Mpendwa mstoa mwenzangu,
Mchezo mzima wa maisha yetu huwa unaanzia kwenye akili. Akili yetu inatupa kile ambacho kimetawala mara nyingi kwenye akili yetu.
Ukiwa na hisia za kushindwa utapata matokeo ya kushindwa. Ukiwa na hisia za kupata zaidi utashangaa na akili yako inakuletea matokeo ya ushindi kwako.
Ukiwa na hisia na kuona kwamba watu wanakudharau, watu wanakusema, kila ukiwaona watu hata wanazungumza mambo yao, utajihisi kama vile wanakusema wewe.
Tunatengeneza maumivu kwenye maisha yetu, kisha maumivu yanatuumiza. Kama mtu akikutukana na ukikataa hutoumia ila ukikubali ndiyo itakutesa.
Aliyekuwa mtawala wa Roma na Mwanafalsafa wa Ustoa Marcus Aurelius aliwahi kunukuliwa akisema,
Kataa hisia za maumivu na maumivu yenyewe yataondoka.
Nukuu;
“Reject your sense of injury and the injury itself disappears.
Kwa mfano, mtu akikutukana na ukimchukulia ni mchina humwelewi akiongea, huwezi kuumia na hata maumivu ya kuchukuliwa umetukanwa yataondoka yenyewe.
Huwa tunasikia maumivu au majeraha mengi kwenye maisha yetu kwa kuyapa umakini majeraha hayo kwenye akili. Lakini ukikataa, hisia za kuumizwa, na maumivu yenyewe yataondoka.
Marcus Aurelius anatuambia kuwa, kila kitu tunachosikia ni maoni, na siyo ukweli. Kitu chochote tunachoona ni mitazamo na siyo kweli.
Nukuu;
“Everything we hear is an opinion, not a fact. Everything we see is a perspective, not the truth.”
Miili yetu huwa inatudanganya sana pale tunapohisi tumechoka, na kama tukikataa kiakili huwa yale maumivu ya kuchoka au hali ya kukataa kuendelea huwa inaondoka yenyewe.
Mtu mmoja asiyejulikana aliwahi kunukuliwa akisema ,fimbo na mawe vinaweza kuvunja mifupa yangu, lakini maneno kamwe hayawezi kuniumiza.
Nukuu; “Sticks and stones may break my bones, but words can never hurt me.”
Kuumizwa kwa maneno ni kuchagua wewe mwenyewe. Ukikataa hakuna kitakachoweza kukuumiza.
Mwandishi wa kitabu cha You can’t hurt me, David Goggin anasema kwamba, kuumia ni kuchagua.
Kwenye maisha hakuna kuumia ni wewe mwenyewe unapokuwa unatafsiri kile kilichotokea. Kwa mfano, unaweza kuona mchakato wa BILIONEA MAFUNZONI ni mgumu lakini siyo mgumu kama ukichagua kukaa kwenye mchakato.Kaman ni kitu ambacho unakipenda na kinatokea ndani ya moyo wako utapuuza maumivu na maumivu yataondoka.
Tunapaswa kufunika maumivu mengi tunayokutana nayo kwa kupuuza yale maumivu. Kwa mfano, aliyekuwa mcheza kikapu Kobe Bryant aliwahi kunukuliwa akisema,
“Maumivu huwa hayakwambii wakati unapaswa kuacha.
Maumivu ni sauti ndogo kichwani inayojaribu kukuzuia kwa sababu inajua ukiendelea utabadilika.”
Nukuu;
Pain doesn’t tell you when you ought to stop. Pain is the little voice in your head that tries to hold you back because it knows if you continue you will change.
Naye aliyekuwa mwanariadha wa Tanzania aliyeweza kushiriki mashindano ya riadha huko Mexico, wakati wa mashindano alipata jereha kwenye mguu wake kitu ambacho kilimfanya ashindwe kuendelea na mbio.
Licha ya kuumia alikubali kuendelea na mbio. Wakati ulimwengu mzima ukimshangaa kwa kitendo cha cha kutokukata tamaa au kuruhusu maumivu ya kuendelea na mbio huku wenzake wote wakiwa wamemaliza zaidi ya saa moja zaidi.
Na alipoulizwa na waandishi wa habari alijibu, nchi yangu haikunituma Mexico kuanza mbio bali kumaliza mbio.
Hapa tunajifunza nini?
Tukatae aina ya maumivu ambayo tunakuwa tunayapata pale tunapokuwa kwenye mchakato wa kitu fulani. Ushindi ni kumaliza kile ulichoanza na siyo kuishia njiani.
Kujisukuma zaidi ndiyo njia pekee ya kufikia uwezo mkubwa uliopo ndani yako na kukomaza akili na mwili wako. Hata kama umechoka, unahisi maumivu, jisukume zaidi kumbuka, kuumia ni kuchagua na kama unajua una kitu kizuri unapata hata maumivu yanatoka yenyewe.
Na hii ndiyo dhana ya kifalsafa unapaswa kuwa nayo ya kupuuza maumivu na kuweka kazi mpaka umalize kile ulichopanga kufanya.
Usiache kufanya pale unapokuwa umechoka, bali nenda zaidi ya ulivyozoea kwenda. Kumbuka hii ni vita yako dhidi yako mwenyewe, hivyo lazima ujisukume zaidi ya ulivyozoea ili kuweza kushinda vita hii.
Unashindana na wewe wenyewe na vita ya maumivu mbalimbali ni kubwa, na yote yanakuja ili kukuzuia usiendelee na mchakato.
Yajayo yanafurahisha, usichoke safari malizia mchakato wa BILIONEA MAFUNZONI ulioanza. Hauko hapa kuanza kuangalia mafunzo bali kushiriki mafunzo na kukaa kwenye mchakato mpaka mwisho.
Rafiki na Mstoa mwenzako,
Mwl Deogratius Kessy
Shukrani mwl deo.
Kumalizia ulichokianza na sio kukimbia unapokutana maumivu.
LikeLike
Vizuri Christopher Mwijage. Kila la heri
LikeLike
Asante sana mwl Deo, hakika, kuanzia sasa nakataa hisia za maumivu, naimani yataondoka yenyewe, naendelea kukataa kushindwa kwani Mimi ni mshindi na nimezaliwa kushinda.
LikeLike
Vizuri sana Mr Beatus Elias Rwitana. Kila la heri
LikeLike
Asante Mwl. Del,
Ninakataa hisia za maumivu hata pale ushindi unapokawia au kushindikana.
LikeLike
Vizuri sana Mr Godfrey Mbise. Kila la heri
LikeLike
Kweli tusiichoke safari ambayo tumeshaona wazi kwamba inatupeleka kule tunakoazimia kufika.
LikeLike
Kweli maumivu yana laghai, na nikivuka maumivu kidogo tuu nabadilika,
Asante sana mstoa tupo pamoja Mpaka mwisho katika mchakato huu wa maisha wa billionea mafunzoni.
LikeLike
Asante Sana
Tubadilishe mtazamo tu na amani itapatikana. Màumivu ni kuiruhusu akili iyape Kibali hisia hasi zikuumize
LikeLike
Asante,kikubwa ni kila siku kuiona ni mpya na kuweza kukaa kwenye mchakato bila kukata tamaa,safari ni ndefu lakini mwendo nimpaka mwisho.
LikeLike