Watu wengi wamekuwa wakiahidi mambo mengi sana kwenye biashara zao.
Kuna wale ambao wamekuwa wakiahidi kuingia kwenye biashara na siku zinakwenda ila hawaingii.
Na kuna wale ambao wamekuwa wakiweka mipango mizuri na bora kwa biashara ila hawafikii utekelezaji wa mipango hiyo.
Ukweli ni kwamba kuahidi au kupanga ni sehemu ndogo sana ya biashara. Na kuwa wazi kabisa siyo biashara.
Biashara ni kile unachofanya, kile unachotoa, ile huduma au bidhaa unayotoa, ambayo inatatua matatizo ya watu.
Kitu kingine nje ya hapo siyo biashara, ni michakato mingine tu.
Jua kipi unachofanya ni biashara na kipi ni michakato tu.
Fanya biashara, toa huduma au bidhaa ambazo zina manufaa kwa wengine.
Kila la kheri.
Kama una changamoto yoyote ya kibiashara ambayo ungependa tuijadili hapa iweke kwenye maoni hapo chini.
-
Pingback: UKURASA WA 502; Kuweza Kufanya Na Kufanya…. | Kisima Cha Maarifa