Siku chache zilizopita niliweka makala iliyokuwa inaelezea faida tano za kuwa na blog na nikawashauri watu wawe na blog. Kama hukuisoma makala hiyo isome hapa(Tengeneza blog yako leo na upate faida hizi tano). Pia nilitoa nafasi kwa wanaohitaji huduma hiyo ya blog wawasiliane na mimi ili tuone jinsi tunavyoweza kusaidiana.

             bloging

  Kwa siku mbili baada ya kuweka makala hiyo nimepokea emails na meseji nyingi sana za watu wanaotaka huduma hii ya blog. Ni kitu kizuri sana na kimenipa faraja kubwa kwamba watu sasa tunaona umuhimu wa kujiboresha na kuboresha shughuli zetu na hii itatusaidia kujitofautisha na watu wengine. Nitumie nafasi hii kuwapongeza wale wote ambao wana mpango wa kuwa na blog. Utayafurahia matunda yake baadae na utashukuru sana kwa kuweza kuwa na blog yako.

  Ili kuweza kuwasaidia watu wengi zaidi kupata huduma hii ya blog nimeandaa huduma za aina mbili. Huduma hizi zitakuwa na gharama kidogo sana ili kumwezesha kila anayehitaji huduma hii aweze kuipata.

  Huduma hizo zitakuwa kama ifuatavyo;

1. Huduma ya kwanza ni kuandaliwa blog nzuri na yenye vitu vyote vya msingi na baada ya hapo mtu anaanza kuitumia blog yake moja kwa moja bila ya kupata usumbufu wa kujaribu kurekebisha rekebisha. Gharama ya huduma hii kwa kawaida huwa nafanya kwa shilingi za kitanzania elfu hamsini(50,000/=) ila kwa kipindi hiki natoa ofa kwa kufanya kwa shilingi elfu thelathini(30,000/=). Ofa hii itakwenda kwa siku chache tu hivyo kama utaihitaji chukua hatua mapema. Gharama hii ni kwa mara moja tu na baada ya hapo unaendelea kutumia blog yako bure kabisa kwa muda wowote utakaotaka.

  Huduma hii inawafaa watu wote ambao hawana muda wa kujifunza kufanya hivi vitu wenyewe na wanataka blog zao mara moja ili waanze kuzitumia.

2. Huduma ya pili ni kuingia kwenye mtandao(blog) itakayokuwa inafundisha mbinu mbalimbali za kuanzisha, kuboresha na kukuza blog. Blog hii itakuwa na mafunzo mengi sana yanayohusu kublog na pia mafunzo yatakuwa yakiendelea kutolewa kulingana na hitaji la mtu. Kwa huduma hii utapewa nafasi ya kuweza kutembelea blog inayoitwa KISIMA CHA MAARIFA. Gharama ya huduma hii ni shilingi elfu kumi(10,000/=) na unalipa mara moja tu. Ukishalipa hiyo elfu kumi unapata nafasi ya kutembelea blog hiyo kwa wakati wowote utakaohitaji wewe, kusoma mafunzo mbalimbali na kuuliza maswali na maelekezo mengine. Blog hii ni private hivyo inaweza kuonekana kwa watu walioruhusiwa tu, jaribu kuibonyeza jina lake(KISIMA CHA MAARIFA) utaambia you have no permission. Ili kupata ruhusa ya kutembelea blog hiyo inabidi ulipie kiasi hiko kidogo cha fedha. Kujua zaidi kuhusu KISIMA CHA MAARIFA bonyeza maandishi haya.

  Huduma hii inawafaa watu wote ambao wanataka kujifunza kuhusu kublog na waweze kufanya wenyewe.

  Unaweza kuwa kwenye huduma zote mbili ili kuweza kwenda haraka katika kuikuza blog yako.

  Kama upo tayari kuanza kunufaika na huduma hizi tafadhali tumia mawasiliano yafuatayo; 0717396253/0755953887, email; amakirita@gmail.com

  Karibu tufanye kazi pamoja ili uweze kukuza blog yako na uwe wa tofauti na kazi zako ziwe za thamani kubwa.