Malengo Matano (5) Muhimu Kwako Kuweka Mwaka 2016 Ili Uwe Na Maisha Bora Sana.

Kila mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka unaofuata, watu huzungumza sana kuhusu malengo. Mwisho wa mwaka watu wanazungumzia malengo waliyoweka kwa mwaka unaoisha. Wengi huwa hawajayafikia na hivyo kujikuta kwenye wakati mgumu, na wachache wanakuwa wameyafikia na hivyo kujisikia vizuri.

 
Mwanzo wa mwaka watu huzungumzia kuhusu kuweka malengo ya mwaka huo mpya. Hapa kila mtu anakuwa na matarajio makubwa kupitia malengo yale ambayo anaweka.
Pamoja na kila mtu kujihusisha na kuweka malengo kwa namna moja au nyingine, bado kumekuwa na changamoto nyingi sana katika uwekaji wa malengo.
Kwanza kabisa watu wanaposikia kuweka malengo, au wanapoweka malengo, huwa wanaangalia eneo moja tu kwenye maisha yao, na eneo hilo ni fedha. Kila malengo yanayowekwa huwa ya fedha au yanayohusiana na fedha. Hivyo mtu atapanga mwaka huu nataka kipato changu kiongezeke mpaka kufikia kiasi fulani, au mwaka huu nataka biashara yangu ikue zaidi, au mwaka huu nataka nipandishwe cheo kazini. Malengo mengi yanakuwa yanazunguka eneo hili la fedha.
Lakini maisha ni zaidi ya fedha, japokuwa fedha ndiyo inatupatia kila kitu muhimu kwenye maisha yetu, kuna vitu vingi sana ambavyo fedha haiwezi kununua. Hivi ni vitu ambavyo tunahitaji kuvifanyia kazi sisi wenyewe, na wala sio kwamba kwa kuwa na fedha basi vitu hivyo vnajitokeza.
Ili uweze kufanyia kazi vitu hivi muhimu ambavyo fedha haiwezi kununua ni lazima uviwekee malengo. Na ndio maana kwa mwaka huu unaoanza 2016 tunataka tushirikiane kwa pamoja, kuweka malengo ambayo yatakuwezesha wewe kuwa na maisha bora. Malengo ambayo yatagusa kila eneo la maisha yako na hivyo kufanikiwa kwa ujumla.
Ni vitu gani ambavyo fedha haiwezi kununua?
Vile vitu muhimu sana kwenye maisha yako, ambavyo huwa vinakuja bure kabisa, ila wewe unahitaji kuvifanyia kazi ndio viweze kuwa bora zaidi kwako. Hapa ni baadhi ya vitu hivyo muhimu.
1. Afya.
Afya ni muhimu sana kwako, na japokuwa unaweza kutibiwa kwenye hospitali kubwa na ya uhakika unapokuwa na fedha, ila afya njema umepewa bure kabisa, na kuifanya iendelee kuwa njema huhitaji fedha nyingi. Ukweli ni kwamba watu wengi wamekuwa hawaziwekei mkazo afya zao na hivyo kuzisahau na hii kupelekea afya hizo kuzorota. Na pale ambapo wanakuja kustuka wanakuta hawawezi tena kuboresha afya zao.
Kwa mfano kama mtu atawekeza nguvu zake kwenye kutafuta fedha, na kusahau kuweka afya yake vizuri, anaweza kuzipata fedha lakini akajikuta pia ana ugonjwa ambao hauwezi kutibika. Ugonjwa kama kisukari ambao utamsumbua mtu kwa muda mrefu sana na hautampa uhuru wa kufurahia mafanikio yake mengine. Afya ni muhimu, na ipo bure, ni wewe kuiwekea malengo.
2. Mahusiano.
Ikiwa utaweka malengo na mipango mizuri sana katika kutafuta fedha, na ukasahau yale mahusiano muhimu sana kwako hata kama utafikia mafanikio hayo ya kifedha bado hutaweza kuyafurahia. Mahusiano ni muhimu sana kwako na hapa yapo mahusiano ya kifamilia, ndugu jamaa na marafiki na hata wale watu unaokutana nao kwenye shughuli zao za kila siku.
Unalipa shilingi ngapi ili kujenga mahusiano yako na familia au marafiki zako? Hakuna gharama ya fedha, ila unahitaji kufanyia kazi mahusiano hayo kama unataka yawe bora. Na huwezi kuyafanyia kazi kama hujaweka malengo ya mahusiano.
3. Wewe binafsi.
Huwa tunasema fedha haimbadilishi mtu, bali inatuonesha uhalisia wa yule mtu. Maana watu wengi huwa wanasema watu wakipata fedha huwa wanabadilika. Ukweli ni kwamba watu hawabadilishi na fedha, ila wanapokuwa na fedha wanakuwa na nafasi kubwa ya kufanya mengi ambayo yataonekana kwa urahisi.
Hivyo pamoja na malengo ya kifedha utakayoweka, ni lazima uweke malengo yako wewe binafsi, unataka kuwa mtu wa aina gani, unataka kutoa mchango gani kwa jamii inayokuzunguka na pia unataka kuacha alama gani utakapoondoka hapa duniani. Yote haya haijalishi ni fedha kiasi gani unazo, bali inajalisha ni jinsi gani umepanga kupeleka maisha yako.
Hayo ni mambo matatu muhimu sana kwa mafanikio yako ambayo umekuwa hupati nafasi ya kuyafanyia kazi kwa undani, na hivyo kuona maisha yako bado sio bora licha ya kuweka juhudi na kupata kipato kizuri.
Wahi nafasi hii ya kuweza kuweka malengo bora sana kwako.
Ili kuhakikisha wewe unafanikiwa kama mtu, yaani kwa ujumla na sio eneo la fedha tu, AMKA CONSULTANTS tumekuandalia semina ya mwaka 2016 ambayo itakuwezesha wewe kuweka malengo matano muhimu sana kwenye maisha yako ili uweze kufikia mafanikio makubwa. Malengo hayo ni katika mambo hayo matatu tuliyojadili hapo juu ukiongeza fedha na kazi au biashara yako.
Katika semina hii utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kuweka malengo haya, na kuyafanyia kazi mpaka pale ambapo utayafanikisha.
Kwa kushiriki semina hii utaondoka na kitu cha kufanyia kazi kwa mwaka 2016 na mwaka huo ukawa wa tofauti sana kwako.
Semina hii inafanyika kwa njia ya mtandao kwa kutumiwa email za masomo na pia kuwa kwenye kundi la wasap. Katika semina hii kila siku utakuw ana kitu cha kufanyia kazi kwenye maisha yako na hivyo kuweka malengo ambayo yatakusukuma mbele zaidi.
Semina hii itafanyika kwa siku kumi na itaanza tarehe 04/01/2016.
Ada ya kushiriki semina hii ni tsh elfu 20 (20,000/=), ila kwa wale ambao ni wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA GOLD hawatahitajika kulipa ada hiyo.
Ili kupata nafasi ya kushiriki fungua maandishi haya na ujaze fomu. Hata kwa wale wanachama wa KISIMA GOLD pia fungua fomu na ujaze taarifa zako.
Baada ya kujaza fomu tuma ada ya kushiriki mafunzo haya ambayo ni tsh 20,000/= kwenye namba zifuatazo; MPESA 0755 953 887, TIGO PESA AU AIRTEL MONEY 0717 396 253. Kwenye kutuma jina litakuja AMANI MAKIRITA.
Chukua hatua mara moja ya kujiunga na semina hii bora sana ili kufanya mwaka 2016 kuwa bora sana kwako.
Wahi kujiunga na kulipia kwa sababu nafasi za kushiriki semina hii ni chache, hii ni ili kuhakikisha wanaoshiriki wanapata thamani kubwa sana.
Nakutakia kila la kheri kwa mwaka 2016, na nakukaribisha sana kwenye semina hii.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
AMKA CONSULTANTS

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: