Kuanzia mwezi november mwaka huu 2015 kutafanyika maboresho zaidi kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Maboresho haya ni kuhakikisha wewe unapata maarifa bora zaidi yatakayokuwezesha wewe kuchukua hatua ya kuboresha kazi zako, biashara zako na hata maisha yako kwa ujumla. Kumbuka maarifa ni muhimu sana kwako kama unataka kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako. na maarifa haya hayapatikani kwingine bali kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
KUHUSU KISIMA CHA MAARIFA.
Kama wewe ni mgeni na hujui KISIMA CHA MAARIFA ni nini basi ni mtandao ambao unakupatia MAARIFA YA MAFANIKIO. Ndani ya kisima unapata mbinu zote muhimu za kukuwezesha kuwa na maisha bora na unayoyafurahia.
KISIMA CHA MAARIFA ni mtandao ambao unajiunga ndio uweze kupata makala hizo nzuri. Na kujiunga kuna uanachama wa aina mbili;
Aina ya kwanza ni SILVER MEMBER ambapo unapata nafasi ya kusoma makala zote kwenye KISIMA ISIPOKUWA ZA WORLD CLASS ambazo hizi ni makala zinazohusu mafanikio ya kiwango cha juu sana na kwa undani zaidi. Ada ya uanachama huu ni tsh elfu 30 kwa mwaka.
Aina ya pili ya uanachama ni GOLD MEMBER ambapo unapata nafasi ya kusoma makala zote kwenye KISIMA na pia unapata nafasi ya kuingia kwenye kundi la wasap ambapo ndani yake unajifunza mengi zaidi. Ada ya uanachama huu ni tsh elfu 50 kwa mwaka.
MABORESHO KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.
Makala zote za nyuma zitaendelea kupaikana na unaweza kuzisoma bila ya tatizo lolote.
Lakini kuanzia mwezi november mwaka huu 2015 kutakuwa na mabadiliko kwenye makala zinazopatikana kwenye KISIMA.
Makala hizi zitakuwa kama ifuatavyo;
Jumatatu; makala za biashara na ujasiriamali.
Jumatano; makala ya WORLD CLASS, hapa zitaingia makala zote za mafanikio, tabia za mafanikio, fedha na mengine mengi ambayo huwezi kuyapata sehemu nyingine.
Jumamosi; makala za uchambuzi wa vitabu, ambapo kila wiki utapata uchambuzi wa kitabu kimoja na pia utapata nafasi ya kupakua kitabu hiko na kujisomea zaidi wewe mwenyewe.
Jumanne na alhamisi kutakuwa kunapatikana makala za ONGEA NA COACH MAKIRITA, hizi zitakuwa zinakujia mara kwa mara na sio kila wiki. Na zitakuwa zinatokana na makala zinazotumwa kwa email.
Jumapili kunakuwa na makala za falsafa ya maisha, hizi nazo zinatumwa kwenye email kwa wale waliojiunga ili kutumiwa makala za falsafa.
Kila siku kunakuwa na makala za KURASA, hizi zitaendelea kupatikana kila siku na zinaweza kusomwa na yeyote.
KUNDI LA WASAP.
Kundi la wasap limekuwa likitumika kupeana maarifa na hamasa ili kufikia mafanikio zaidi. Pia kulikuwa na kipengele cha mjadala kila jumapili ambapo mara chache tulikuwa tunapata mtu wa kutushirikisha kile anachofanya na mafanikio aliyofikia.
Kwa sasa kwenye kundi hili kutakuwa na mabadiliko kidogo.
Kwanza kila siku asubuhi saa kumi na moja unaamshwa ili uianze siku yako mapema. Na unaianza siku yako kwa tafakai nzuri sana itakayoifanya siku yako iwe ya tofauti na ya kipekee. Hii ni kila siku, siku zote saba za wiki.
Pili kila jumapili saa 12 jioni mkapa saa 2 usiku kutakuwa na DARASA LA JUMAPILI ambapo kutakuwa na mada mbalimbali zinazohusu mafanikio ambazo zitafundishwa. Na zitafundishwa kwa njia ya mjadala ambapo kila mwanachama atapata nafasi ya kushiriki kwa kushirikisha uelewa wake kwenye mada husika na hata kuuliza maswali na kutoa mawazo yake. Kupitia darasa hili tutashirikishana mengi zaidi katika safari yetu ya mafanikio na hapa ndipo utaweza kuchota madini mengi zaidi kutoka kwa wana mafanikio wenzako.
Tatu ndani ya kundi hili utapata nafasi kwa siku yoyote na muda wowote kuuliza kitu ambacho ungependa kujua zaidi na pia kuwashirikisha wengine kitu ambacho wewe unakijua na ungependa wengine pia wakijue. Hiki kitakuwa kijiwe kizuri sana cha wana mafanikio kupeana yale muhimu ya mafanikio. Hivyo kila siku kati ya saa moja kamili usiku, mpaka saa mbili kamili usiku, kuondoa jumamosi na jumapili itakuwa ni muda wa mtu kushirikisha anachojua au kuuliza chochote ambacho angependa kujua.
Hupaswi kukosa nafasi ya kuwa kwenye kundi hili zuri na la kipekee.
HATUA YA WEWE KUCHUKUA.
Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kama bado hujafanya hivyo. Kujiunga unajaza fomu kisha unalipa ada ya mwaka, unaweza kulipa SILVER ambayo ni tsh elfu 30 kwa mwaka na kupata makala tu au unaweza kulipia GOLD ambayo ni tsh elfu 50 kwa mwaka na ukapata nafasi ya kusoma makala zote na pia kuingia kwenye kundi la wasap. Mimi binafsi nakushauri sana ujiunge kwa uanachama wa GOLD kwa sababu nafasi za kundi la wasap ni 100 tu na hakutakuwa na makundi zaidi ya moja. Lipo kundi moja tu ili niweze kuweka nguvu zangu zote hapo, likijaa hatutapokea tena wanachama wa GOLD, mpaka mwaka utakapoisha na labda mtu akawa hakulipia ada ndio utapata nafasi hiyo.
Hivyo nakushauri sana ujiunge kwa GOLD MEMBER, hutajutia.
Kuhusu gharama.
Ndio gharama hizi zipo chini ukilinganisha na thamani utakayopata. Na nimeziweka hivi chini ili kuhakikisha kila mtu anapata nafasi hii nzuri. Kwa sababu najua sio kitu ambacho kipo kwenye utamaduni wetu, kulipia ili kujifunza kitu ambacho sio lazima sana. Hivyo baadae gharama hizi zitakuja kuongezeka, ila usiwe na wasi wasi, jiunge leo hii.
KAA KWENYE KISIMA MWEZI MMOJA BURE.
Najua huenda una wasiwasi kama kweli kwa gharama utakayotoa utapata thamani inayoendana na gharama hiyo. Naomba nikutoe wasiwasi huo kwamba hutapoteza chochote.
Cha kufanya ni hivi, jiunge leo na GOLD MEMBER lipia ada, na kuwa kwenye kisima kwa mwezi mmoja, halafu niandikie ujumbe kama hujaridhishwa na unataka urudishiwe fedha yako. nakuhakikishia nitakurudishia fedha yako bila ya kukuuliza swali jingine lolote. Najaribu kujenga biashara zangu kwenye uaminifu wa hali ya juu sana, hivyo napenda kufanya kazi na watu ambao wanaridhika na kile wanachokipata. Ondoa shaka, hutapoteza chochote na una mengi sana ya kupata.
NAWEZA KULIPA KWA AWAMU?
Hapana, huwezi kufanya hivyo, unahitaji kulipa ada kamili. Sio kwamba sipendi kupokea malipo yako ya awamu, bali kwa uzoefu limetusumbua hilo. Nakupenda sana rafiki yangu, lipa ada kamili tuendelee kuwa pamoja.
KAMA TAYARI WEWE NI MWANACHAMA ZINGATIA HILI;
Kwa wale wanachama wa awali kabisa wa KISIMA CHA MAARIFA, walipata nafasi ya kukaa zaidi ya mwaka mmoja bila kulipia ada. Sasa kipindi kile kinaisha mwaka huu.
Nawakumbusha muanze kulipa ada zenu kwa sasa ili kuendelea kuwepo kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Mfumo tunaotumia unafuta uanachama moja kwa moja tarehe inapofika, kuepuka usumbufu fanya malipo yako ya uanachama mwezi mmoja kabla ya tarehe ya ukomo wa uanachama wako. Kwa wale wote waliojiunga na KISIMA CHA MAARIFA mwaka 2014 anza kulipa ada yako sasa ili uendelee kufurahia huduma za KISIMA CHA MAARIFA.
KUJIUNGA.
Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.
MALIPO.
Kufanya malipo ya ada ya KISIMA CHA MAARIFA tumia namba zifuatazo;
MPESA 0755 953 887
TIGO PESA 0717 396 253
AIRTEL MONEY – tuma airtel money kwenda tigo na tumia namba 0717396 253
Namba hizo za simu zinaleta jina AMANI MAKIRITA.
Kama upo nje ya nchi tuwasiliane kwa wasap kwenye namba +255 717 396 253 na nitakupa utaratibu wa kufanya malipo.
Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, hii ndio nyumba halisi ya mafanikio.