Ni mwaka wa pili sasa ambapo AMKA MTANZANIA imekuwa nawe bega kwa bega katika safari yako ya kufikia mafanikio katika maisha. Kupitia AMKA MTANZANIA na blog nyingine zilizopo chini ya AMKA CONSULTANTS umekuwa ukipata makala zenye mafunzo mbalimbali yenye lengo la kubadili maisha yako na kuwa bora zaidi.

Katika kipindi chote hiki baadhi ya wasomaji wamekuwa wakituandikia na kutupa ushuhuda ni jinsi gani AMKA MTANZANIA imebadili maisha yao. Shuhuda hizi zimekuwa hamasa kubwa sana kwa waandishi kupata msukumo wa kuandaa makala bora zaidi ili ziweze kuwasaidia wengi zaidi.

Leo tunaombakusikia kutoka kwako, tunaomba kusikia ni jinsi gani AMKA MTANZANIA imebadili maisha yako na kuwa bora zaidi.

Pia tungeomba kupata maoni yako ni jinsi gani tunaweza kuiboresha AMKA MTANZANIA ili iweze kuwasaidia wengi zaidi.

Ili kuweza kutupatia ushuhuda wako na maoni yako pia tafadhali bonyeza maandishi haya na jaza fomu. Ni zoezi fupi sana ambalo litakuchukua muda kidogo.

Kwa nini  ni muhimu wewe kutupatia ushuhuda na maoni yako?

Ni muhimu sana wewe kutupatia ushuhuda wako na hata maoni yako kwa sababu ushuhuda wako utawahamasisha waandishi wa AMKA MTANZANIA kuweza kufanya kazi zaidi. Na pia unaweza kutumika kama mfano katika kuwahamasisha wengi zaidi ili nao waweze kubadili maisha yao.

Pia huu ni mwisho wa mwaka hivyo tunafanya tathmini na kujipanga kwa ajili ya mwaka mpya 2015, maoni yako yatatusaidia sisi kuweza kukuhudumia wewe zaidi na hivyo uendelee kunufaika zaidi na zaidi.

Pia kwa wewe kutoa ushuhuda wako na hata maoni pia unakuwa umeshiriki katika kuwasaidia watu wengine nao kuboresha maisha yao.

Tunaamini kila mmoja wetu ana kitu ambacho anaweza kumsaidia mwingine. Anza sasa kwa kuwasaidia wengine kupata huduma bora sana kupitia AMKA MTANZANIA, unaweza kufanya hivyo kwa kubonyeza hapa na kuweka ushuhuda na maoni yako kwenye fomu itakayofunguka.

Wiki moja ya likizo.

Kwa mwaka mzima, kila siku ya wiki umekuwa ukipata makala mpya kwenye AMKA MTANZANIA. Ni makala ambazo zimeandaliwa vizuri kwa ajili ya kukuwezesha wewe kutoka hatua moja na kwenda hatua nyingine. Hii ni kazi kubwa sana ambayo inafanywa na waandishi na wahamasishaji wa AMKA MTANZANIA. Katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka AMKA MTANZANIA tutakuwa nalikizo ya wiki moja. Katika wiki hiyo hakutakuwa na makala mpya kwenye blog na hivyo utapewa vitu vya kujisomea kwenye wiki hiyo.

Likizo hii itawafanya waandishi wote kuweza kujipanga zaidi kwa mwaka ujao 2015 na miaka mingi inayokuja. Hii ni ili kuifanya AMKA MTANZANIA kuendelea kuwa chanzo kikubwa cha mabadiliko katika maisha yako na watu wengine wengi.

Semina ya siku 21 za mafanikio mwaka 2015.

AMKA MTANZANIA imekuandalia semina ambayo itaendeshwa kwa njia ya mtandao kwa siku 21, kuanzia tarehe 05/01/2015 mpaka tarehe 25/01/2015. Semina hii itakusaidia wewe katika kuweka malengo makubwa ambayo utayafikia na pia itakusaidia kuweza kubadili maisha yako na kuwa bora zaidi. Itakupa msingi ambao utaweza kuutumia kufanya mabadiliko makubwa kwa mwaka 2015.

Uandikishaji wa kushiriki kwenye semina hii unaendelea na mwisho ni tarehe 31/12/2014. Gharama ya semina hii ni tsh elfu kumi na nafasi za ushiriki ni chache ili kuweza kuwahudumia vizuri washiriki wote. Semina itaendeshwa kwa njia ya mtandao ambapo kila mshiriki atatumiwa email yenye mafunzo kwa kila siku ya semina. Kila mshiriki ataweza kuuliza swali na kupewa ufafanuzi zaidi kadiri ya mahitaji yake.

Kujiandikisha kwenye semina hii tuma ada ya ushiriki ambayo ni tsh 10,000/= kwenye namba 0717396253 au 0755953887 na kisha tuma ujumbe wenye jina lako na email yako.

Wahi kujiandikisha kabla ya nafasi kujaa na muda kuisha. Mafunzo haya hayatarudiwa tena kwa kipindi cha karibuni.

Nakutakia kila la kheri katika kuendelea kuboresha maisha yako. Kumbuka kutoa maoni yako ya kuboresha AMKA MTANZANIA na pia ushuhuda wako. Ni muhimu sana kwa maendeleo yetu sote, bonyeza maandishi haya na ujaze fomu.

TUPO PAMOJA.

kitabu-kava-tangazo4322