwa havijali kabisa kuhusu wewe na unafanya nini.
Vitu hivyo huwa vinataka mtu kuvichukulia hatua mara moja kama anataka kunufaika navyo.
Na kama mtu hatakuwa tayari kuchukua hatua kwenye vitu hivyo, haviwezi kumsubiri, bali vinasonga mbele.
Vitu vyenye sifa hizo ni vingi, lakini hapa tunakwenda kuangalia viwili ambavyo vina nguvu kubwa sana kwako. Viwili hivyo ni kazi na muda.
Kazi ndiye rafiki wa kweli.
Ni kupitia kazi ndiyo tunapata fursa ya kupata chochote tunachotaka.
Kazi huwa haijali kama unaipenda au unataka kuifanya.
Kazi inataka kufanyika.
Bila juhudi kuwekwa, hakuna matokeo yanayopatikana.
Unaweza kuikwepa kazi kadiri utakavyotaka wewe mwenyewe, lakini jua kwa uhakika hiyo kazi hakuna mahali inakwenda, inakusubiri uweze kuifanya.
Wakati wa ujana, watu wengi sana huhangaika na njia za mkato za kupata kile wanachotaka bila ya kuweka kazi.
Wanahangaika sana na njia hizo, lakini mwisho wa siku wanarudi kwenye msingi wa kuweka kazi ndiyo wafanikiwe.
Kazi haijali sana unataka au hutaki nini, yenyewe inataka ifanyike.
Kama haitafanyika, haitaondoka, itaendelea kusubiri mpaka mtu aamue kweli kuifanya.
Muda ndiyo sarafu tunayopima nayo maisha yetu.
Kadiri muda unavyokwenda, ndivyo tunavyopunguza muda wetu wa kuishi hapa duniani.
Muda huwa unaendelea kwenda bila ya kujali. Pale unapoona unapaswa kusubiri kwa sababu huna maandalizi ya kutosha, muda unaendelea kwenda.
Muda utaendelea kwenda bila ya kujali ni nini wewe unafanya au unashindwa kufanya.
Dunia haitasimama kukusubiri wewe mpaka uwe tayari, itaendelea kwenda kwa kasi yake yenyewe.
Kuchwa na kuchea, kila siku, ndiyo mwendo wa dunia.
Kadiri unavyoelewa mapema umuhimu wa muda na kufanyia kazi, ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi nzuri ya kupata kile unachotaka.
Muda utaendelea kwenda, utake au usitake, muda unakwenda.
Kazi inahitajika kufanywa, upende au usipende.
Yazingatie sana hayo mawili ili uweze kuyatumia vizuri kwenye kupata kile unachotaka.
Weka kazi na muda kwa msimamo mkali, na utaweza kujipa uhakika wa kupata chochote unachotaka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante kocha,Nitaendelea kuthamini Kazi na muda wangu, Kwa kufanya yale yenye tija.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kuweka kazi na muda kwa msimamo mkali, utaweza kujipa uhakika wa kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Weka kazi na muda kwa msimamo mkali na utaweza kupata chochote unachotaka.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha nitaendelea kuithamini kazi na muda usemi sahihi ni muda ni tiba kwa kweli hili nimekuwa nalipitia katika maisha yangu mfano nataka nunua kitu chenye gharama kubwa nafanya Hesabu najikuta sikimudu naachana nacho lakini baada ya muda naona mutu anakuja na hicho kitu na anakiniuzia kwa bei nzuri kwa hiyo nikweli muda ni tiba
LikeLike
Umesema vyema kabisa.
LikeLike
Muda unaendelea kwenda utake usitake anza hivyohivyo bila kusubiri hata kama haujakamilika utaboresha mbele na pia usijubiri nenda wakukutembele mrekebishane mbele
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante kocha,Nitajitahidi kuweka kazi mbele na mda ili niweze kupata kusudi langu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kazi ni rafiki wa kweli tuweke kazi ili tupate tunavyovitaka
Asante sana
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Naweka kazi na muda kwa msimamo ili niweze kupata matokeo ninayotaka kwenye maisha yangu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Hakika Kocha,kazi na muda havimsubiri mtu. Asante sana.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kazi haijali sana kama unataka au hutaki. Yenyewe itaka ifanyike
LikeLike
Hakuna namna
LikeLike
Kazi lazima ifanyike hakuna mkato
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nitaweka kazi na muda katika kile ninachofanya ili kujiletea maendeleo.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Muda huwa unaendelea kwenda bila ya kujali.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Muda, Kazi, nitaendelea kufanya kazi kwa kuzingatia muda sahihi,
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Wakati wa ujana, watu wengi sana huhangaika na njia za mkato za kupata kile wanachotaka bila ya kuweka kazi.
Wanahangaika sana na njia hizo, lakini mwisho wa siku wanarudi kwenye msingi wa kuweka kazi ndiyo wafanikiwe.
Kazi haijali sana unataka au hutaki nini, yenyewe inataka ifanyike.
Kama haitafanyika, haitaondoka, itaendelea kusubiri mpaka mtu aamue kweli kuifanya.
LikeLike
Kazi haikwepeki.
LikeLike
Nahakikisha naweka kazi na muda wa kutosha na hatimaye nitapata kile ninachopigania asante Kocha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Naweka juhudi kubwa katika kazi, Kwa msimamo na nikithamini Muda…nitapata chochote ninachokitaka
LikeLike
Hakika
LikeLike
RAFIKI WA KWELI NI KAZI
LikeLike
Ndiyo
LikeLike