3184; Haina Mjadala.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye safari ya kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha, lazima uwe na mchakato ambao unaufuata mara zote bila kuacha.
Unapaswa kuwa na mambo ambayo utayafanya bila ya kuruhusu hofu au sababu zozote zile kukuzuia.
Hii ni dhana inayoitwa Haina Mjadala (Non Negotiable).
Kwenye mambo hayo, hupotezi muda kujiuliza kama utafanya au hufanyi au ufanye muda gani.
Ni utafanya, kwa muda uliopanga kufanya, iwe unajisikia kufanya au la.
Tupo hai kwa sababu kuna mambo huwa tunayafanya bila ya mjadala.
Hujadili iwapo upumue au la, bali unalazimika kupumua, kwa sababu ni muhimu.
Kadhalika hata uwe umetingwa kiasi gani, huwezi kuahirisha kula chakula kwa siku kadhaa.
Hayo ni mambo muhimu, ambayo lazima uyafanye, liwake jua, inyeshe mvua.
Kama umeweza kula na kupumua kila siku, licha ya matatizo na changamoto nyingi ambazo umekuwa unakabiliana nazo, basi pia unaweza kupata mafanikio makubwa, hata kama unaanzia wapi.
Kitu pekee unachohitaji ni kuwa na mchakato wako wa mafanikio ambao unautekeleza kila siku bila ya mjadala.
Unapanga na kisha kufanya kama ulivyopanga.
Bila ya kuwa na hofu wala kukwamishwa na sababu zozote zile.
Ukishakuwa na hofu ya kufanya kitu, hofu hiyo inaendelea kuwa na nguvu kadiri unavyokuwa hukifanyi kitu hicho.
Ukishakuwa na sababu za kutokufanya kitu, kila wakati sababu hizo zitakuwa zinajitokeza.
Kusahau, kupitiwa na kuchoka ni mambo ambayo huwa yanatolewa na wale ambao hawajajitoa kweli kupata kile wanachotaka.
Lakini mtu anapokitaka kitu kweli na akawa hana mbadala mwingine wowote, lazima atakipata au atakufa akikipambania.
Huwa kuna kauli inayosema nionyeshe ratiba yako ya kila siku na nitakuonyesha utaenda kuwa mtu wa aina gani.
Hili halihitaji mtu uwe na nguvu za kutabiri mambo yajayo.
Bali unahitaji tu kuangalia yale mambo ambayo mtu anayapa kipaumbele zaidi na kujiuliza kama ataenda nayo hivyo kwa miaka mingi ni matokeo gani atapata?
Kwa sababu sisi binadamu ni viumbe wa tabia. Chochote tunachofanya mara moja, huwa tuna nafasi kubwa ya kurudia tena kufanya.
Hakuna kitu ambacho tunakifanya mara moja tu kwenye maisha yetu.
Huwa tunafanya kwa kurudia rudia.
Ndiyo maana mtu anayeshindwa kufanya kitu fulani ambacho ulitaka afanye, kwa sehemu kubwa hatafanya, hata kama atakuahidi kufanya.
Utahangaika naye sana, lakini mwisho wa siku hatafanya, kwa sababu ndivyo alivyo.
Kila unapokubali hofu ikuzuie kufanya kitu, unazidi kuipa hofu hiyo nguvu ya kuendelea kukuzuia kufanya. Hivyo ufanyaji unaendelea kuwa mgumu kwako.
Kila unaporuhusu sababu yoyote ikukwamishe kufanya, maana yake umejiambia wewe mwenyewe na wengine wote kwamba kuna vitu vingine muhimu kwako kuliko kufanya hicho ulichopanga kufanya.
Na kama kitu siyo muhimu kabisa kwako, hakuna namna kitafanyika.
Ni mambo gani kwenye mchakato wako wa mafanikio umeshayafanya kuwa haina mjadala?
Mambo gani ambayo kila siku lazima uyafanye hata iweje?
Karibu ushirikishe kwenye maoni hapo chini.
Muhimu ni shirikisha yale ambayo tayari unayafanya kila siku na siyo yale ambayo unatamani ungeweza kuyafanya kila siku.
Kuna tofauti kubwa sana hapo ambapo usipoielewa utajikwamisha sana kupiga hatua.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Mambo ninayofanya bila mjadala. Non negotiable!
Kukaa kwenye mchakato kila siku.
Kusona.
Kuandika.
Kuwasiliana na wateja tarajiwa waliokaribia kununua.
LikeLike
Safi sana,
Komaa humo humo.
LikeLike
Mambo ninayo yafanya kila siku nikuwa kwenye kiwanda kwasababu mimi ni mupya kwenye biashara ya uzalishaji wa mawesa nahakikisha nakuwa hapo kila siku ili niijue biashara yangu kwa kinaa
LikeLike
Vizuri sana, kuwa na ufuatiliaji wa karibu wa biashara yako.
LikeLike
Mambo ambayo nafanya.
Kushiriki vipindi vya BIT sio mjadala haijalishi nimelala saa ngapi.
Kujifunza kufanya Quiz.
Kuhudumia wateja wangu.
Kusimamia fedha na biashara yangu.
Maelekezo ninayopewa aidha kocha clabu_hugeuka kuwa lazima ili yaweze kutekelezwa
LikeLike
Safi sana, simama imara hivyo na utafanya makubwa.
LikeLike
Mambo ninayo yafanya kila siku ni:
kushiriki katika vipindi vya BIT na uweka katika matendo.
kufika ofisini asubuhi na mapema.
kuwasiliana na wateja kwa lengo la kukuza mauzo.
LikeLike
Vizuri, weka msimamo kwenye hayo.
LikeLike
Mambo ninayofanya kila siku, ukiacha ninayofanya ili niishi na afya bora:
Ufugaji Kuku: kujifunza kila siku kitu kuhusu Kuku, mazao yake, manufaa kweye biashara na lishe kwa familia.
Bustani ya mboga na Matunda: matunzo kwa ajili ya chakula na biashara.
LikeLike
Vizuri, endelea kufanya.
LikeLike
Mambo ambayo nayafanya kila siku ni kijifunza kila siku najifunza
Asante sana
LikeLike
Vizuri sana,
Endelea na hilo.
LikeLike
HAKUNA MJADALA. Kitu pekee ambacho najivunia kufanya kwa sasa kila siku ni vitatu, kuandika, kusoma na kufundisha.
Asante sana
LikeLike
Safi sana, endelea na hayo kwa msimamo.
LikeLike
Asante Sana Kocha. Huu ujumbe umezidi kuniamsha zaidi na kunitaka nifanye zaidi maana nayataka mafanikio Kama Pumzi. Mambo nayaoyafanya kwa msimamo ni
1. Kuhudhuria na kufatilia BM
2. Kukamilisha mchakato wa Changamoto ya siku 100
3. Kusali au kufanya Tahajudi
4. Kuishi Ustoa
Najiona Nina Deni kubwa la kulipa kabla ya maiti yangu
LikeLike
Safi sana, yasimamie hayo.
LikeLike
,
Kitu ambacho nafanya bila mjadala
1. Kuamka saa kumi na kushiriki kipindi Cha BM
2. Kufanya sala kila siku asubuhi
3. Kusimamia Mzunguko wa fedha binafsi na kwenye biashara
4. Kuwasiliana na timu na Wateja
5. Kusoma na Kuandika na kujifanyia tathmini.
Asante
LikeLike
Vizuri sana,
Kaa humo.
LikeLike
Asante kocha,Mambo ninayoyafanya kila siku, nikujifunza mafunzo ya bm na kukaa kwenye mchakato bila kuacha na kufuatilia mwenendo wa biashara kila siku.
LikeLike
Vizuri, yazingatie hayo.
LikeLike
-Kichina
-Kujifunza biashara
-Kuwafuatilia waliifanikiwa kuliko mimi
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Mambo ninayofanya kila siku ni kufuatilia mchakato wa BM
LikeLike
Vizuri
LikeLike
1.Kuonekana Nina roho mbaya
2.Kutokujali wengine wanasema nini
3.Taking risk
4.kujifunza endelevu, nimechagua kujifunza siku zote nitakazokuwa hai hapa duniani
5.Maamuzi Magumu.
6.Kuwa na malengo makubwa sana
LikeLike
Vizuri, endelea kwa msimamo.
LikeLike
Jambo ambalo halina mjadala ni kuamka kila siku na kuweka akiba kila siku..
LikeLike
Vizuri
LikeLike