3296; Hakuna kingine muhimu.

Rafiki yangu mpendwa,

Sababu namba moja ya watu wengi kushindwa kupata matokeo makubwa waliyokuwa wanayataka ni kutawanya nguvu zao kwenye mambo mengi.

Wanakuwa wanapambania vitu vingi kwa wakati mmoja, kitu ambacho kinapunguza ufanisi wao.
Kwa sababu hata kama watapata matokeo, yanakuwa ni ya kawaida sana.

Matokeo makubwa sana huwa yanapatikana pale mtu anapoweka rasilimali zake zote kwenye kitu kimoja.
Anachagua kitu kimoja tu ambacho ndiyo kinakuwa muhimu zaidi kwake.
Hapo anakuwa hakuna kingine muhimu kwake isipokuwa hicho alichochagua.

Baada ya kuchagua kitu kimoja ambacho ndiyo pekee muhimu, anapaswa kuyataka sana matokeo anayokuwa anayategemea.
Yaani kitu pekee anachokuwa anakiona kwenye hicho anachofanya ni yale matokeo anayokuwa anategemea kuyapata.

Kila wanapoangalia, wanachoona ni yale matokeo makubwa wanayokuwa wanayataka.
Hivyo ufanyaji wao wote unakuwa umesukumwa na matokeo hayo.
Hakuna namna anapokea kingine chochote chini ya kile anachotaka kupata.

Kwa kukataa kupokea vitu vya chini, moja kwa moja anakuwa amejipandisha juu na kupokea vilivyo juu kweli.
Jambo moja la kushangaza kuhusu dunia ni pale unapokataa kupokea chochote chini ya unachotaka, unapata unachotaka.

Chagua kile hasa unachotaka, puuza vingine vyote. Weka jugudi kubwa. Kataa matokeo yoyote ya chini ya unayoyategemea.
Ukidhamiria hayo kweli, utaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.

Ukihangaika na mengi, hupati chochote kikubwa. Unatawanya sana nguvu zako bila ya mafanikio makubwa.
Ukihangaika na kimoja, unajiongezea uhakika wa kukipata.
Ni juu yako kuchagua njia ipi uende nayo, kwa sababu hakuna mwingine anayeweza kukufanyia maamuzi hayo.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe