3256; Njia mbili.
Rafiki yangu mpendwa,
Maisha huwa yana njia kuu mbili ambapo lazima mtu uchague moja ambayo ndiyo utaisafiri kwa kipindi chote cha maisha yako.
Njia ya kwanza ni ya mtu kuwa na ndoto kubwa ambazo unazipambania mpaka kuzifikia.
Ndoto hizo zinakuwa ni kubwa sana kiasi cha kukutaka uweke kila ulichonacho katika kuzipambania.
Mtu anayechagua njia hii anakuwa hana budi bali kupuuza mengine yote ambayo hayana mchango kwake kufikia ndoto kubwa alizonazo.
Ni wachache sana wanaoichagua hii njia. Wengi hujaribu na kuishia njiani, kwa kushindwa kujitoa kwa namna inavyohitajika.
Njia ya pili ni njia ya usumbufu ambapo mtu anahangaika na kila kinachokuja mbele yake.
Wanaopita kwenye njia hii huwa wanaamini uwepo wa njia ya mkato ya kupata chochote ambacho mtu anataka bila ya kufanya kazi sana.
Hilo linawapelekea kila wakati kuwa na kitu kipya wanachokimbizana nacho, kwa kuamini hicho ndicho kimebeba mafanikio yao.
Kwa bahati mbaya sana, watu wengi huwa hawapati hata nafasi ya kuchagua ni njia ipi watakayotumia.
Badala yake huwa wanajikuta tayari wapo kwenye njia ya pili, njia ya kuhangaika na mambo mengi yasiyokuwa na tija kwa mtu.
Kwa sababu hivyo ndivyo walio wengi wanavyoendesha maisha yao, imezoeleka na hata kuonekana ndiyo njia bora na ya kipekee.
Watu wengi huwa hawajui kama njia ya kwanza ipo. Hivyo maisha yao yamekuwa yanaenda kwa mazoea ambayo ndiyo wale waliowazunguka wanaenda hivyo.
Wanaojua uwepo wa njia ya kwanza ni wale ambao tayari ndani yao wana msukumo wa kufanya mambo makubwa zaidi ya ilivyozoeleka. Hawa tayari huwa wanajikuta kwenye njia ya kwanza na wakipambania kile wanachokitaka sana.
Wapo pia ambao huwa wanajua uwepo wa njia ya kwanza kupitia kujifunza.
Lakini pamoja na kujifunza na kujua, uhalisia huwa ni tofauti kabisa na mipango ambayo mtu anakuwa ameiweka.
Hivyo wengi wa wanaojifunza njia ya kwanza huwa hawaendi nayo kwa muda mrefu mpaka kupata matokeo makubwa. Wanapoanza kuifanyia kazi njia hiyo wanategemea matokeo ya haraka. Ni pale wanapokutana na changamoto au matokeo kuchelewa ndiyo safari huwa inaishia hapo na wanahamia kwenye njia ya pili.
Rafiki, kama bado hujaichagua njia ya kwanza kama njia yako kuu, fanya hivyo sasa.
Chagua kitu kimoja ambacho ndiyo utakipambania kwa maisha yako yote.
Kisha kipe kitu hicho kipaumbele namba moja kwenye maisha yako.
Vitu vingine vyote vinafuata baada ta kitu hicho, hivyo hata ufanyaji wa vitu vingine, haupewi nafasi ya kuvuruka kilicho kikuu.
Kubali maisha yako yazamie kwenye kile kikubwa kimoja unachotaka kufikia.
Kuwa bora sana kwenye kitu hicho kiasi cha kuweza kupuuza mengine yote.
Toa thamani kubwa sana kwa wengine kupitia kile ulichochagua kufanya, kiasi cha watu hao kuwa tegemezi kwako kwenye kukamilisha mambo yao.
Kuyatoa maisha yao kwa ujumla ili kuweza kufikia ndoto kubwa unazokuwa nazo ni njia yenye uhuru mkubwa kwa anayeielewa njia hii na kukubaliana nayo.
Kataa kufuata mkumbo wa kuhangaika na mambo yasiyokuwa na tija, kwa sababu hilo ndiyo linalowapoteza walio wengi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Njia mbili
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Ni kukaa kwenye njia moja.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Njia ya kwanza ndio mpango mzima katika kufikia maendeleo makubwa
Asante sana
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kataa kufuata mkumbo wa kuhangaika na mambo yasiyokuwa na tija, kwa sababu hilo ndiyo linalowapoteza walio wengi.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante Kocha,
Katika njia mbili, nitatumia njia ya kwanza isiyofuata tu mkumbo.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
(MVFF) nimechagua kitu kimoja ndiyo nitapambana kwa maisha yangu yote.
🙏🙏🙏
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Nimechagua njia ya kwanza, kuepuka usumbufu
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Nimechagua kuwa na ndoto kubwa ambazo ninazipambania mpaka kuzifikia na ninakataa njia za usumbufu za kuhangaika na kila kinachokuja mbele yangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nina ndoto kubwa sana ya kuwa tajiri mkubwa. Sitafuata mkumbo nitaipambania ndoto yangu
LikeLike
Safi sana, kaa humo.
LikeLike
Nimekuwa nakomaa na njia mbili, hakika nakwenda kubadilika na kubaki kwenye NJIA MOJA PEKEE mpaka kufikia malengo makubwa niliyonayo.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Mimi kwakweli nikiri aazi kuwa njia ya pili imenipa matokeo mabaya sana hadi kubaki njia panda hadi hapo nilipokuja kukutana na kocha na sasa nimechagua kubaki njia ya kwanza hadi kupata ubilionea bila shaka yoyote
LikeLike
Umefanya maamuzi mema, kaa humo.
LikeLike
inabidi kuwa na lengo kubwa sana linalokunyima usingizi. Linakuamusha asubuhi na mapema na linakufanya uchelewe kulala.
LikeLike
Ndiyo, huo ndiyo msukumo utakaokupa makubwa.
LikeLike
Asante sana kocha,huko kwenye kufuata mkumbo nashkr nilishatoka sasa ni kupambania ndoto yaku kubwa biashara na uwekezeji.
LikeLike
Safi sana kwa maamuzi hayo na kila la kheri kwenye kupambana.
LikeLike
Asante kocha nimechagua njia ya kwanza Nina ndoto kubwa ambazo nazipambania mpaka kuzifikia.Sitahangaika na chochote kinachokuja mbele yangu.
LikeLike
Vizuri sana, zingatia hilo.
LikeLike
Nimechagua njia ya kwanza kama njia yangu kuu ktk kuyaendea mafanikio makubwa ninayoyataka.
LikeLike
Safi sana na kila la kheri.
LikeLike
Njia ya kutohitaji usumbufu nitaweka nguvu zangu zote kwenye kuuza gesi na vifaa vyote vinavyohusu gesi. Asante Kocha.
LikeLike
Safi sana, fokasi kwenye eneo hilo mpaka upate ukuaji mkubwa kabla hujahangaika na mengine.
LikeLike
Njia yangu kuu ni kuwa na ndoto ya ubilionea kupitia biashara na uwekezaji. Nina uhakika nitafikia ndoto yangu au nitakufa nikiwa naipambania zaidi ya hapo hakuna njia mkato
LikeLike
Safi sana kwa kuchagua na kukubali mapambano, kaa humo.
LikeLike
nachagua njia ya kuifikia ndoto yangu. Hakuna kingine zaidi ya hicho
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Njia kuu tu ili kufikia ndoto kubwa nilizonazo.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Nimechagua njia ya kwanza na nitabaki hapo
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Njia yangu kuu ni kilimo cha Mkonge,hii nina uhakika wa kufikia mafanikio yangu makubwa ninayoyataka.
LikeLike
Safi sana, pambania hapo.
LikeLike