3244; Mara moja moja na kila mara.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye maisha kuna mambo ambayo mtu unaweza kujikusanya na kuyafanya mara moja moja.
Yanaweza kuwa mambo makubwa na ya kishujaa, ambayo wengi hawawezi kuyafanya.
Lakini bado ni mambo ambayo hayawezi kumpa mtu mafanikio makubwa.
Hiyo ni kwa sababu mafanikio siyo zao la kufanya kitu mara moja moja, bali kufanya kila mara.
Ili uweze kupata mafanikio makubwa kwenye jambo lolote, lazima uweze kulifanya kila mara na kwa muda mrefu.
Kila unachofanya kinajikusanya na kuchangia mafanikio makubwa.
Sahau kuhusu kujikusanya na kuweza kufanya makubwa sana mara moja moja. Japo unaweza kufanya makubwa ndani ya muda mfupi, hayawezi kuchangia kwenye mafanikio makubwa na yanayodumu.
Unachopaswa kujenga ni uwezo wa kufanya kitu kila mara, kwa msimamo bila kuacha.
Hata kama unavyofanya ni vya kawaida, uwezo wa kufanya kila mara, unawezesha kuzalisha matokeo bora.
Ushujaa wa kuweza kufanya makubwa kwa muda mfupi unaweza kuwafurahisha watu.
Lakini mafanikio makubwa na yanayodumu ni zao yale unayofanya kila mara bila kuacha.
Kitu chochote ambacho utachagua kukifanya kila siku bila kuacha, hata kama hufanyi kwa ukubwa, mkusanyiko wa ufanyaji kwa kujirudia rudia una nguvu kubwa ya kuleta mafanikio.
Kwa maana hiyo basi, chochote unachopanga kuanza kufanya, jiulize kama unaweza kukifanya kila siku bila ya kuacha.
Kama jibu ni ndiyo, basi endelea kufanya, maana hapo kuna fursa ya kufanikiwa.
Lakini kama kuna chochote kinachoweza kukuzuia usifanye kila siku, basi hutaweza kufanya kila siku na hilo litakuzuia kupata mafanikio makubwa.
Kila mtu anaweza kujikusanya na kufanya jambo la kishujaa mara moja moja.
Lakini kufanya kila mara na kwa msimamo, hata kama ni vitu vya kawaida, wengi wanakwama.
Na pale wengi wanapokwama ndipo huwa na mafanikio makubwa.
Hivyo basi, kanuni ya mafanikio ni rahisi na imenyooka;
1. Chagua kile ambacho unaweza kukifanya kila mara bila kuacha.
2. Fanya kila mara hata pale unapokuwa na sababu ya kuacha kufanya.
3. Usihangaike sana na mambo magumu kabla hujafanya yale ya msingi kabisa.
Tukae humo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Vizuri sana Kocha Dr Makirita Amani. Chagua kile unachoweza kufanya na kifanye kila mara bila kuacha.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante kocha kwa makala ya leo kitu kikubwa nilichoondoka nacho ni hiki “Kitu chochote ambacho utachagua kukifanya kila siku bila kuacha, hata kama hufanyi kwa ukubwa, mkusanyiko wa ufanyaji kwa kujirudia rudia una nguvu kubwa ya kuleta mafanikio.” kuna nguvu kubwa sana ya kufanya kitu bila kuacha 2021 nilichagua kufanya biashara ya juisi bila kuacha licha ya changamoto nyingi nilizokutana nazo nimekomaa nazo sijaacha adi leo bado sijaacha nakomaa kwa kufanya naendelea kujifunza na kuwa bora pia nawavutia wale ambao mwanzoni walinikataa na nina imani kwa kuendelea kufanya nilichochagua nitafikia mafanikio makubwa.
LikeLike
Vizuri sana, endelea kukomaa, ushindi ni kutokuacha.
LikeLike
ASANTE sana nimechagua kuweka akiba ya elf 30 utt kila siku bila kuacha na naanza sasa
LikeLike
Safi sana, nenda hivyo kwa msimamo.
LikeLike
Nitafanya Yale ya msingi Mara kwa mara
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante Kocha,
Nitafanya yale ya msingi bila kutafuta sababu au visingizio vya kuacha kufanya.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Asante sana kwa makala nzuri nitahakikisha nafanya mambo ya msingi kwa wakati wote..
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Kufanya kwa muendelezo “Mimi na kichina-普通话” nilianza kujifunza January 2018-ni miaka michache imepita, ila kwa hakika kimefungua fursa za kipikee katika maisha yangu. Leo nafanya biashara na viwanda vinne 4 vya wachina, lengo langu kwa mwaka 2024 ni kuweza kufikia idadi ya viwanda kwa ujumla angalau 10 vya wachina. Nilianza nao kama walimu wangu baadae waajiri wangu na SASA tunahusiana kibiashara.
LikeLike
Vizuri sana, endelea kufanya kila mara.
LikeLike
Hakika kufanya kitu mara kwa mara baadae kinakuwa ni tabia na mali yako kabisa kama vile ukienda sehemu na kufanya mazoezi kila siku watu wanaanza kukuita mtu wa mazoezi sehemu zingine watu wanakuita mwanajeshi kutokana na hiyo nidhamu ya kurudia rudia
LikeLike
Hakika
LikeLike