Amka mtanzania iliandaa semina iliyofanyika ubungo plaza siku ya jumamosi tarehe 18/01/2014. Semina hiyo ilifanyika kwa mafanikio makubwa na wahudhuriaji walijifunza mengi.

  Mada zilizozungumzwa ni;

1. Wewe ni zaidi ya unavyojijua.

2. Wewe ndiye kiongozi mkuu wa maisha yako.

3. Umuhimu wa kujihamasisha na kujiendeleza binafsi.

4. Jinsi ya kuweka malengo makubwa na utakayoyafikia.

    a. umuhimu wa kuweka malengo

    b. lengo kuu kwenye maisha

    c. aina tano za malengo unayotakiwa kuweka

    d. hatua saba za kuweka malengo ambapo lazima utayafikia.

5. Makosa makubwa unayofanya wakati wa kuweka na kutimiza malengo yako na jinsi ya kuyaepuka.

6. Safari ya kuelekea kwenye mafanikio ya uchumi binafsi.

1.semina

  Pamoja na semina kufanika kwa mafanikio makubwa kulikuwa na changamoto kubwa ambayo ilikuwa ni mahudhurio ya watu. Watu waliohudhuria semina ni wachache sana ukilinganisha na watu waliojaza fomu kwamba watahudhuria.

  Baadhi ya waliojaza fomu walitoa udhuru wa kutohudhuria ila zaidi ya nusu ya watu waliojaza fomu hawakutoa taarifa yoyote na hawakuhudhuria licha ya kukumbushwa mara nyingi. Hii imekuwa ni changamoto kubwa.

  Kutokana na watu wengi walioko nje ya dar es salaam kuhitaji mafunzo ya semina hii, tutaitoa tena semina hii kwa njia ya email. Mafunzo yatakayotolewa kwa email ni JINSI YA KUWEKA MALENGO MAKUBWA UTAKAYOYAFIKIA NA JINSI YA KUEPUKA MAKOSA UNAYOYAFANYA KWENYE KUWEKA MALENGO.

  Kama ulishindwa kuhudhuria semina hii ni nafasi nyingine ya kujifunza kuhusu kuweka malengo. Ni somo zuri na pana ambalo watu wengi wanashindwa kuelewa umuhimu wake. Mafunzo haya kwa njia ya email yatafanyika kwa siku tano ambapo kila siku utatumiwa sehemu ya mafunzo. Gharama ya mafunzo haya ni tsh 10,000/=. Kama unataka kushiriki mafunzo haya tuma email kwenda amakirita@gmail.com na useme unataka kushiriki mafunzo kwa njia ya email ili upewe utaratibu.

  Karibu sana na nakutakia kila la kheri kwenye mwaka 2014 uwe wa mafanikio makubwa kwako.

  Kwa wale ambao walishindwa kufika kwenye semina ila wangetamani kuwepo tafadhali weka maoni yako hapo chini ni changamoto gani ilikufanya ushindwe kufika. Maoni yako ni muhimu sana kwenye maandalizi ya semina ijayo. Tafadhali usiondoke bila kuacha maoni yako. Asante sana.