3178; Sijali, Naweka Kazi.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye michezo, hasa mpira wa miguu, mashindano ambayo yanafanyika kwa njia ya ligi, timu inaweza kuwa imeshashinda kwa pointi ambazo imejikusanyia kabla hata ya ligi kuisha.
Lakini lazima timu hiyo ikamilishe michezo yote iliyobaki kwenye mzunguko wa ligi.
Ushindi unaweza kuwa umeshapatikana kabisa, lakini lazima muda usubiriwe, wa michezo yote kukamilika.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye ushindi wa maisha ya mafanikio.
Ushindi wa mafanikio siyo wa kusubiri mpaka kufikia kilele.
Bali ni ushindi unaopatikana kwa maamuzi ambayo mtu unafanya kisha kusubiri muda ili ushindi huo ujidhihirishe.
Yaani safari ya mafanikio ni sawa na ligi ambayo unaanza kwa kupewa ushindi, halafu kazi yako kuu inakuwa kulinda ushindi huo usipotee.
Hivyo unalazimika kuweka juhudi kubwa mara zote ili kulinda usipoteze.
Ni sawa na kuogelea, ukisimama unazama.
Hivyo lazima uendelee kupiga mbizi, iwe unataka au hutaki, unajisikia au hujisikii.
Ili usipoteze ushindi ambayo unakuwa umeanza nao, unapaswa kwenda na mtazamo wa; SIJALI, NAWEKA KAZI.
Umeshajua nini unataka na umeshajua unapaswa kufanya nini ili kukipata.
Hivyo kinachobaki ni wewe kuweka kazi ili ukipate.
Ukishaweza kufikia hatua ya hujali bali unaweka kazi, ushindi ni uhakika kwako.
Unajisikia kuchoka sana? Usijali, weka kazi.
Watu hawakuelewi? Usijali, weka kazi.
Unakutana na magumu na changamoto? Usijali, weka kazi.
Matokeo yanachelewa? Usijali, weka kazi.
Ukiweza kufikia ngazi hii ambayo kuweka kwako kazi hakuathiriwi na chochote kile, ushindi ni wa uhakika kwako.
Hata kama unaanzia chini kabisa na huna chochote.
Ndiyo maana nakuambia umeshashinda, unachosubiri ni muda tu upewe kombe.
Lakini pia muda huo hauna mwisho.
Maana zoezi la kutojali na kuweka kazi ni endelevu.
Ukiacha tu, umepoteza kila kitu.
Siku Elon Musk anatangazwa na jarida la Forbes kama mtu tajiri zaidi duniani, hakuwa na mengi ya kusema.
Kupitia mtandao wa twitter (sasa X) aliandika; “How strange. Well, back to work…”
Akimaanisha; “Inashangaza. Sawa, narudi kazini.”
Kwa watu wa kawaida kufikia nafasi hiyo ingekuwa ndiyo ushindi mkubwa kwao na hata kuacha kujitesa.
Lakini kwa Elon, ushindi ulishaanza kabla ya hayo matokeo.
Na ushindi huo unaendelea baada ya hayo matokeo.
Ni ushindi wa SIJALI, NAWEKA KAZI.
Ni watu wachache sana wanaoweza kwenda vizuri na dhana ya SIJALI, NAWEKA KAZI.
Inamtaka mtu kujitoa kweli kweli kupata kile anachotaka.
Ndiyo kinachowatofautisha wanaopata ushindi mkubwa na wanaobaki kawaida.
Dunia haitakuangusha kamwe kama utakuwa tayari kuweka kazi mara zote.
Hakuna kazi inayopotea bure bila kulipwa.
Na kikubwa sana wanachokosa watu kwenye kazi ni msimamo na subira.
Maana kila mtu anaweza kuweka juhudi kubwa.
Ila wanaoshinda ni wale wanaoweza kuweka juhudi hizo kwa muda mrefu bila kuacha, hata wakutane na nini.
Wakipoteza wanaendelea kuweka juhudi.
Na hata wakishinda wanaendelea na juhudi.
Wasiofanikiwa huwa wanayumbishwa sana na matokeo wanayopata.
Wakipata matokeo mabaya wanaona hawawezi tena, hivyo wanakata tamaa na kuacha kuendelea kuweka kazi.
Na hata wakipata matokeo mazuri, wanayasherekea sana na kujiona wameshamaliza, hawahitaji tena kuweka kazi.
Na hivyo ndivyo wanavyoshindwa vibaya sana.
Sisi ushindi wetu ni wa uhakika kwa sababu tumechagua kuendelea kuweka kazi bila kuacha, haijalishi ni matokeo ya aina gani tumepata.
Tukipata matokeo mabaya, tunaendelea kuweka kazi.
Na hata tukipata matokeo mazuri, tunaendelea kuweka kazi.
HATUJALI, TUNAWEKA KAZI na ndiyo maana tunao uhakika wa ushindi.
Kwenye hii safari, kushindwa ni pale unapoacha kufanya.
Hivyo ni mwiko kwetu kuacha kuweka kazi, hata iweje.
Tunajua muda utatupa chochote tunachotaka, kama tutaendelea kuweka kazi.
HATUJALI, TUNAWEKA KAZI huku tukiwa na subira isiyochoka.
Ushindi tunao, hatutakubali kuupoteza kwa namna yoyote ile.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Sijali naweka kazi.
LikeLike
Safi.
LikeLike
Sijali naweka kazi. Ushindi ninao siwezi kukubali kuupoteza.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Unajisikia kuchoka sana? Usijali, weka kazi.
Watu hawakuelewi? Usijali, weka kazi.
Unakutana na magumu na changamoto? Usijali, weka kazi.
Matokeo yanachelewa? Usijali, weka kazi.
Tuko pamoja Kocha.
LikeLike
Kazi iwekwe.
LikeLike
Ukipata shida weka kazi
Ukidharauliwa wewe weka kazi
Hawakuelewi wewe weka kazi
Jitengenezee ushindi hata kabla ya kumaliza mbio na ukishashinda ndiyo mwanzo aa kuwka kazi
Wengi wetu wakifanijiwa wanabweteka aakati unatakiwa uendelee kuweka kazi tena natena
LikeLike
Kazi haina mwisho.
LikeLike
Nitaweka kazi kwa wakati wote bila kuchoka Asante sana kocha
LikeLike
Kazi kazi
LikeLike
Sijali na weka kazi. Iwe unaona matokeo au huoni, usijali wewe weka kazi..
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Kazi ni kazi.
LikeLike
Msimamo na subira kwenye kazi zangu ni msingi wa kupata ninachotaka. Asante.
LikeLike
Kazi haiwezi kukutupa.
LikeLike
Ahsante sana, sitajali matokeo gani napata nitaweka kazi najua muda utanipa kwa matokeo kwa muda unaostahili.
LikeLike
Kazi ni matokeo ya uhakika.
LikeLike
Sijali naweka kazi.
Matokeo ya ushindi yanakuja kutokana na kazi ninayoiweka.
LikeLike
Kazi ni ushindi.
LikeLike
Ushindi tunao hatukubali kupoteza kwa muda wowote ule.
LikeLike
Kazi inadumisha ushindi.
LikeLike
Asante sana kocha,binafs,sijali naweka kazi mbele, ushindi kwangu ni lazima.
LikeLike
Kazi ni ushindi wa uhakika.
LikeLike
Sijali, Naweka kazi tu bila kuacha
LikeLike
Kazi ndiye rafiki wa kweli.
LikeLike
Ushindi tunao hatukubali kupoteza
Hatujali,tunaweka kazi
Asante sana
LikeLike
Kazi lazima iwekwe.
LikeLike
Sijali,naweka kazi
Ushindi tunao tuwe na subira
Shukrani kocha.
LikeLike
Weka kazi sana.
LikeLike
Ni kazi tu bila kujali matokeo
LikeLike
Kazi haijali, lazima iwekwe.
LikeLike
SIJALI, NAWEKA KAZI!
LikeLike
Ni muhimu kuweka kazi.
LikeLike
Sijali naweka kazi ni swala la muda tuu mafanikio kwangu ni lazima
LikeLike
Vizuri, weka kazi.
LikeLike
Asante kocha,wajibu wangu ni kutojali na kuweka kazi mbele ili nifanikiwe.
LikeLike
Kazi lazima iwekwe.
LikeLike
Naweka kazi ushindi ni swala la muda tu!
LikeLike
Kazi inaleta ushindi wa uhakika.
LikeLike
Sijali naweka Kazi.
Nabakia kwenye mchakato naweka Kazi tu. Mie sio mtu wa tukio Wala kungoja matokeo Ila naweka kazi kubwa, Thamani kubwa na maarifa kutoa kilicho bora
LikeLike
Weka kazi, hakuna namna nyingine.
LikeLike
Sijali matokeo mimi naweka kazi!
LikeLike
Kazi inapaswa kuwekwa bila kujali kingine chochote.
LikeLike
Sijali naweka Kazi ndio maana Nina uhakika Wa ushindi
LikeLike
Weka kazi kujihakikishia ushindi.
LikeLike