Habari za leo rafiki?

Watu wamekuwa wanasema muda ni fedha, na hilo ni kosa kubwa sana wanalofanya kwenye maisha yao, linalowapelekea wao kushindwa kutumia muda wao vizuri.

Muda siyo fedha, kwa sababu moja muhimu, poteza fedha na utaweza kupata nyingine, lakini poteza muda na hutaweza kuupata tena kwenye maisha yako.

Muda ni rasilimali pekee ambayo ina ukomo kwenye maisha yetu. Ni rasilimali ambayo hatuwezi kuipata zaidi, tunaweza kutumia kwa kiasi kilichopo na hatuwezi kuzidisha hata kiasi kidogo.

Changamoto za muda zimekuwa ni nyingi kwa kila kizazi. Lakini kwa kizazi chetu, changamoto zimekuwa kubwa zaidi. Hii ni kutokana na mambo ya kufanya kuwa yanaongezeka kila siku, lakini muda wetu ni ule ule. Yaani pamoja na kuja kwa mitandao ya kijamii na teknolojia nyingine, bado tuna masaa 24 pekee kwa siku.

Hii ina maana kwamba, kwa chochote unachochagua kufanya kwenye muda wako, maana yake pia unakuwa umechagua kuacha kufanya kitu kingine. Je kati ya unachofanya na unachoacha kufanya, kipi muhimu?

Kwenye somo letu hili la leo, nimekushirikisha mambo matatu muhimu ya kufanya ili uweze kutawala muda wako, na kuweza kufanya makubwa. Katika somo hili nimekupa mbinu za kuweza kupangilia muda wako na kuweza kuweka vipaumbele muhimu kwako.

Kuna njia moja ya kusimamia muda ya kuwa na vipaumbele kwenye makundi A, B C na D. Kwenye somo hili nimekushirikisha namna ya kupanga vipaumbele vyako kwenye makundi hayo manne. Na kundi moja kati ya hayo, unapaswa kulifuta kabisa. Angalia somo hili kujua zaidi.

Mwisho kabisa, kuna muda ambao umekufa, kwa kizungu tunaweza kusema DEAD TIME. Huu ni muda ambao lazima upotee, yaani upo kwenye mazingira ambayo huna namna lazima tu muda uende, labda kama upo kwenye foleni. Hakuna namna ya kuondoka pale. Sasa huo ni muda bora kabisa kwenye amisha yako, ni muda ambao unaweza kuutumia kufanya makubwa kwenye amisha yako. Kwenye somo la leo nimeeleza kwa kina namna ya kutumia muda huu.

Nisikuweke hapa muda mwingi rafiki, bali ingia kwenye somo letu la leo, uweze kujifunza na kuanza kutawala muda wako leo.

Angalia somo hili zuri la leo kuhusu muda kwa kubonyeza maandishi haya. Pia unaweza kuangalia somo hili moja kwa moja hapo chini kama kifaa chako kinaruhusu.

Rafiki, nimekuwa nakusisitiza jambo moja, nakushirikisha mafunzo mengi, lakini kama hutachukua hatua, haya yote yatakuwa ni kazi bure. Hivyo nakusihi sana uchukue hatua ili uweze kufanikiwa. Na kama utapenda tuwe karibu zaidi, tujifunze kwa pamoja na niwe kocha wako, karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Kujiunga, nitumie ujumbe kwa wasap namba 0717396253 wenye neno KISIMA CHA MAARIFA na nitakupa maelekezo.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,


Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.