3241; Kufanya na kupiga hatua.
Rafiki yangu mpendwa,
Ni wengi wanaokuwa na mipango mikubwa kwenye maisha yao.
Lakini wanaochukua hatua ya kufanya kwenye mipango waliyonayo ni wachache sana.
Watu wanaopanga lakini hawafanyi, siyo kwa sababu hawawezi kufanya, bali ni kwa sababu wanakosa mwongozo sahihi wa kufanya.
Ili wewe uweze kufanya na kupiga hatua kwenye maisha yako, unapaswa kuzingatia yafuatayo.
Fanya kila siku.
Ni rahisi kuendelea kufanya kuliko kuanza upya baada ya kuwa umeacha.
Hivyo kama unataka kufanya na kupiga hatua, fanya kila siku bila kuacha.
Usiruhusu sababu yoyote ikukwamishe kufanya.
Fanya hadharani.
Fanya kwa kuonekana na wengine kwamba unafanya.
Waambie wengine kile unachotaka kufanya na jinsi ulivyojitoa ili kukipata.
Kadiri wengi wanavyojua mipango yako, ndivyo wanavyokukumbusha pale unapoacha kufanya au unapofanya yasiyokuwa sahihi.
Fanya kwa kushirikiana na wengine.
Ukiwa unafanya mwenyewe ni rahisi kukubali sababu na kuacha kufanya.
Lakini unapokuwa unafanya kwa kushirikiana na wengine, unalazimika kufanya hata kama huna kwa sababu hutaki kuwaangusha wengine.
Fanya kwa lazima.
Kuwa na kitu kinachokulazimisha ufanye la sivyo unapata madhara au kuingia gharama kubwa.
Hii inaweza kuwa ahadi umetoa kwa wengine kama utaacha kufanya au kuyumba.
Hapa pia ndipo mtu wa kukusimamia ufanye anapoingia, ambaye anahakikisha unafanya hasa na hakubaliani na sababu zako kirahisi.
Fanya zaidi ya unavyofikiria.
Wakati unapanga kufanya, kuna picha fulani ulikuwa nayo.
Wakati unaingia kufanya, mambo yanakuwa tofauti na ulivyokuwa unafikiria.
Hapo ndipo wengi hukata tamaa na kuacha.
Lakini wewe unapaswa kuendelea kufanya hata kama mambo hayajaenda kama ulivyotarajia.
Anayefanya mara zote huwa anazalisha matokeo tofauti ukilinganisha na wasiofanya.
Wewe weka kipaumbele kwenye ufanyaji kwa kuzingatia hatua ulizojifunza hapa.
Ukawe na ufanyaji bora, unaokupa matokeo makubwa unayoyataka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Fanya zaidi ya unavyofikiria.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Fanya kila siku,
Fanya hadharani,
Fanya kwa kushirikiana na wengine,
Fanya kwa lazima na
Fanya zaidi unavyofikiria.
Asante kocha kwa hatua hizi.
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike
Fanya bila sababu na matokeo yatakuja yenyewe
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitaweka kipaumbele kwa kuzingatia hatua zifuatazo:-
1. Kufanya kila siku
2.Kufanya hadharani
3. Kufanya kwa kushirikiana na wengine
4. Kufanya kwa ulazima
5. Kufanya zaidi ya ninavyofikiria
Nitafanya kwa ubora na kupata matokeo makubwa ninayoyataka.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kama unataka kufanikiwa fanya kila siku bila kuacha
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Anayefanya mara zote huwa anazalisha matokeo tofauti ukilinganisha na wasiofanya.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kuendelea kufanya kwa msimamo kila siku bila kuacha hata siku ndiyo njia kuu ya kuelekea kwenye ushindi MKUU
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Nitafanya like ninachotakiwa kufanya kila siku.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nitaendelea kufanya kila siku kwa lazima yaliyomuhimu sana bila kuangalia yeyote ila kwa kutambua umuhimu wake.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante Kocha,
Nitaendelea kufanya mara zote kile nilicho panga hata pale matokeo siyo matarajio. Nikikosea nitatambua pa kurekebisha hivyo kuwa bora zaidi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nitajitahidi kufanya kila siku. Asante kwa makala
LikeLike
Vizuri
LikeLike