3209; Ngumu kutunza kuliko kutengeneza.
Rafiki yangu mpendwa,
Unapokuwa unaanzia chini kabisa, kiu yako kubwa inakuwa ni kufanikiwa na kufika juu.
Unakuwa tayari kufanya kila kinachopaswa kufanyika ili upate matokeo unayoyataka.
Safari inaweza kuwa ngumu, lakini kwa sababu ya kujitoa kweli kweli, unafika ulikokuwa unataka kufika.
Hapo sasa ndipo penye hatari kubwa sana kwenye maisha ya mafanikio.
Kwani baada ya kupata mafanikio fulani ndipo wengi wanajisahau, wanaacha kufanya yale yaliyowafikisha walikotaka kufika.
Matokeo yake ni watu kupata anguko kubwa kila baada ya mafanikio wanayokuwa wameyapata.
Kwa maneno mengine kutunza mafanikio ni kugumu kuliko kuyatengeneza mafanikio hayo.
Kuyatengeneza mafanikio kunahitaji mambo machache ambayo yanapaswa kufanyika kwa uhakika na msimamo.
Unapaswa kujua kwa hakika kile hasa unachotaka, kuamua kwamba utakipata na kisha kufanyia kazi mpaka kukipata.
Ukishakipata sasa, unakuwa hujamaliza matatizo yako, bali unakuwa umefungua matatizo mengine mapya kabisa.
Ambayo ni matatizo ya kutunza kile ambacho mtu ameweza kukitengeneza.
Wengi kwa kukosa mafunzo ya aina hii mapema, huwa wanajikuta kwenye mlolongo wa kutafuta na kupoteza.
Njia bora ya kuondokana na yote hayo ni kujifunza kuyatunza mafanikio kama unavyokazana kuyatengeneza.
Kwanza kwa kuhakikisha wale wanaotaka kunufaika nayo umewazuia wasiweze kujipenyeza.
Mafanikio kwa wengi imekuwa ni kitu kigeni kiasi kwamba wanapoyapata wanakuwa na mahangaiko makubwa.
Ni mahangaiko hayo ndiyo yanayowapelekea kupoteza mafanikio yanayokuwa yamepatikana.
Huwa kuna kauli inasema, Mungu akitaka kukuadhibu anakupa kile hasa unachotaka.
Inaweza kukushangaza hiyo imekaaje, lakini huhitaji hata kufikiria sana.
Wewe angalia tu mifano ya watu waliopata fedha nyingi kwa pamoja.
Labda ni mtu kashinda bahati nasibu, kapata urithi au mafao.
Tunajua kwa mifano halisia kwamba fedha hizo huwa hazidumu kwa muda mrefu.
Na zaidi, zinamwacha mtu akiwa kwenye hali mbaya kuliko alivyokuwa awali.
Kadiri unavyokazana kuyajenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako, ndivyo pia unavyopaswa kukazana kujifunza jinsi ya kuyatunza mafanikio hayo.
Weka mipango ambayo utaitekeleza hata kama utakuwa umeshapiga hatua kubwa.
Na muhimu zaidi, chagua mchakato ambao utauishi kwa maisha yako yote, iwe una mafanikio au huna.
Yafanye maisha yako yote kuongozwa na mchakato uliochagua na kamwe usiache kutekeleza mchakato huo bila kujali matokeo unayokuwa umeshapata.
Kinachowafanya wengi kushindwa baada kupata mafanikio kidogo ni kuuacha mchakato na kuishi maisha ya tofauti.
Hapo ndipo wanapojikuta wakirudi nyuma.
Wewe unajua vyema, wajibu wako namba moja ni kuendelea kukaa kwenye mchakato mara zote na kwa msimamo bila kuyumba.
Usikubali kupoteza kirahisi kile ambacho umehangaika sana kukipata.
Jifunze kutunza kama unavyokazana kutengeneza.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kweli jifunze kutunza kama unavyokazana kutengeneza.
LikeLike
Bila hivyo tutakuwa na mahangaiko ya bure.
LikeLike
Asante sana kocha. Kupata mafanikio ni kitu kimoja, kutumza mafanikio ni kitu kingine.
Muhimu ni kuwa ma mchakato unaofuatwa kila mara kwa msimamo.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Kazi si kutengeneza tu,kazi ni kutunza mafanikio.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ni kweli kutunza ni ngumu sana kuliko kutafuta na kubaki nacho ukiweza kupata mafunzo ya kutunza ni muhimu zaidi ili uendelee kubaki nacho na kikusaidie kufika mbali au kufikia mafanikio makubwa zaidi
Muhimu sana ni kuishi maisha ya kawaida kama ulivyokuaga bila ya kupata mafanikio yaani kama ulifanikiwa mil 200 maisha yako ukiwa na watu yasikubadilishe hadi kujionyesha kwa watu kuwa unazo hadharani hapana uwe wa kawaida tu kama ulivyokua ila ikubadilishie kuelekea mafanikio mengine invest slowly and silently
LikeLike
Hiyo ndiyo siri kuu, usibadilishe maisha haraka.
LikeLike
Ni kweli kabisa changamoto ipo kwenye utunzaji zaidi na sio kupata
Asante sana
LikeLike
Tukazane kutunza.
LikeLike
Nakubaliana na hili
LikeLike
Vizuri, fanyia kazi.
LikeLike
Kuyatunza mafanikio kunahitaji ujasiri maana changamoto zake ni kubwa na ngumu kuliko ulipokuwa huna mafanikio. Wanasema kupata ushindi ni rahisi maana unaweza kuwa ulibahatisha ukashinda ika kubakia nao na kuulinda huwezi kubahatisha maana bahati haiwi kwako milele. Mafanikio sio kilema kwamba ukikipata basi kimekuwa chako…nooo.
Kutunza mafanikio au ushindi inahitaji mikakati na juhudi kubwa.
LikeLike
Tunahitaji kuweka kazi kubwa kuyatunza mafanikio kama tulivyoyatengeneza.
LikeLike
Asante Kocha,
Sitakubali kupoteza kirahisi kile ambacho nimehangaika sana kukitafuta na kukipata, nitajifunza kukitunza kama ambavyo ninakitengeneza.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante kocha,Njia sahihi ya kuweza kutunza utajiri ni kukaa kwenye mchakato bila kuyumba.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha kwa makala hii,
Ninajifunza kutunza mafanikio kama ninavyokazana kutengeneza,,, Nimechagua mchakato ambao nitauishi kwa maisha yangu yote iwen nina mafanikio au sina.
LikeLike
Vizuri na kila la kheri.
LikeLike
Asante sana kocha uki sahihi sana kwa hilo
LikeLike
Karibu
LikeLike