3288; Hatua unayochukua.
Rafiki yangu mpendwa,
Kila mtu kuna vitu anavyokuwa anavitaka kwenye maisha yake.
Na anaweza kujiwekea malengo na mipango mbalimbali juu ya vitu anavyotaka.
Lakini ili mtu aweze kupata kile anachotaka, anapaswa kuchukua hatua kwenye yale anayopanga.
Hilo ni la msingi kabisa, lakini limekuwa linapuuzwa na wengi.
Wengi wanadhani kupanga na kusema inatosha kuwaletea yale wanayoyataka.
Kuna ambao wanaanza kuchukua hatua, lakini wanapokutana na magumu au changamoto mbalimbali wanaacha kwa kuona haiwezekani.
Hawa nao hawapati wanachotaka, siyo kwa sababu haiwezekani, bali kwa sababu hawajafanya kadiri ya inavyohitajika.
Kuna wanaofanya, lakini matokeo yanapochelewa wanaacha kufanya. Wanaona kuchelewa kwa matokeo ni kutokuwezekana kwa kitu.
Halafu sasa, kuna ambao wanafanya, wanapata matokeo makubwa, halafu wanaacha kufanya kwa kuona wameshamaliza kila kitu.
Hawa nao huwa wanapata anguko kubwa baadaye.
Mafanikio na kufanya ni vitu ambavyo vinakwenda pamoja na haviwezi kutenganishwa.
Tangu mtu anapoanza mpaka anafanikiwa, lazima awe anaendelea kufanya bila ya ukomo.
Ni kupitia kufanya ndiyo mtu anaweza kujifunza na kuwa bora zaidi.
Kwa kufanya, mtu anapiga hatua kubwa sana kuliko kupanga na kusema pekee.
Unachotaka na unachofanya vinapaswa kwenda pamoja ili uweze kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.
Usiwapigie watu kelele sana juu ya nini unachotaka.
Bali waonyeshe kwa yale unayofanya.
Fanya wakati wote, bila kuchoka wala kuacha na utaweza kuzalisha matokeo makubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Usiwapigie watu kelele juu ya nini unachotaka, bali waonyeshe kwa yale unayofanya.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Mafanikio na kufanya ni vitu vinavyokwenda pamoja.Nitaendelea kufanya licha ya matokeo kuchelewa au kupatikana.
LikeLike
Kupitia kufanya ndio mtu anajifunza..
Sio kupiga kelele kwa unachotaka Bali waonyeshe unachofanya.
🙏🙏🙏
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Vizuri na kila la kheri.
LikeLike
Asante,kocha sitawapigia watu kelele bali nitafanya ili nipige hatua kubwa kwa sababu mafanikiona kufanya ni vitu vinavyoenda pamoja. Nitaendelea kufanya ata kama nitafanikiwa sitaacha kufanya.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Fanya wakati wote, bila kuchoka wala kuacha na utaweza kuzalisha matokeo makubwa.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Panga na waonyeshe kwa vitendo na ufanye kila mara na kwa muda mrefu ili kupata matokeo mazuri
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kupanga bila kufanya ni kujidanganya
LikeLike
Kweli
LikeLike
Mafanikio na kufanya vinakwenda pamoja.
Huwezi kuvitenganisha
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nitawaonyesha watu kile ninachotaka kwa kufanya badala ya kusema. Asante kocha
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ni kupitia kufanya ndiyo mtu anaweza kujifunza na kuwa bora zaidi.asante sana
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike