3141; Kwa nini hufanyi?
Rafiki yangu mpendwa,
Unajua unachotaka kwenye maisha yako, wapi unapotaka kufika.
Pia unajua nini unapaswa kufanya ili uweze kupata unachotaka.
Lakini sasa, kwa nini hufanyi yale unayopaswa kufanya ili kupata unachotaka kupata?
Na hata pale inapotokea unaanza kufanya, kwa nini huna mwendelezo?
Kwa nini unaanza kufanya na kuishia njiani?
Nini kinakukosesha msimamo kwenye ufanyaji?
Unapanga kabisa mpaka muda wa kufanya yale unayopaswa kufanya.
Lakini muda huo unapofika, unaahirisha kufanya.
Kwa nini inakuwa hivyo?
Miaka kumi iliyopita, ungeanza kufanya na ukafanya kwa msimamo bila kuacha, leo hii ungekuwa mbali zaidi ya hapo ulipo sasa.
Nini kimekukwamisha kufanya hivyo?
Una miaka mingine kumi mbele yako, ambayo usipokuwa na tahadhari, nayo utaipoteza kama ulivyopoteza hiyo iliyopita.
Umewahi kujiuliza kwa nini unapumua kila mara bila kuacha hata kama umetingwa kiasi gani?
Huwa huachi kabisa kula chakula hata kama kila kitu hakipo sawa.
Lakini inapokuja kwenye kufanya yale unayopaswa kufanya ili kupata unachotaka, huwa unaruhusu sababu mbalimbali zikuzuie.
Kwa nini unaruhusu hayo?
Rafiki, kwa nini hufanyi yale unayopaswa kufanya ili kupata unachotaka kwa namna unavyopaswa kufanya?
Weka maoni yako hapo chini ya swali hilo, kwa uhalisia kabisa kutoka ndani ya moyo wako.
Kutokana na majibu yako, weka mkakati wako wa ufanyaji bila kuruhusu kukwamishwa na chochote kile.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nikijichunguza kwa mengi ambayo napaswa kufanya na kisha sifanyi ni kutokana na uvivu na uzembe.Kwa mfano wa kupumua na kula naona kabisa nina wajibu wa kujisukuma kufanya yale muhimu bila kuacha ili miaka 10 ijayo nifurahie mafanikio na si kujutia.
LikeLike
Amua kufanya na ufanye kweli.
LikeLike
Nitaacha uzembe na kufanya yote ninayopanga kufanya.
Kufanya ndiyo njia sahihi ya kunifikisha kwenye malengo niliyojiwekea.
LikeLike
Vizuri, timiza hili la kufanya.
LikeLike
Kwa nini hufanyi, Namshkr sana tangu kuingia kisima cha maarifa,kupata mafunzo ya kutosha na Elimu nzuri ya Falsafa ya ustoa swali hilo hapo juu limepungua, nitajitahidi kutekeleza na kutimiza,kwa kifupi ninachopenda nafanya.Asante kocha
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kwa nini hufanyi?
Kwenye kufanya wengi huwa wanatoa sababu nzuri kama vile uvivu, uzembe na ujinga na siyo sababu za kweli.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Sifanyi kwa msimamo kwa sababu ya Uzembe wangu. Nitajitahidi kujisukuma na kuondoa hali ya uzembe ili nifanye kwa msimamo bila Kuacha.
LikeLike
Vizuri kwa kutambua hilo, chukua hatua.
LikeLike
Asante kocha,Kwa nini hufanyi? Kutofanya au kutokaa kwenye mchakato ni maamuzi ya uzembe tu.hivyo nitajitahidi kwa kufanya kila siku bila kuacha ndo mkakati mkubwa.
LikeLike
Vizuri, chukua hatua.
LikeLike
Nitajitahidi kufanya mambo yote muhimu kwa msimamo bila kuacha kama ninavyopumua na kula kila siku. Asante Kocha
LikeLike
Vizuri sana, tekeleza.
LikeLike
Ahsante kocha, hapo ni uvivu, uzembe na kuhofia watu wengine watanionaje lakini sasa nitajitahidi kufanya kwa muendelezo
LikeLike
Vizuri, kila la kheri.
LikeLike
Kwa nini hufanyi? Sina sababu ya msingi zaidi ya uvivu na uzembe na kutokuhusianisha dhana hii ya kufanya na kupumua na kula. Kwa sababu ikitokea jambo lolote linaloleta kikwazo kwenye kupumua na kula nitafanya kila namna kuondoa hicho kikwazo ili nisife. Na kwenye hili la kufanya nitajitahidi kuondoa vikwazo vyote vinavyonizuia nisifanye ili nisife. Asante
LikeLike
Vizuri sana, tekeleza hivyo.
LikeLike
Kutofanya ni kwa sababu ya usembe na kuwa na vipaumbele visivyo sahihi.
LikeLike
Hapo kwenye vipaumbele panapoteza wengi sana.
LikeLike
Kwa hakika ni uvivu na uzembe lakini nitajitahidi kufanya ninachotakiwa kufanya ili nipate ninachokihitaji. Ninachokihitaji kinahitaji mchato wa muda mrefu na kufanya matendo kwa msimamo
LikeLike
Vizuri, tekeleza hivyo.
LikeLike
Uzembe,na kuwa na mambo mengi kwa wakati mmoja(kukosa focus).
Kuacha uzembe
Kuacha mambo mengi ambayo hayanifikishi kwenye malengo na kuwa na to do list ya mambo nayotakiwa.
LikeLike
Vizuri, tekeleza hilo.
LikeLike
Ahsante na hongera sana kocha kwa uabdishi wa makala hii.
Changamoto ni nyingi sana njiani, Kuna mambo mengi huwa yananikuta mpaka najikuta kupoteza kabisa mwelekeo lakini kwakuwa nakumbushwa hivi, Sasa nipo tayari kuendelea na mapambano kama nilivyopanga.
Mkakati wangu ni kuwa, nitafanya kazi kwa nguvu sana kuanzia Sasa na kuondoa mazoea yote.
Ahsante sana
LikeLike
Usiahidi tu, bali tekeleza pia.
LikeLike
Uvivu, uzembe na kuchukulia mambo kawaida ni vitu vinavyochangia kushindwa kufanya kwa msimamo. Nitaviepuka vitu hivi ili niweze kufanya kwa msimamo yale yaliyo muhimu kwangu na kupata matokeo ninayotaka.
Asante sana Kocha
LikeLike
Vizuri, tekeleza.
LikeLike
Sifanyi Yale ninayopaswa kufanya ni kwa sababu ya
Uzembe. Ninaahidi kuachana na uzembe , nitajitahidi
Kila wakati kunikumbusha Hilo kwamba uzembe ni adui na moja. Hivyo ni kupambana nao kwa nguvu zote.
Asante kocha
LikeLike
Vizuri, tekeleza.
LikeLike
Kufanya Yale ya muhimu na Kwa msimamo Kwa muda mrefu ndio uhakika wa kutoa hapo ulipo kupitia kanuni hiyo nitafanya kila lilnalotakiwa kufanywa kwenye maisha yangu ili kuleta mafanikio makubwa
Asante
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Uvivu na uzembe, hakuna kingine..
Hasa hasa kwenye kuanza kufanya lakini nikishaanza uvivu na uzembe huwa unaondoka hadi nihakikishe nimemaliza na nimefanya kwa ubora.
LikeLike
Vizuri sana.
Endelea na mbinu hiyo ya kuanza.
LikeLike
Kudhani sijawa tayari kuanza ndiyo sababu kubwa na kingine kudhani fedha kiasi flani ndiyo itafanya nianze. Kifupi natakiwa KUJITAFUTA Kwa kuanza kufanya.
LikeLike
Huhitaji kujitafuta zaidi ya pale ulipo sasa, unachohitaji ni kuanza kufanya.
LikeLike
Kitu kimoja wapo kutokujali na kushindwa kujali wengine pia nakwenda kufanya bila kuacha na ntapunguza uzembe wa kutokuweka jitihada kubwa zaidi..
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kwanini hufanyi yale unayopaswa kufanya ili kupata unachotaka kupata.
LikeLike
Eti.
LikeLike
Kwa vitu ambavyo nimepanga kufanya,hakika huwa najitoa kweli kufanya,na ukiona sijafanya ujue niko kwenye mkakati wa kukifanya,kinachonisukuma kuwa hivi ni kuogopa kuja kujuta baadae,kuwa ninge……
LikeLike
Majuto huwa yanaumiza sana.
LikeLike
Sifanyi ninayopaswa kufanya ili kupata ninachotaka kupata ,Sababu ni uzembe tu.
Mkakati wangu sitafanya kingine chochote kabla ya kufanya kile ninachotakiwa kufanya.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ni kweli kocha, Huwa nakuwa na mipango mingi ila utekelezaji Huwa naishia njiani. Ila zamu hii Kwa kuanza na hii Semina. Ngoja nikomae nipate watu 500. Ninaenda kufanya yote nilioahidi Kwa msimamo Bila kuacha.
Kupiga simu
Matangazo ya Facebook
Kutuma sms 1000 Kila siku Whatsap
Email
Nitafanya hivyo Kwa msimamo Kila siku
LikeLike
Safi sana, jipime kwenye hilo kwenye huu mchakato wa siku 100, kamilisha yote bila kuacha.
LikeLike
Sina sababu ya msingi zaidi ya uzembe mkubwa kwasasa nimejikana nafsi nimeachana na uzembe nimekuwa nimtu wakuchukua hatua
LikeLike
Achana na huo uzembe.
LikeLike
Kweli najua ninachokitaka pia na kinachohitajika kufanyika ilikupata ninachokihitaji ila mwendeleo kufanya kilasiku bila kuacha ni changamoto
Mkakati ninaokwenda kufanyia kazi ni kufanya lile linalo hitajika kufanyika bila kujari nipo kwenye hari gani
LikeLike
Vizuri, tekeleza.
LikeLike