IANZE SIKU YAKO HIVI….

  Waswahili wanasema ‘nyota njema huonekana asubuhi’, hawakuishia hapo, wanasema pia ‘biashara asubuhi, jioni mahesabu’. Kwenye semi hizo inaonesha kabisa kwamba mambo yote yanategemea mwanzo ukoje. Yaani jibu la mwisho inategemea na umeanzaje.

new daynew day2

  Hivyo ndivyo ilivyo kwa siku pia, siku inayokwenda vizuri na kuisha vizuri ni siku iliyanzwa vizuri. Usitegemee kuanza siku yako kwa kisirani halafu iishe kwa furaha, ni ngumu sana.

  Ianze siku yako kwa mambo makuu mawili, kwanza furahia na shukuru kwa kuianza siku na pili tegemea kufanya makubwa kwenye siku yako.

  Shukuru kwa kuiona siku mpya na furahia kwa kuwa ni siku pekee unayoweza kufanya kile ulichopanga kufanya. Hakikisha hakuna ‘anaekuvuruga’ na kundoa furaha yako asubuhi na mapema. Jitahidi kufurahia siku yako asubuhi ili siku nzima ujawe na furaha.

  Tegemea kufanya makubwa kwenye siku yako. Tayari umepanga siku yako kabla ya kulala, na leo umeamka ukiwa na furaha tayari kwa kwenda kutekeleza mipango yako. Tegemea matokeo mazuri na makubwa kutoka kwenye mipango yako. Tegemea kufanya mabadiliko na kusaidia watu.

  Hakikisha uso wako umevaa tabasamu siku nzima, ndio, tabasamu kwa sababu umeamua kuyafurahia maisha. Usikubali tabasamu lako liondolewe na mtu ama kitu chochote. Kama kuna kitu ama mtu anakuharibia tabasamu lako basi ni bora kutafuta njia ya kubadili hiyo hali.

smilesmile2

  Siku hii ni yako na wewe mwenyewe ndiye unaeweza kuchagua jinsi unavyotaka iende. Amua kuwa na siku nzuri iliyojaa furaha na uzalishaji. Anza siku yako vyema na uyafurahie maisha.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: