Habari rafiki?
Karibu kwenye utaratibu wetu wa kujisomea vitabu, ambapo kila mwezi unapatiwa kitabu cha kujisomea. Na utaratibu huu umeboreshwa sana kwa sasa ambapo kila mwezi msomaji anapatiwa kitabu cha kiswahili cha kujisomea. Hapo awali vitabu vilikuwa ni kwa lugha ya kiingereza na hivyo wale ambao hawaielewi lugha hii hawakupata fursa hii nzuri ya kujifunza kila mwezi kwa kujisomea kitabu.
 
Sasa kila mwezi utapatiwa kitabu kizuri cha kujisomea ambacho kitakupatia maarifa na hamasa ya wewe kuchukua hatua ili kuwa na maisha bora na ya mafanikio.
Mwezi huu wa tano tunakwenda kusoma kitabu; BIASHARA NDANI YA AJIRA, Jinsi Ya Kuanzisha Na Kukuza Biashara Yako Ukiwa Bado Umeajiriwa. Hiki ni kitabu ambacho kinakupa wewe mbinu za kuweza kufanya biashara wakati bado umejiriwa. Hili limekuwa changamoto kwa wengi na biashara nyingi zinazoanzishwa na waajiriwa zimekuwa zikishindwa kukua au hata kufa kabisa.

 
Kitabu hiki kimechambua kwa undani mambo yote ya kuzingatia katika kufanya biashara ukiwa kwenye ajira. Pia kuna aina za biashara unazoweza kuanza kufanya ukiwa kwenye ajira. Kuna aina za uwekezaji unazoweza kufanya ukiwa upo kwenye ajira.
Kingine kizuri sana utakachojifunza kwenye kitabu hiki ni MIFEREJI NANE YA KIPATO unayotakiwa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha, na jinsi ya kujijengea mfereji hii. Na pia utajifunza mbinu za kuilinda kazi yako dhidi ya mkataba wako wa ajira na hata majungu ya wafanyakazi wenzako hasa pale biashara yako itakapoanza kuonesha mafanikio. 

YALIYOMO KWENYE KITABU HIKI

 
JINSI YA KUPATA KITABU HIKI;
Kitabu kinatumwa kama nakala tete yaani softcopy kwenye mfumo wa pdf. Kwa mfumo huu unaweza kusoma kitabu hiki kwenye simu yako kama ina uwezo wa kusoma vitabu na pia unaweza kusoma kwa kutumia kompyuta.
Kupata sura mbili za kitabu hiki na kuanza kukisoma sasa bonyeza maandishi haya na kupakua kitabu. Ili kupata kitabu kizima fuata utaratibu uliopo hapo chini.
 
Unatumiwa kitabu hiki kwa njia tatu, utachagua ile unayotaka wewe;
1. Kwa njia ya wasap, unaweza kutumiwa kwenye namba yako ya wasap na ukapakua kusoma.
2. Kwa njia ya telegram, pia unaweza kutumiwa kwenye namba yako ya telegram na ukapakua kusoma.
3. Kwa njia ya email, unaweza kutumiwa kitabu hiki moja kwa moja kwenye email yako.
Gharama ya kitabu hiki ni shilingi za Kitanzania elfu kumi tu (tsh 10,000/=). Ili kupata kitabu hiki tuma fedha kwenye namba zifuatazo;
1. Kama unatumia M- PESA tuma kwenda namba 0755 953 887 (jina AMANI MAKIRITA)
2. Kama unatumia TIGO PESA au AIRTEL MONEY tuma kwenda namba 0717 396 253 (jina AMANI MAKIRITA)
3. Kama upo nje ya Tanzania tuwasiliane kwa wasap 0717 396 253 au email na nitakupa utaratibu mzuri wa kulipia kulingana na ulipo. 16
Ukishatuma malipo ya kitabu, tuma ujumbe wa kawaida au wasap kwenda namba 0717 396 253 wenye jina la kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA na utatumiwa kitabu hiki kizuri. 
 
Karibu sana rafiki yangu, ujipatie kitabu hiki ambacho kitakuwezesha kuanzisha na kukuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa.
Kama bado hujapata sura mbili za mwanzo za kitabu hiki zisome kwa kupakua kitabu hiki. Bonyeza maandishi haya na utapakua kitabu hiki na uanze kusoma.
TUPO PAMOJA,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.